bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 15
2 Kings 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 16 →
1
Katika mwaka wa 27 wa Yeroboamu, mfalme wa Waisiraeli, Azaria, mwana wa Amasia, akapata kuwa mfalme wa Wayuda.
2
Alikuwa mwenye miaka 16 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 52. Jina la mama yake ni Yekolia wa Yerusalemu.
3
Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana kama yote, baba yake Amasia aliyoyafanya.
4
Matambiko ya vilimani tu hayakukoma, maana watu waliendelea bado kutambika na kuvukiza vilimani pa kutambikia.
5
Bwana akampiga mfalme, akawa mwenye ukoma hata siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya wagonjwa waliotengwa, naye mwanawe Yotamu akawa mkuu nyumbani mwa mfalme, akawaamua watu wa nchi hii.
6
Mambo mengine ya Azaria nayo yote, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
7
Azaria alipokwenda kulala na baba zake, wakamzika kwa baba zake mjini mwa Dawidi, naye mwanawe Yotamu akawa mfalme mahali pake.
8
Katika mwaka wa 38 wa Azaria, mfalme wa Wayuda, Zakaria, mwana wa Yeroboamu, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli mle Samaria miezi 6.
9
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, kama baba zake walivyofanya, hakuyaepuka makosa ya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Waisiraeli.
10
Salumu, mwana wa Yabesi, akamlia njama, akampiga machoni pa watu, akamwua, akawa mfalme mahali pake.
11
Mambo mengine ya Zakaria tunayaona, yameandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Waisiraeli.
12
Hapo limetimia lile neno la Bwana, alilomwambia Yehu kwamba: Wanao wa vizazi vinne watakaa katika kiti cha kifalme cha Waisiraeli. Ikawa hivyo.
13
Salumu, mwana wa Yabesi, akapata kuwa mfalme katika mwaka wa 39 wa Uzia, mfalme wa Wayuda, akawa mfalme mle Samaria siku za mwezi mmoja.
14
Ndipo, Menahemu, mwana wa Gadi, wa Tirsa, alipopanda, akaingia Samaria, akampiga Salumu, mwana wa Yabesi, mle Samaria, akamwua, akawa mfalme mahali pake.
15
Mambo mengine ya Salumu nayo njama yake, aliyomlia mfalme, tunayaona, yameandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Waisiraeli.
16
Siku zile Menahemu akaupiga mji wa Tifusa nao wote waliokuwamo na mipakani kwake toka Tirsa; kwa kuwa hawakumfungulia lango la mji, akawaua, nao wanawake waliokuwa wenye mimba akawatumbua.
17
Katika mwaka wa 39 wa Azaria, mfalme wa Wayuda, Menahemu, mwana wa Gadi, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli mle Samaria miaka 10.
18
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, siku zake zote hakuyaepuka makosa yote ya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Waisiraeli.
19
Puli, mfalme wa Asuri, alipijia nchi hiyo, ndipo, Menahemu alipompa Puli vipande vya fedha 1000, ndio shilingi milioni 12, kusudi amsaidie kwa mikono yake kuushupaza ufalme wake mkononi mwake.
20
Kisha Menahemu akawatoza Waisiraeli hizo fedha kwa kwamba: Kwao wenye mali kila mmoja ampe mfalme wa Asuri vipande vidogo vya fedha 50, ndio shilingi 200. Kisha mfalme wa Asuri akarudi, hakukaa huko katika nchi hiyo.
21
Mambo mengine ya Menahemu nayo yote, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Waisiraeli?
22
Menahemu alipokwenda kulala na baba zake, mwanawe Pekaya akawa mfalme mahali pake.
23
Katika mwaka wa 50 wa Azaria, mfalme wa Wayuda, Pekaya, mwana wa Menahemu, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli mle Samaria miaka 2.
24
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, hakuyaepuka makosa ya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Waisiraeli.
25
Peka, mwana wa Remalia, mkuu wake wa askari 30 akamlia njama, akamwua pamoja na Argobu na Arie huko Samaria katika jumba kubwa lililokuwa nyumba ya mfalme, hata watu 50 wa wana wa Gileadi walikuwa naye. Alipokwisha kumwua akawa mfalme mahali pake.
26
Mambo mengine ya Pekaya nayo yote, aliyoyafanya, tunayaona, yameandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Waisiraeli.
27
Katika mwaka wa 52 wa Azaria, mfalme wa Wayuda, Peka, mwana wa Remalia, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli mle Samaria miaka 20.
28
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, hakuyaepuka makosa ya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Waisiraeli.
29
Siku za Peka, mfalme wa Waisiraeli, akaja Tiglati-Pileseri, mfalme wa Asuri, akaiteka miji ya Iyoni na Abeli-Beti-Maka na Yanoa na Kedesi na Hasori na Gileadi na Galila, ndiyo nchi yote ya Nafutali, nao watu akawahamisha kwenda Asuri.
30
Ndipo, Hosea, mwana wa Ela, alipomlia njama Peka, mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, kisha akawa mfalme mahali pake katika mwaka wa 20 wa Yotamu, mwana wa Uzia.
31
Mambo mengine ya Peka nayo yote, aliyoyafanya, tunayaona, yameandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Waisiraeli.
32
Katika mwaka wa 2 wa Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Waisiraeli, Yotamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Wayuda, akapata kuwa mfalme.
33
Alikuwa mwenye miaka 25 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 16. Jina la mama yake ni Yerusa, binti Sadoki.
34
Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana kama yote, baba yake Uzia aliyoyafanya.
35
Matambiko ya vilimani tu hayakukoma, maana watu waliendelea bado kutambika na kuvukiza vilimani pa kutambikia. Yeye ndiye aliyelijenga lango la juu la Nyumba ya Bwana.
36
Mambo mengine ya Yotamu nayo yote, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
37
Siku zile Bwana akaanza kumtuma Resini, mfalme wa Ushami, na Peka, mwana wa Remalia, waijie nchi ya Yuda.
38
Yotamu alipokwenda kulala na baba zake, akazikwa kwa baba zake mjini mwa baba yake Dawidi, naye mwanawe Ahazi akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25