bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 11
2 Kings 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 12 →
1
Atalia, mamake Ahazia, alipoona, ya kuwa mwanawe amekufa, akaondoka, akawaangamiza wazao wote wa kifalme.
2
Lakini Yoseba, binti mfalme Yoramu, umbu lake Ahazia, akamchukua Yoasi, mwana wa Ahazia, akamwiba katikati ya wana wa mfalme waliokwenda kuuawa, akamweka pamoja na mnyonyeshaji wake katika chumba cha kulalia. Ndivyo, alivyomficha, Atalia asimwone; kwa hiyo hakuuawa.
3
Akakaa naye na kufichwa Nyumbani mwa Bwana miaka sita, Atalia alipokuwa mfalme wa kike wa nchi hiyo.
4
Katika mwaka wa saba Yoyada akatuma kuwachukua wakuu wa mamia ya askari na wapiga mbio, akawapeleka kwake Nyumbani mwa Bwana, akafanya maagano nao akiwaapisha mle Nyumbani. Kisha akawaonyesha mwana wa mfalme,
5
akawaagiza kwamba: Hili ndilo neno, mtakalolifanya: fungu lenu la tatu watakaoingia kazi siku ya mapumziko na walinde ulinzi wa nyumba ya mfalme;
6
fungu jingine la tatu na walinde penye lango la Suri, nalo fungu jingine la tatu na walinde langoni nyuma ya wapiga mbio! Ndivyo, mtakavyolinda ulinzi wa hiyo nyumba na kuzuia watu.
7
Navyo vikosi vyenu viwili watakaotoka kazini siku ya mapumziko, wote sharti walinde ulinzi wa Nyumba ya Bwana kwake mfalme!
8
Sharti mmzunguke mfalme pande zote kila mtu akiyashika mata yake, kila atakayeingia katika hii mipango ya watu na auawe! Hivyo sharti mwe na mfalme, akitoka, hata akiingia.
9
Wakuu wa mamia wakayafanya yote, kama mtambikaji Yoyada alivyowaagiza; kila mtu akawachukua watu wake walioingia kazi siku ya mapumziko nao waliotoka kazi siku ya mapumziko, wakaja kwa mtambikaji Yoyada.
10
Kisha huyu mtambikaji akawapa wakuu wa mamia mikuki na ngao za mfalme Dawidi zilizokuwamo Nyumbani mwa Bwana.
11
Wakawapanga wapiga mbio, kila mtu na mkuki wake mkononi mwake kuanzia upande wa kuume wa Nyumba kuufikia upande wa kushoto wa Nyumba, kuifikia meza ya kutambikia na tena kuifikia Nyumba yenyewe, wamzunguke mfalme pande zote.
12
Kisha akamtoa mwana wa mfalme, akamvika kilemba cha kifalme, wakampa nacho kizingo cha Ushahidi, wakamfanya kuwa mfalme wakimpaka mafuta. Kisha wakapiga makofi na kusema: Pongezi, mfalme!
13
Atalia alipozisikia sauti za wapiga mbio na za watu, akaja naye hapo, watu walipokuwa, penye Nyumba ya Bwana.
14
Alipotazama, akamwona mfalme, akisimama katika ulingo kama desturi, nao wakuu na wapiga matarumbeta wakisimama kwake mfalme, nao watu wote wa nchi yao wakawa wenye furaha na kupiga matarumbeta. Ndipo, Atalia alipoyararua mavazi yake na kupiga kelele kwamba: Mmedanganyika! Mmedanganyika!
15
Ndipo, mtambikaji Yoyada alipowaagiza wakuu wa mamia waliovisimamia vikosi, akawaambia: Mtoeni hapa penye mipango ya watu! Naye atakayemfuata na auawe kwa upanga! Kwani mtambikaji alisema, asiuawe Nyumbani mwa Bwana.
16
Wakamkamata kwa mikono, naye alipofika penye njia, farasi waliyoishika ya kuingia nyumbani mwa mfalme, akauawa hapo.
17
Kisha Yoyada akafanya agano na Bwana, yeye na mfalme wa watu, wawe ukoo wake Bwana; agano jingine akamfanyia mfalme na watu.
18
Ndipo, watu wote wa nchi hiyo walipoiingia nyumba ya Baali, wakaibomoa, nazo meza za kumtambikia na vinyago vyake wakavivunjavunja kabisa, naye Matani, mtambikaji wa Baali, wakamwua mbele ya meza za kutambikia. Kisha yule mtambikaji akaweka wakaguzi wa Nyumba ya Bwana.
19
Kisha akawachukua wakuu wa mamia nao askari nao wapiga mbio pamoja na watu wote wa nchi hii, wakamtoa mfalme Nyumbani mwa Bwana, wakaingia nyumbani mwa mfalme na kushika njia ya lango la wapiga mbio; ndivyo, alivyopata kukaa katika kiti cha kifalme cha wafalme.
20
Nao watu wote wa nchi hii wakafurahi, nao mji ukatulia. Lakini Atalia walikuwa wamemwua kwa upanga nyumbani mwa mfalme.
21
Naye Yoasi alikuwa mwenye miaka saba alipoupata ufalme.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25