bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 33
Isaiah 33
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 34 →
1
Ole wako ewe mwangamizi, unayeangamiza bila wewe kuangamizwa! Ole wako wewe mtenda hila, ambaye hakuna aliyekutendea hila! Utakapokwisha kuangamiza wewe utaangamizwa! Utakapomaliza kuwatendea watu hila wewe utatendewa hila.
2
Ee Mwenyezi-Mungu, utuonee huruma, kwako tumeliweka tumaini letu. Uwe kinga yetu kila siku, wokovu wetu wakati wa taabu.
3
Kwa kishindo cha sauti yako watu hukimbia; unapoinuka tu, mataifa hutawanyika.
4
Maadui zao wanakusanya mateka, wanayarukia kama panzi.
5
Mwenyezi-Mungu ametukuka, yeye anaishi juu mbinguni. Ameujaza Siyoni haki na uadilifu.
6
Enyi watu wa Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu atawajalieni usalama, atawaokoa na kuwapa hekima na maarifa. Hazina yenu kuu ni kumcha Mwenyezi-Mungu.
7
Haya, mashujaa wao wanalia, wajumbe wa amani wanaomboleza.
8
Barabara kuu zimebaki tupu; hamna anayesafiri kupitia humo. Mikataba inavunjwa ovyo, mashahidi wanadharauliwa. Hamna anayejali tena maisha ya binadamu.
9
Nchi inaomboleza na kunyauka; misitu ya Lebanoni imekauka, bonde zuri la Sharoni limekuwa jangwa, huko Bashani na mlimani Karmeli miti imepukutika majani yake.
10
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Sasa mimi nitainuka; sasa nitajiweka tayari; sasa mimi nitatukuzwa.
11
Mipango yenu yote ni kama makapi, na matokeo yake ni takataka tupu. Pumzi yangu itawaangamiza kama moto.
12
Watu watakuwa kama wamechomwa kuwa majivu, kama miiba iliyokatwa na kuteketezwa motoni.
13
Sikilizeni mambo mliyofanya enyi mlio mbali, nanyi mlio karibu kirini uwezo wangu.”
14
Wenye dhambi katika Siyoni wanaogopa, wasiomcha Mungu wanatetemeka na kusema: “Nani awezaye kuukaribia moto huu mkali? Nani awezaye kustahimili miali ya moto wa milele?”
15
Ni mtu aishiye kwa uadilifu na asemaye ukweli; mtu anayedharau kabisa utajiri wa dhuluma, anayekataa hongo kata kata, asiyekubali kamwe kusikia mipango ya mauaji, wala hakubali macho yake yaone maovu.
16
Mtu wa namna hiyo anaishi juu, mahali salama penye ngome na miamba; chakula chake atapewa daima, na maji yake ya kunywa hayatakosekana.
17
Mtaweza kumwona mfalme katika fahari yake, mtaiona nchi anayotawala, kubwa na pana.
18
Mtafikiria tisho lililopita na kujiuliza, “Wako wapi wale waliokadiria na kukisia kodi? Wako wapi wale waliopeleleza ulinzi wetu?”
19
Hamtawaona tena watu wale wenye kiburi, wanaozungumza lugha isiyoeleweka.
20
Tazameni Siyoni tunamofanya sikukuu zetu; tazameni mji Yerusalemu, makao matulivu, hema imara; vigingi vyake havitangolewa kamwe, kamba zake hazitakatwa hata moja.
21
Humo Mwenyezi-Mungu atatuonesha ukuu wake. Kutakuwa na mito mikubwa na vijito, ambamo meli za vita hazitapita, wala meli kubwa kuingia.
22
Maana Mwenyezi-Mungu ni hakimu wetu, yeye ni mtawala wetu; Mwenyezi-Mungu ni mfalme wetu, yeye ndiye anayetuokoa.
23
Ewe Siyoni, kamba zako zimelegea, haziwezi kushikilia matanga yake, wala kuyatandaza. Lakini nyara nyingi zitagawanywa; hata vilema wataweza kuchukua sehemu yao.
24
Hakuna atakayesema tena ni mgonjwa; watu watasamehewa uovu wao wote.
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 34 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66