bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 32
Isaiah 32
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 33 →
1
Kutatokea mfalme atakayetawala kwa uadilifu, nao viongozi wataongoza kwa kufuata haki.
2
Kila mmoja atakuwa kama mahali pa kujikinga na upepo, kama mahali pa kujificha wakati wa tufani. Watakuwa kama vijito vya maji katika nchi kame, kama kivuli cha mwamba mkubwa jangwani.
3
Macho hayatafumbwa tena, masikio yatabaki wazi.
4
Wafanyao mambo kwa hamaki wataamua kwa busara, wenye kigugumizi wataongea sawasawa.
5
Wapumbavu hawataitwa tena waungwana, wala walaghai hawataitwa tena waheshimiwa.
6
Wapumbavu hunena upumbavu, na fikira zao hupanga kutenda uovu, kutenda mambo yasiyo mema, kusema mambo ya kumkufuru Mwenyezi-Mungu. Huwaacha wenye njaa bila chakula, na wenye kiu huwanyima kinywaji.
7
Ulaghai wa walaghai ni mbaya; hao huzua visa viovu, na kumwangamiza maskini kwa maneno ya uongo, hata kama madai ya maskini ni halali.
8
Lakini waungwana hutenda kiungwana, nao hutetea mambo ya kiungwana.
9
Inukeni, enyi wanawake mnaostarehe, mnisikilize; sikilizeni ninayosema enyi mabinti mlioridhika.
10
Katika mwaka mmoja hivi mtatetemeka nyinyi mliotosheka; maana hamtapata mavuno yoyote, na mavuno ya zabibu yatatoweka.
11
Tetemekeni kwa woga, enyi mnaojikalia tu; tetemekeni kwa hofu, enyi mnaostarehe! Vueni nguo zenu, mbaki uchi, mjifunge vazi la gunia viunoni mwenu.
12
Jipigeni vifua kwa huzuni, ombolezeni, kwa sababu ya bustani zilizokuwa nzuri, kwa mizabibu iliyokuwa ikizaa sana,
13
kwa ardhi ya watu wangu inayoota miiba na mbigili, kwa nyumba zote zilizojaa watu wenye furaha, kwa mji uliokuwa na shangwe.
14
Maana ikulu ya mfalme itaachwa mahame, mji huo wa watu wengi utahamwa. Mlima na mnara wa ulinzi utakuwa mapango milele, pundamwitu watapitapita huko kwa furaha, kondoo watapata malisho yao humo.
15
Hali itaendelea kuwa hivyo mpaka tumiminiwe roho ya Mungu kutoka juu. Hapo jangwa litakuwa shamba la rutuba tena, na mashamba ya rutuba yatakuwa msitu.
16
Haki itadumu katika nchi iliyokuwa nyika, uadilifu utatawala katika mashamba yenye rutuba.
17
Kutokana na uadilifu watu watapata amani, utulivu na usalama utadumu milele.
18
Watu wangu watakaa katika makao ya amani, katika maskani salama na mazingira matulivu.
19
Msitu wa adui utatoweka kabisa, na mji wake utaangamizwa.
20
Lakini heri yenu nyinyi: Mtapanda mbegu zenu popote penye maji, ng'ombe na punda wenu watatembeatembea watakavyo.
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 33 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66