bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 21
2 Kings 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 22 →
1
Manase alikuwa mwenye miaka 12 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 55 mle Yerusalemu, nalo jina la mama yake ni Hefusiba.
2
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kwa kuyafuata matapisho ya wamizimu, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Isiraeli.
3
Akavijenga tena vijumba vya kutambikia vilimani, baba yake Hizikia alivyoviangamiza, akaweka nazo meza za kumtambikia Baali, akatengeneza nacho kinyago cha Ashera, kama Ahabu, mfalme wa Waisiraeli, alivyofanya, akaviangukia navyo vikosi vyote vya mbinguni na kuvitumikia.
4
Namo Nyumbani mwa Bwana akajenga penginepengine pa kutambikia, namo humo ndimo, Bwana alimosema: Yerusalemu ndimo, Jina langu litakamokaa.
5
Katika nyua zote mbili za Nyumba ya Bwana akajenga pa kuvitambikia vikosi vya mbinguni.
6
Hata mwanawe akamtumia kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa motoni, tena akaagulia mawingu, akapiga bao, akatumia nao wakweza mizimu na wapunga pepo, akazidi kuyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, amkasirishe.
7
Nacho kinyago cha Ashera, alichokitengeneza, akakiweka katika Nyumba ile, Bwana aliyomwambia Dawidi na mwanawe Salomo: Humu Nyumbani namo Yerusalemu, niliouchagua katika mashina yote ya Isiraeli, nitalikalisha Jina langu kale na kale.
8
Sitaikimbiza tena miguu ya Waisiraeli katika nchi hii, niliyowapa baba zao, wakijiangalia tu na kuyafanya yote, niliyowaagiza, na kuyafuata Maonyo, mtumishi wangu Mose aliyowaagiza.
9
Lakini hawakusikia, naye Manase akawaponza kufanya mabaya kuliko wamizimu, Bwana aliowaangamiza mbele ya wana wa Isiraeli.
10
Kisha Bwana akasema vinywani mwa watumishi wake wafumbuaji kwamba:
11
Kwa kuyafanya hayo matapisho Manase, mfalme wa Wayuda, amefanya mabaya kuliko yote, waliyoyafanya Waamori waliokuwako mbele yake, nao Wayuda akawakosesha kwa kuyatambikia magogo yake.
12
Kwa sababu hii Bwana Mungu wa Isiraeli anasema hivi: Mtaniona, nikileta mabaya, yaingie Yerusalemu nako kwa Wayuda, nao watu wote watakaoyasikia masikio yao yote mawili yatawavuma.
13
Nitautandia Yerusalemu kamba ya kupimia iliyoupima Samaria, niweke nayo mizani iliyoupima mlango wa Ahabu, kisha nitausafisha mji wa Yerusalemu, kama mtu anavyosafisha bakuli, kisha hulifudikiza.
14
Nao watakaosalia kwao waliokuwa wangu nitawatupa na kuwatia mikononi mwa adui zao, wanyang'anywe mali zao na kutekwa na adui zao wote,
15
kwa kuwa wameyafanya yaliyo mabaya machoni pangu, wakanikasirisha tangu siku ile, baba zao walipotoka huko Misri, hata siku hii ya leo.
16
Manase akazidi sana kumwaga damu za watu wasiokosa, akaujaza Yerusalemu hizo damu toka upande huu mpaka upande wa pili; tena kosa lake kubwa lilikuwa hilo la kuwakosesha Wayuda, wayafanye yaliyo mabaya machoni pake Bwana.
17
Mambo mengine ya Manase nayo yote, aliyoyafanya, na makosa yake, aliyoyakosa, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
18
Manase alipokwenda kulala na baba zake, akazikwa katika bustani penye nyumba yake, ndio katika bustani ya Uza, naye mwanawe Amoni akawa mfalme mahali pake.
19
Amoni alikuwa mwenye miaka 22 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 2 mle Yerusalemu; jina la mama yake ni Mesulemeti, binti Harusi, wa Yotiba.
20
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, kama baba yake Manase alivyofanya.
21
Akaendelea kuzishika njia zote, alizozishika baba yake, akayatumikia magogo ya kutambikia, baba yake aliyoyatumikia, naye akayaangukia.
22
Akamwacha Bwana Mungu wa baba zake, hakuishika njia ya Bwana.
23
Ndipo, watumishi wa Amoni walipomlia njama, wakamwua mfalme nyumbani mwake.
24
Lakini watu wa nchi hiyo wakawaua wote waliomlia mfalme Amoni njama, kisha hao watu wa nchi hiyo wakamfanya mwanawe Yosia kuwa mfalme mahali pake.
25
Mambo mengine ya Amoni, aliyoyafanya hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
26
Wakamzika kaburini mwake katika bustani ya uza, naye mwanawe Yosia akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25