bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 2
2 Kings 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 3 →
1
Bwana alipotaka kumpaza Elia mbinguni kwa nguvu za upepo wenye ngurumo, Elia na Elisa walikuwa wakienda njiani kutoka Gilgali.
2
Elia akamwambia Elisa: Kaa hapa! Kwani Bwana amenituma kwenda Beteli. Elisa akajibu: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, tena hivyo, wewe mwenyewe ulivyo mzima, sitakuacha kabisa. Wakatelemka kwenda Beteli.
3
Ndipo, wanafunzi wa wafumbuaji waliomo Beteli walipomtokea Elisa, wakamwambia: Unajua, ya kuwa leo Bwana atamwondoa bwana wako kichwani pako? Akasema: Nami nayajua, nyamazeni tu!
4
Elia akamwambia: Elisa, kaa hapa! Kwani Bwana amenituma kwenda Yeriko. Akajibu: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, tena hivyo, wewe mwenyewe ulivyo mzima, sitakuacha kabisa. Wakaja Yeriko.
5
Ndipo, wanafunzi wa wafumbuaji waliomo Yeriko walipomjia Elisa, wakamwambia: Unajua, ya kuwa leo Bwana atamwondoa bwana wako kichwani pako? Akasema: Nami nayajua, nyamazeni tu!
6
Elia akamwambia: Kaa hapa! Kwani Bwana amenituma kwenda Yordani. Akajibu: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, tena hivyo, wewe mwenyewe ulivyo mzima, sitakuacha kabisa. Wakaenda wote wawili.
7
Watu hamsini waliokuwa wanafunzi wa wafumbuaji wakaja, wakasimama mbali ng'ambo ya huku, wao wawili waliposimama Yordani.
8
Ndipo, Elia alipolishika joho lake, akalizinga, akalipigisha maji; ndipo, yalipogawanyika huku na huko, nao wote wawili wakapita pakavu.
9
Walipokwisha pita, Elia akamwambia Elisa: Omba unayoyataka, nikufanyizie, nikiwa sijaondolewa kwako! Elisa akasema: Ninataka, mafungu mawili ya roho yako yaje kunikalia.
10
Elia akajibu: Umeomba neno gumu. Utakaponiona, nikiondolewa kwako, na ulipate! Usipoviona, hutalipata.
11
Ikawa, wangaliko njiani na kusema, mara gari la moto likatokea pamoja na farasi wa moto, likawatenga wale wawili. Ndivyo, Elia alivyopaa mbinguni kwa nguvu za upepo wenye ngurumo.
12
Elisa alipoviona akalia kwamba: Baba yangu! Baba yangu! Wewe gari la Waisiraeli na wapanda farasi wake! Lakini hakumwona tena; kisha akazishika nguo zake, akazirarua, zitoke vipande viwili.
13
Kisha akaliokota joho lake Elia lililokuwa limeanguka, akarudi, akasimama kando ya mto wa Yordani.
14
Akalishika hilo joho la Elia lililokuwa limeanguka, akalipigisha maji akisema: Bwana Mungu wa Elia yuko wapi? Basi; hapo, yeye naye alipoyapiga maji, mara maji yakagawanyika huku na huko, naye Elisa akapita.
15
Wanafunzi wa wafumbuaji waliokuwako Yeriko ng'ambo ya huku walipomwona wakasema: Roho yake Elia inamkalia Elisa. Wakamwendea, wakamwangukia chini.
16
Wakamwambia: Tazama, huku wako watu hamsini wenye nguvu; acha, tuwatume, waende kumtafuta bwana wako! Labda roho ya Bwana imemchukua, ikamweka juu ya mlima mmoja au katika bonde moja. Akawaambia: Msiwatume!
17
Walipomhimiza sana, mpaka akilegea, akasema: watumeni! Ndipo, walipowatuma wale watu hamsini, wakamtafuta siku tatu, lakini hawakumwona.
18
Waliporudi kwake, yeye alikuwa angaliko Yeriko, akawaambia: Sikuwaambia, msiende?
19
Kisha watu wa huo mji wakamwambia Elisa: Tazama, hapa, mji huu unapokaa, ni pema, kama wewe bwana unavyoona, lakini maji ni mabaya, kwa hiyo nchi hii hupoozesha mimba, ziharibike.
20
Akasema: Nileteeni bakuli jipya, kisha tieni chumvi humo! Walipomletea,
21
akaenda nje kufika hapo, maji yalipotokea, akaitupa ile chumvi papo hapo akisema: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nimeyapatia maji haya uzima, hayataua tena, wala hayatapoozesha tena mimba.
22
Ndipo, yale maji yalipopona hata siku hii ya leo, kama Elisa alivyosema.
23
Toka huko akapanda kwenda Beteli; alipokuwa akipanda njiani, watoto wakatoka mjini, wakamfyoza wakimwambia: Panda, Chakipara! Panda, Chakipara!
24
Alipogeuka nyuma akawaona, akawaapiza katika Jina la Bwana. Ndipo, chui wawili walipotoka mwituni, wakararua kwao watoto 42.
25
Kisha akatoka huko kwenda mlimani kwa Karmeli, toka huko akarudi Samaria.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25