bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 14
2 Kings 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 15 →
1
Katika mwaka wa 2 wa Yoasi, mwana wa Yoahazi, mfalme wa Waisiraeli, Amasia, mwana wa Yoasi, akapata kuwa mfalme wa Wayuda.
2
Alikuwa mwenye miaka 25 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 29. Jina la mama yake ni Yoadani wa Yerusalemu.
3
Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana, lakini hakuwa kama baba yake Dawidi; naye akayafanya yote, baba yake Yoasi aliyoyafanya.
4
Matambiko ya vilimani tu hayakukoma, maana watu waliendelea bado kutambika na kuvukiza vilimani pa kutambikia.
5
Ikawa, ufalme ulipopata kushupaa mkononi mwake, akawaua watumishi wake waliomwua baba yake mfalme.
6
Lakini wana wao wale wauaji hakuwaua, kwa kuwa imeandikwa katika kitabu cha Maonyo ya Mose, Bwana aliyomwagiza kwamba: Baba wasiuawe kwa ajili ya wana, wala wana wasiuawe kwa ajili ya baba, ila kila mtu na auawe kwa kosa lake yeye!
7
Naye ndiye aliyewapiga Waedomu watu 10000 katika Bonde la Chumvi, akauteka nao mji wa Sela katika vita hivyo, akauita jina lake Yokiteli mpaka siku hii ya leo.
8
Kisha Amasia akatuma wajumbe kwa Yoasi, mwana wa Yoahazi, mwana wa Yehu, mfalme wa Waisiraeli, kumwambia: Njoo, tuonane uso kwa uso!
9
Naye Yoasi, mfalme wa Waisiraeli, akatuma wajumbe kwa Amasia, mfalme wa Wayuda, kwamba: Kingugi kilichoko Libanoni kilituma kwa mwangati ulioko Libanoni kwamba: Mpe mwanangu mwanao wa kike, awe mkewe! Ndipo, nyama wa porini wa huko Libanoni alipopita, akakikanyaga kile kingugi na kukiponda.
10
Kwa kuwa umewapiga Waedomu, moyo wako unakukuza; jitutumue, lakini kaa nyumbani mwako! Mbona unataka kujitia katika vita vibaya, uanguke wewe na Wayuda pamoja nawe?
11
Lakini Amasia hakusikia; ndipo, Yoasi, mfalme wa Waisiraeli, alipopanda, wakaonana uso kwa uso, yeye na Amasia, mfalme wa Wayuda, huko Beti-Semesi katika nchi ya Wayuda.
12
Wayuda wakashindwa na Waisiraeli, wakakimbia kila mtu hemani kwake.
13
Naye Yoasi, mfalme wa Waisiraeli, akamkamata Amasia, mfalme wa Wayuda, aliyekuwa mwana wa Yoasi, mwana wa Yoahazi, kule Beti-Semesi, kisha akaja Yerusalemu, akalivunja boma la Yerusalemu toka lango la Efuraimu hata lango la pembeni, ndio mikono 400.
14
Akachukua dhahabu na fedha zote, navyo vyombo vyote vilivyopatikana Nyumbani mwa Bwana namo katika vilimbiko vya nyumbani mwa mfalme nao watu, aliowataka kuwa kole, kisha akarudi Samaria.
15
Mambo mengine ya Yoasi aliyoyafanya na matendo yake yenye nguvu aliyoyatenda alipopiga vita na Amasia, mfalme wa Wayuda, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Waisiraeli?
16
Yoasi alipokwenda kulala na baba zake, akazikwa Samaria kwa wafalme wa Waisiraeli, naye mwanawe Yeroboamu akawa mfalme mahali pake.
17
Naye Amasia, mwana wa Yoasi, mfalme wa Wayuda, akawapo tena miaka 15 baada ya kufa kwa Yoasi, mwana wa Yoahazi, mfalme wa Waisiraeli.
18
Mambo mengine ya Amasia hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
19
Walipomlia njama mle Yerusalemu, akakimbilia Lakisi; ndipo, walipotuma watu kumfuata huko Lakisi, wakamwua huko.
20
Wakamchukua kwa farasi, akazikwa mle Yerusalemu kwa baba zake mjini mwa Dawidi.
21
Kisha watu wote wa Yuda wakamchukua Azaria aliyekuwa mwenye miaka 16, wakamfanya kuwa mfalme mahali pa baba yake Amasia.
22
Yeye akaujenga Elati, akaurudisha kwao Wayuda, mfalme alipokuwa amelala na baba zake.
23
Katika mwaka wa 15 wa Amasia, mwana wa Yoasi, mfalme wa Wayuda, Yeroboamu, mwana wa Yoasi, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli mle Samaria miaka 41.
24
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, hakuyaepuka makosa yote ya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Waisiraeli.
25
Yeye akairudisha mipaka ya Waisiraeli toka Hamati mpaka kwenye bahari ya nyikani, kama Bwana Mungu wa Isiraeli alivyosema kinywani mwa mtumishi wake mfumbuaji Yona, mwana wa Amitai, wa Gati-Heferi.
26
Kwani Bwana aliyaona mateso ya Waisiraeli yaliyokuwa yenye machungu sana, akaona, ya kuwa waliofungwa nao waliofunguliwa wanamalizika, kwa kuwa hakuwako aliyewasaidia Waisiraeli.
27
Naye Bwana alikuwa hajasema, ya kuwa atalifuta jina la Isiraeli, litoweke chini ya mbingu, kwa hiyo akawasaidia kwa mkono wa Yeroboamu, mwana wa Yoasi.
28
Mambo mengine ya Yeroboamu, nayo yote, aliyoyafanya, na matendo yake yaliyokuwa yenye nguvu, alipopiga vita, tena jinsi alivyoirudisha kwa Waisiraeli miji ya Damasko na ya Hamati iliyokuwa kale ya Wayuda, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Waisiraeli?
29
Yeroboamu alipokwenda kulala na baba zake wafalme wa Waisiraeli, mwanawe Zakaria akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25