bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 57
Isaiah 57
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 56
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 58 →
1
Mtu mwadilifu akifa, hakuna mtu anayejali; mtu mwema akifariki, hakuna mtu anayefikiri na kusema: “Mtu huyo mwema ameondolewa asipatwe na maafa,
2
ili apate kuingia kwenye amani.” Watu wanaofuata njia ya haki, watakuwa na amani na kupumzika.
3
Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Njoni hapa nyinyi wana wa wachawi; nyinyi wazawa wa wachawi, wazinzi na malaya.
4
Je, mnadhani mnamdhihaki nani? Mnamfyonya nani na kumtolea ulimi? Nyinyi wenyewe ni wahalifu tangu mwanzo, nyinyi ni kizazi kidanganyifu.
5
Nyinyi mnawaka tamaa kwenye miti ya mialoni, na katika kila mti wa majani mabichi. Mnawachinja watoto wenu na kuwatambika katika mabonde na nyufa za majabali.
6
Mnachagua mawe laini mabondeni, na kuyafanya kitovu cha maisha yenu. Mnayamiminia tambiko ya kinywaji na kuyapelekea tambiko ya nafaka! Je, mimi nitaridhishwa kwa vitu hivyo?
7
Mmeweka vitanda vyenu juu ya milima mikubwa, na kwenda huko kutoa tambiko.
8
Nyuma ya milango na miimo mmetundika kinyago chenu. Nyinyi mnaniacha mimi na kutandika na kuvipanua vitanda vyenu. Mnafanya mapatano na hao mliopenda vitanda vyao. Humo mnazitosheleza tamaa zenu mbaya, huku mnakodolea macho kinyago chenu.
9
Mnajitia marashi na manukato kwa wingi kisha mnakwenda kumwabudu Moleki. Mnawatuma wajumbe wenu huko na huko, kujitafutia miungu ya kuabudu; hata kuzimu walifika.
10
Mlichoshwa na safari zenu ndefu, hata hivyo hamkukata tamaa; mlijipatia nguvu mpya, ndiyo maana hamkuzimia.
11
“Mlimwogopa na kutishwa na nani hata mkasema uongo, mkaacha kunikumbuka mimi na kuacha kabisa kunifikiria? Mimi sikuwaambia kitu kwa muda mrefu; ndio maana labda mkaacha kuniheshimu!
12
Mnafikiri mnafanya sawa, lakini nitayafichua matendo yenu, nayo miungu yenu haitawafaa kitu.
13
Mtakapolia kuomba msaada, rundo la vinyago vyenu na liwaokoe! Upepo utavipeperushia mbali; naam, pumzi itavitupilia mbali. Lakini watakaokimbilia usalama kwangu, wataimiliki nchi, mlima wangu mtakatifu utakuwa mali yao.”
14
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Jengeni! Jengeni! Tayarisheni njia! Ondoeni vikwazo vyote njiani mwa watu wangu!”
15
Hivi ndivyo asemavyo Mungu aliye juu kabisa, aishiye milele na ambaye jina lake ni “Mtakatifu”: “Mimi nakaa huko juu, mahali patakatifu, nakaa pia na wenye majuto na wanyenyekevu. Mimi nitawatia moyo walio wanyenyekevu na kuwapa nguvu wenye majuto.
16
Maana sitaendelea kuwalaumu wala kuwakasirikia daima. La sivyo hao niliowaumba watadhoofika mbele yangu, nami ndiye niliyewapa pumzi yangu ya uhai.
17
Niliwakasirikia kwa sababu ya uovu na tamaa zao; niliwaadhibu, nikauficha uso wangu na kukasirika. Lakini wao waliendelea kufuata njia zao wenyewe.
18
Niliiona mienendo yao, lakini nitawaponya; nitawaongoza na kuwapa faraja, nitawatuliza hao wanaoomboleza.
19
Mimi nitawapa amani, amani kwa walio mbali na walio karibu! Mimi nitawaponya.
20
Lakini waovu ni kama bahari iliyochafuka, ambayo haiwezi kutulia; mawimbi yake hutupa tope na takataka.”
21
Mungu wangu asema hivi: “Watu waovu sitawapa amani.”
← Chapter 56
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 58 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66