bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 23
2 Kings 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 24 →
1
Ndipo, mfalme alipotuma wajumbe, wakusanye kwake wazee wote wa Wayuda na wa Yerusalemu.
2
Kisha mfalme akapanda kwenda Nyumbani mwa Bwana pamoja na Wayuda wote na wenyeji wote wa Yerusalemu na watambikaji na wafumbuaji na watu wote pia, wadogo kwa wakubwa, wakaenda naye, akawasomea masikioni pao maneno yote ya kitabu cha Agano kilichooneka Nyumbani mwa Bwana.
3
Kisha mfalme akaja kusimama penye ile nguzo, akafanya mbele ya Bwana agano la kumfuata Bwana na kuyaangalia maagizo yake na mashuhuda yake na maongozi yake kwa moyo wote na kwa roho yote, ayasimamishe maneno ya Agano hili yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Nao watu wote wakaliitikia agano hili, walishike na kulisimamia.
4
Kisha mfalme akamwagiza mtambikaji mkuu Hilkia na watambikaji wa pili na walinzi wa vizingiti, watoe Jumbani mwa Bwana vyombo vyote vilivyotengenezwa vya kumtambikia Baali na Ashera na vikosi vyote vya mbinguni, wakavichoma moto nje ya Yerusalemu kwenye mashamba ya Kidoroni, nayo majivu yao akayatuma kupelekwa Beteli.
5
Akawakomesha watambikaji wa kimizimu, wafalme wa Wayuda waliowaweka, wavukize vilimani pa kutambikia katika miji ya Wayuda na katika mitaa ya Yerusalemu, ndio waliomvukizia Baali, hata jua na mwezi na nyota zilizoko njiani kwa jua na vikosi vyote vya mbinguni.
6
Nacho kinyago kile cha Ashera akakitoa Nyumbani mwa Bwana na kukipeleka nje ya Yerusalemu kwenye mto wa Kidoroni, akakichoma moto huko kwenye mto wa Kidoroni na kukipondaponda, kiwe mavumbi tu, nayo hayo mavumbi akayatupa kwenye makaburi yao walio watuwatu tu.
7
Navyo vyumba vya wagoni wa Patakatifu vilivyokuwamo Nyumbani mwa Bwana akavibomoa; ndimo, wanawake walimofuma mahema ya Ashera.
8
Nao watambikaji wote akawatoa katika miji ya Wayuda, akavichafua vijumba vya vilimani, hao watambikaji walimovukizia toka Geba mpaka Beri-Seba, navyo vijumba vya kutambikia vilimani vilivyokuwa malangoni upande wa kushoto wa hapo pa kuliingilia lango la Yosua, mkuu wa mji, watu walipoingia mjini, navyo akavibomoa kabisa.
9
Lakini wale watambikaji wa vilimani hawakupata ruhusa kutambika penye meza ya kumtambikia Bwana mle Yerusalemu, wakala tu kwa ndugu zao mikate isiyochachwa.
10
Akapachafua napo Tofeti katika bonde la wana wa Hinomu, mtu asiweze tena kumtolea Moleki mwanawe wa kiume au wa kike, awe ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa motoni.
11
Akawakomesha nao wale farasi, wafalme wa Wayuda waliowekea jua hapo pa kuingia Nyumbani mwa Bwana karibu ya chumba cha kulalia cha mtumishi wa nyumbani Natani-Meleki kilichokuwa katika kijumba kile kilichojengwa upande wa machweoni kwa jua, nayo magari ya jua akayateketeza motoni.
12
Nazo meza za kutambikia zilizokuwa darini penye chumba cha juu cha Ahazi zilizotengenezwa na wafalme wa Wayuda nazo meza za kutambikia, Manase alizozitengeneza katika nyua zote mbili za Nyumba ya Bwana, mfalme akazivunjavunja na kuzitoa hapo, kisha akayatupa mavumbi yao katika mto wa Kidoroni.
13
Mfalme akavichafua navyo vijumba vya vilimani pa kutambikia vilivyoko ng'ambo ya Yerusalemu kuumeni kwenye Mlima wa Mwangamizaji, Salomo, mfalme wa Waisiraeli, alivyovijenga vya kutambikia Astoreti, lile tapisho la Wasidoni, na Kemosi, lile tapisho la Wamoabu, na Milkomu, lile chukizo la wana wa amoni.
14
Akazivunja nazo nguzo za mawe za kutambikia, nayo miti ya Ashera akaikatakata, kisha akapajaza mahali pao mifupa ya watu.
15
Akaivunjavunja nayo meza ya kutambikia iliyokuwa Beteli kilimani. Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Waisiraeli, alikotengeneza kijumba cha kutambikia; basi, ile meza yenyewe pamoja na kijumba cha kutambikia pale kilimani akaivunjavunja, kisha yote pia yaliyokuwako huko kilimani akayateketeza kwa moto, akayapondaponda, yawe mavumbi tu, hata kinyago cha Ashera akakiteketeza.
16
Yosia alipogeuka akaona makaburi yaliyokuwa katika mlima ule, akatuma kuichukua mifupa iliyokuwa mle makaburini, akaiteketeza juu ya meza ya kutambikia, akaichafua hivyo kwa lile neno la Bwana, alilolitangaza yule mtu wa Mungu aliyeyatangaza mambo haya.
17
Akauliza tena: Hicho kijengo, ninachokiona, ndio nini? Watu wa huo mji wakamwambia: Ni kaburi la mtu wa Mungu aliyetoka Yuda na kuyatangaza haya, uliyoyafanya juu ya meza ya kutambikia huku Beteli.
18
Ndipo, aliposema: Mwacheni huyu, alale! Mtu asiisumbue mifupa yake! Basi, wakaacha kuigusa mifupa yake nayo mifupa ya mfumbuaji aliyetoka Samaria.
19
Nazo nyumba zote zilizojengwa za kutambikia vilimani kwenye miji ya Samaria, wafalme wa Waisiraeli walizozijenga, wamkasirishe Bwana, Yosia akaziondoa, nazo akazifanyizia mambo kama yale yote, aliyoyafanya huko Beteli.
20
Nao watambikaji wote wa vilimani waliokuwako huko akawachinja, wawe ng'ombe za tambiko juu ya zile meza za kutambikia, hata mifupa ya watu akaiteketeza juu yao, kisha akarudi Yerusalemu.
21
Kisha mfalme akawaagiza watu wote kwamba: Fanyeni sikukuu ya Pasaka ya Bwana, kama ilivyoandikwa katika kitabu hiki cha Agano!
22
Kwani Pasaka kama hiyo haikufanywa tangu siku za waamuzi waliowaamua Waisiraeli hata siku zote za wafalme wa Waisiraeli na wa Wayuda.
23
Ila Pasaka hii ya Bwana ilifanywa mle Yerusalemu katika mwaka wa 18 wa mfalme Yosia.
24
Nao wakweza mizimu na wapunga pepo na vinyago vya nyumbani na magogo ya kutambikia na matapisho yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda namo Yerusalemu Yosia akayaondoa, kusudi ayatimize maneno ya Maonyo yaliyoandikwa katika kile kitabu, mtambikaji Hilkia alichokiona Nyumbani mwa Bwana.
25
Mfalme kama yeye hakuwako mbele yake aliyemwelekea Bwana kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote na kwa nguvu yake yote, ayafanye Maonyo yote ya Mose, wala nyuma yake hakuondokea aliyekuwa kama yeye.
26
Lakini Bwana hakuyaacha makali yake makuu yenye moto yaliyowawakia Wayuda kwa ajili ya matendo ya kumkasirisha, manase aliyomkasirisha nayo.
27
Kwa hiyo Bwana akasema: Wayuda nao nitawaondoa usoni pangu, kama nilivyowaondoa Waisiraeli, tena nitautupa nao mji huu wa Yerusalemu, niliouchagua, nayo Nyumba hii, niliyoisema: Jina langu litakaa humu.
28
Mambo mengine ya Yosia nayo yote, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
29
Hizo siku zake akapanda Farao Neko, mfalme wa Misri, kwenda kupigana na mfalme wa Asuri kwenye mto wa Furati. Mfalme Yosia alipotoka kumpinga, yule akamwua kule Megido papo hapo, alipomwona.
30
Watumishi wake wakamchukua garini, alipokwisha kufa, wakamtoa Megido na kumpeleka Yerusalemu, wakamzika kaburini mwake. Kisha watu wa nchi hii wakamchukua Yoahazi, mwana wa Yosia, wakampaka mafuta, wakamfanya kuwa mfalme mahali pa baba yake.
31
Yoahazi alikuwa mwenye miaka 23 alipoupata ufalme, akawa mfalme miezi 3 mle Yerusalemu; jina la mama yake ni Hamutali, binti Yeremia, wa Libuna.
32
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama yote, baba zake waliyoyafanya.
33
Farao Neko akamfunga huko Ribula katika nchi ya Hamati, asiwe mfalme mle Yerusalemu, akailipisha nchi hii vipande 100 vya fedha, ndio shilingi milioni na 200000, na kipande kimoja cha dhahabu, ndio shilingi 220000.
34
Kisha Farao Neko akamfanya Eliakimu, mwana wa Yosia, kuwa mfalme mahali pa baba yake Yosia, akaligeuza jina lake, akamwita Yoyakimu. Lakini Yoahazi akamchukua, aje naye Misri; ndiko, alikokufa.
35
Zile fedha na dhahabu Yoyakimu akampa Farao; lakini hakuwa na budi kuitoza nchi machango, apate kuzilipa hizo fedha, Farao alizozitaka; watu wa hiyo nchi yake akamtoza kila mmoja kwa mali, alizowaziwa kuwa nazo; ndivyo, alivyowachangisha hizo fedha na dhahabu za kumpa Farao Neko.
36
Yoyakimu alikuwa mwenye miaka 25 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 11 mle Yerusalemu; jina la mama yake ni Zebuda, binti Pedaya, wa Ruma.
37
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama yote, baba zake waliyoyafanya.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25