bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 44
Isaiah 44
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 43
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 45 →
1
“Sikiliza ewe taifa Israeli mtumishi wangu; sikiliza ewe kizazi cha Yakobo mteule wangu.
2
Mimi, Mwenyezi-Mungu Muumba wako, niliyekufanya tangu tumboni mwa mama yako, nimekuja kukusaidia wewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Usiogope, ewe taifa la Yakobo, mtumishi wangu, naam, usiogope ewe Yeshuruni mteule wangu.
3
“Nitaimwagilia maji nchi iliyokauka, na kutiririsha mto katika nchi kame. Nitawamiminia roho yangu wazawa wako, nitawamwagia watoto wako baraka yangu.
4
Watachipua kama nyasi penye maji mengi, kama majani kandokando ya vijito.
5
“Mmoja atasema: ‘Mimi ni wa Mwenyezi-Mungu’, mwingine atajiita kwa jina la Yakobo, mwingine ataandika mkononi mwake, ‘Wa Mwenyezi-Mungu’, na kujitambulisha kwa jina la Israeli.”
6
Mwenyezi-Mungu, Mfalme na Mkombozi wa Israeli, naam, Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Mimi ni wa kwanza na wa mwisho; hakuna Mungu mwingine ila mimi.
7
Ni nani Mungu aliye kama mimi? Mwache atangaze na kusema wazi mbele yangu. Nani alitangaza hapo kale mambo ambayo yatatukia? Na watuambie yale ambayo bado kutokea.
8
Enyi watu wangu, msiogope wala msiwe na hofu, Je, sikuwaambia tangu zamani mambo yatakayotokea? Nyinyi ni mashahidi wangu. Je, yuko Mungu mwingine ila mimi? Je, kuna mwenye nguvu mwingine? Huyo simjui!”
9
Watu wote wanaotengeneza sanamu za miungu ni bure kabisa; na vitu hivyo wanavyovifurahia haviwafai chochote. Wanaoshuhudia hiyo miungu ya uongo ni vipofu na wajinga. Kwa hiyo hao wataaibishwa!
10
Ajabu ya mtu kutengeneza sanamu au kinyago cha mungu ambaye hawezi kumsaidia chochote!
11
Hakika wote wanaomheshimu wataaibishwa, tena hao mafundi wa sanamu ni binadamu tu. Basi, wakutane wote, wajitokeze, nao watatishika na kuaibishwa.
12
Mfuachuma huchukua madini, akayayeyusha motoni na kufua sanamu. Huigongagonga kwa nyundo ili kuipa umbo kwa mikono yake yenye nguvu. Wakati wote huo yeye huona njaa na kuchoka; huona kiu na nguvu kumwishia.
13
Kadhalika naye seremala hupima kipande cha mbao, akakitia alama kwa kalamu yake, kisha kwa vifaa vyake hukichonga na kukipa umbo la binadamu na sura ya kupendeza; kisha akaiweka sanamu hiyo ya mungu mahali pake pa pekee.
14
Mtu hukata mti wa mwerezi ili autumie, au huchagua mberoshi au mwaloni. Huuacha ukue kati ya miti ya msituni. Au hupanda mwerezi na mvua huustawisha.
15
Sehemu ya mti huo itatumiwa kama kuni; mtu huota moto wake na kuoka mikate yake juu yake. Sehemu nyingine ya mti huohuo, mtu hujichongea sanamu ya mungu, akainakshi, halafu akaiabudu.
16
Kisha huchukua kuni zake akaoka nazo moto, akachoma nyama juu yake, akala, akashiba. Halafu hukaa hapo akiota moto na kusema, “Naam! Ama kweli nimepata joto! Huo ndio moto!”
17
Sehemu iliyobaki ya mti huohuo, hujichongea sanamu ya mungu, kinyago chake, kisha huisujudia na kuiabudu. Huiomba akisema, “Wewe ni mungu wangu, niokoe!”
18
Watu hao hawajui wala hawaelewi kitu chochote. Wamefumbwa macho wasiweze kuona; kadhalika na akili zao wasiweze kufahamu.
19
Hakuna awezaye kutafakari; au kuwa na akili na kufikiri na kusema: “Nusu ya mti huo niliwashia moto; tena nikaoka mikate juu ya makaa yake, nikachoma nyama, nikala. Je, sehemu iliyobaki nitatengeneza sanamu ambayo ni chukizo na kukisujudia hicho kipande cha mti?”
20
La! Fikira zake zimeambatana na hicho ambacho ni majivu tu! Mtu huyo amepotoka hata hawezi kujiokoa mwenyewe na kusema: “Kweli ninachoshika mkononi ni udanganyifu mtupu!”
21
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ewe taifa la Yakobo kumbuka; naam, kumbuka ewe Israeli: Wewe ni mtumishi wangu. Nilikuumba ili uwe mtumishi wangu, nami kamwe sitakusahau.
22
Nimeyafagilia mbali makosa yako kama wingu, nimezifanya dhambi zako zitoweke kama ukungu. Rudi kwangu maana mimi nimekukomboa.”
23
Imbeni kwa furaha enyi mbingu, kwa sababu ya hayo aliyotenda Mwenyezi-Mungu. Pazeni sauti enyi vilindi vya dunia! Imbeni kwa furaha enyi milima! Enyi misitu na miti yote iliyomo, imbeni. Maana Mwenyezi-Mungu amewakomboa wazawa wa Yakobo, naye atatukuka katika nchi ya Israeli.
24
Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wako, aliyekuumba tangu tumboni mwa mama yako, asema: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyeumba vitu vyote. Mimi peke yangu nilizitandaza mbingu, niliiumba dunia kwa nguvu yangu mwenyewe!
25
Mimi huzivuruga ishara za watabiri waongo na kuwapumbaza waaguzi. Mimi huyakanusha maneno ya wenye hekima na kufanya ujuzi wao kuwa upumbavu.
26
Lakini huuthibitisha ujumbe wa mtumishi wangu, na kukamilisha maaguzi ya wajumbe wangu. Mimi ndimi niuambiaye mji wa Yerusalemu: Wewe Yerusalemu, utakaliwa tena na watu. Na miji ya Yuda: Nyinyi mtajengeka tena: Magofu yenu nitayarekebisha tena.
27
Mimi ndimi ninayeviamuru vilindi: Kaukeni.
28
Ndimi nimwambiaye Koreshi: Wewe utawachunga watu kwa niaba yangu. Wewe utatekeleza mipango yangu yote. Ndimi ninayesema kuhusu Yerusalemu: Wewe Yerusalemu utajengwa tena upya; na juu ya hekalu: Msingi wako utawekwa tena.”
← Chapter 43
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 45 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66