bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 23
Isaiah 23
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 24 →
1
Kauli ya Mungu dhidi ya Tiro. Ombolezeni, enyi mabaharia wa mbali baharini, maana Tiro mji wenu umeharibiwa, humo hamna tena makao wala bandari. Mtazipokea habari hizo mtakaporejea kutoka Kupro.
2
Nyamazeni kwa mshangao enyi wakazi wa pwani, naam, tulieni enyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao wajumbe wenu wanapita baharini,
3
wakasafiri katika bahari nyingi. Mapato yenu yalikuwa nafaka ya Misri, mkaweza kufanya biashara na mataifa.
4
Aibu kwako ewe Sidoni, mji wa ngome kando ya bahari! Bahari yenyewe yatangaza: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa, wala sijawahi kuzaa; sijawahi kulea wavulana, wala kutunza wasichana!”
5
Habari zitakapoifikia Misri kwamba Tiro imeangamizwa, Wamisri watafadhaika sana.
6
Ombolezeni enyi wenyeji wa Foinike! Jaribuni kukimbilia Tarshishi.
7
Je, huu ndio mji wa furaha wa Tiro, mji ambao ulijengwa zamani za kale, ambao wakazi wake walikwenda kumiliki nchi za mbali?
8
Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro, mji uliowatawaza wafalme, wafanyabiashara wake walikuwa wakuu, wakaheshimiwa duniani kote?
9
Ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote. Alifanya hivyo akiharibu kiburi chao na kuwaaibisha waheshimiwa wake.
10
Limeni sasa ardhi yenu enyi wakazi wa Tarshishi; maana hamna tena bandari kwa ajili ya meli kubwa.
11
Mwenyezi-Mungu ameunyosha mkono wake juu ya bahari, amezitetemesha falme; ametoa amri kuziharibu ngome za Kanaani.
12
Alisema: “Ewe binti Sidoni hutaweza kufanya sherehe tena; hata ukikimbilia Kupro, huko nako hutapata pumziko!”
13
(Ni Wakaldayo, wala si Waashuru, waliowaacha wanyama wa porini wauvamie mji wa Tiro. Wao ndio waliouzungushia mji huo minara ya kuushambulia, wakayabomoa majumba yake na kuufanya magofu.)
14
Pigeni yowe enyi meli za Tarshishi, maana kimbilio lenu limeharibiwa.
15
Hapo mji wa Tiro utasahaulika kwa muda wa miaka sabini, muda wa maisha ya mfalme. Baada ya miaka hiyo sabini, mji wa Tiro utakumbwa na kile watu wanachoimba juu ya malaya:
16
“Twaa kinubi chako uzungukezunguke mjini, ewe malaya uliyesahaulika! Imba nyimbo tamutamu. Imba nyimbo nyinginyingi ili upate kukumbukwa tena.”
17
Baada ya miaka hiyo sabini, Mwenyezi-Mungu atauadhibu mji wa Tiro, nao utarudia kufanya uzinzi kwa kujiuza kwa mataifa yote ya dunia.
18
Fedha utakayopata itawekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Mji wenyewe hautafaidika kwa fedha hiyo ila wale wanaomwabudu Mwenyezi-Mungu wataitumia kununulia chakula kingi na mavazi mazuri.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66