bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 1
2 Samuel 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 2 →
1
Ikawa, Sauli alipokwisha kufa, Dawidi akarudi kwa kuwapiga Waamaleki; kisha Dawidi akakaa Siklagi siku mbili.
2
Ilipokuwa siku ya tatu, mara akaja mtu aliyetoka makambini kwa Sauli, nguo zake zilikuwa zimeraruliwa, napo kichwani pake palikuwa na vumbi; naye alipofika kwake Dawidi akajitupa chini na kumwangukia.
3
Dawidi alipomwuliza: Unatoka wapi? akamwambia: Nimekimbia makambini kwa Waisiraeli.
4
Ndipo, Dawidi alipomwambia: Nisimulie yaliyofanyika huko! Akamwambia, ya kuwa watu walikimbia penye mapigano, kwa maana wengi wa kwao waliangushwa, wakafa, naye Sauli na mwanawe Yonatani wamekufa.
5
Dawidi akamwuliza huyo kijana aliyempasha habari hizi: Umejuaje, ya kuwa Sauli amekufa na mwanawe Yonatani?
6
Yule kijana aliyempasha hizi habari akamwambia: Ikanitukia, nifike mlimani kwa Gilboa, mara nikamwona Sauli, akiuegemea mkuki wake, nayo magari pamoja na wapanda farasi wakamsonga.
7
Alipogeuka nyuma, akaniona, akaniita; nami nikamwitikia kwamba: Nipo hapa!
8
Akaniuliza: Wewe nani? Nikamjibu: Mimi Mwamaleki.
9
Akaniambia: Njoo hapa, nilipo, uniue! Kwani kizunguzungu kimenipata, nayo roho yangu ingali nzima.
10
Ndipo, nilipokuja hapo, alipokuwa, nikamwua, kwani nilijua, ya kuwa hawezi kupona kwa hivyo, alivyoanguka;. kisha nikakichukua kilemba chake kichwani pake na kikuku chake mkononi pake, nimevileta hapa kwa bwana wangu, ni hivi!
11
Ndipo, Dawidi alipoyakamata mavazi yake, akayararua, nao watu wote waliokuwa naye wakafanya hivyo.
12
Wakaomboleza na kulia machozi, wakafunga mfungo mpaka jioni kwa ajili ya Sauli na kwa ajili ya mwanawe Yonatani na kwa ajili ya watu wa Bwana na kwa ajili yao wa mlango wa Isiraeli, kwa kuwa wameangushwa na panga.
13
Kisha Dawidi akamwuliza huyo kijana aliympasha habari hizi: Wewe u mtu wa wapi? Akasema: Mimi ni mwana wa mtu mgeni wa Amaleki.
14
Dawidi akamwambia: Kumbe hukuogopa kuuinua mkono wako, umwangamize aliyepakwa mafuta na Bwana?
15
Ndipo, Dawidi alipomwita mmoja wao vijana, akamwambia: Njoo, umpige! Naye alipompiga, akafa;
16
kisha Dawidi akamwambia: Damu yako na ikujie kichwani pako! Kwani kinywa chako kimekuponza na kusema kwamba: Mimi nimemwua aliyepakwa mafuta na Bwana.
17
Kisha Dawidi akatunga ombolezo hili la kumwombolezea Sauli na mwanawe Yonatani.
18
Akaagiza kuwafundisha wana wa Yuda wimbo huu wa upindi, nao utaukuta, umeandikwa katika kitabu cha Mnyofu:
19
Isiraeli, waliokuwa pambo lake wameuawa vilimani kwako! Imekuwaje, wakiangushwa hao mafundi wa vita?
20
Msiyasimulie Gati, wala msiyatangaze njiani kwa Askaloni, wasipate kufurahi wanawake wa Wafilisti, wasipige vigelegele wao wanawake wa kimizimu!
21
Msione tena umande wala mvua, ninyi milima ya Gilboa, yasiwe tena kwenu mashamba yenye malimbuko! Kwani ndiko, zilikoachwa ngao zao hao mafundi wa vita, ngao yake Sauli naye, kama hakupakwa mafuta.
22
Upindi wake Yonatani ulikuwa hauponyi, ijapo wawe mafundi wa vita wenye unono, uliotaka kuwaua; upanga wake Sauli haukurudi alani, usipokuwa umeua.
23
Sauli na Yonatani walipatana kwa kupendana mioyoni, hawakutengeka walipoishi, wala walipokufa. Walikuwa wepesi kuliko kozi, walikuwa wenye nguvu kuliko simba.
24
Ninyi wanawake wa Kiisiraeli, mwombolezeeni Sauli! Kwani aliwavika mavazi ya kifalme yenye urembo mwingi, kisha hizo nguo zenu akazipamba kwa mapambo ya dhahabu.
25
Imekuwaje, wakiangushwa vitani hao mafundi wa vita? Yonatani akiuawa vilimani kwako?
26
Moyo wangu umesongeka kwa ajili yako, maana wewe ulinipendeza sana, ndugu yangu Yonatani, upendo wako ulinifurahisha kuliko upendo wa wanawake.
27
Imekuwaje, wakiangushwa hao mafundi wa vita? hayo mata makali ya kupigia vita yakiangamia hivyo?
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24