bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 3
Isaiah 3
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 4 →
1
Sasa, Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataondoa kutoka Yerusalemu na Yuda kila tegemeo: Tegemeo lote la chakula, na tegemeo lote la kinywaji.
2
Ataondoa mashujaa na askari, waamuzi na manabii, waaguzi na wazee,
3
majemadari wa vikosi vya watu hamsini, na watu wenye vyeo, washauri, wachawi stadi na walozi hodari.
4
Mungu ataweka watoto wawatawale; naam, watoto wachanga watawatawala.
5
Watu watadhulumiana, kila mtu na jirani yake; vijana watawadharau wazee wao, na watu duni watapuuza wakuu wao.
6
Wakati huo ndugu atamwambia ndugu yake wakiwa bado nyumbani kwa baba yao: “Wewe unalo koti; utakuwa kiongozi wetu. Chukua hatamu juu ya uharibifu huu!”
7
Lakini siku hiyo atasema, “Mimi siwezi kuwa mwuguzi, nyumbani mwangu hamna chakula wala mavazi. Msinifanye mimi kuwa kiongozi wenu.”
8
Watu wa Yerusalemu wamejikwaa, watu wa Yuda wameanguka, kwa kuwa wanampinga Mwenyezi-Mungu kwa maneno na matendo, wakipuuza utukufu wake miongoni mwao.
9
Ubaguzi wao unashuhudia dhidi yao; wanatangaza dhambi yao kama ya Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao watu hao, kwani wamejiletea maangamizi wenyewe.
10
Waambieni waadilifu jinsi walivyo na bahati: Kwani watakula matunda ya matendo yao.
11
Lakini ole wao watu waovu! Mambo yatawaendea vibaya, kwani waliyotenda yatawapata wao wenyewe.
12
Watu wangu watadhulumiwa na watoto; wanawake ndio watakaowatawala. Enyi watu wangu, viongozi wenu wanawapotosha, wanavuruga njia mnayopaswa kufuata.
13
Mwenyezi-Mungu yu tayari kuanza mashtaka, anasimama kuwahukumu watu wake.
14
Mwenyezi-Mungu anawashtaki wazee na wakuu wa watu wake: “Nyinyi ndio mlioliharibu shamba la mizabibu; mali walizowanyanganywa maskini zimo nyumbani kwenu.
15
Mnamaanisha nini kuwakandamiza watu wangu, kuwatendea ukatili watu maskini? Nauliza mimi Bwana, Mwenyezi-Mungu wa majeshi.”
16
Mwenyezi-Mungu asema: “Wanawake wa Siyoni wana kiburi; wanatembea wameinua shingo juu, wakipepesa macho yao kwa tamaa. Hatua zao ni za maringo, na miguuni njuga zinalia.
17
Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nitawaadhibu; nitawanyoa nywele hao wanawake wa Siyoni, na kuwavua nguo za kufunika uchi wao.”
18
Siku yaja ambapo Mwenyezi-Mungu atawanyanganya wanawake wa Yerusalemu vitu vyote wanavyoringia: Njuga, kaya, mikufu,
19
vipuli, vikuku, shungi,
20
vitambaa vya kichwani, bangili, vibwebwe, vibweta vya marashi, hirizi,
21
pete, hazama,
22
mavazi ya sikukuu, mitandio, majoho, mikoba,
23
mavazi yaoneshayo, mavazi ya kitani, vilemba na shela.
24
Badala ya kunukia marashi watatoa uvundo; badala ya mishipi mizuri watatumia kamba; badala ya nywele nzuri watakuwa na upara; badala ya mavazi mazuri watavaa matambara; uzuri wao wote utageuka kuwa aibu.
25
Wanaume wenu wataangamia kwa upanga, watu wenu wenye nguvu watakufa vitani.
26
Malango ya mji yatalia na kuomboleza; nao mji utakuwa kama mwanamke aliyepokonywa kila kitu, ameketi mavumbini.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66