bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 11
2 Samuel 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 12 →
1
Ikawa, mwaka ulipopita, siku hizo wafalme wanapozoea kwenda vitani, ndipo, Dawidi alipomtuma Yoabu na watumishi wake pamoja naye na Waisiraeli wote, wakawaangamiza wana wa Amoni, wakausonga mji wa Raba kwa kuuzinga, lakini Dawidi alikuwa anakaa Yerusalemu.
2
Siku moja saa za jioni Dawidi akaondoka kitandani pake, akatembea darini juu ya nyumba ya mfalme. Toka huko juu darini akaona mwanamke aliyeoga, naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana wa kumtazama.
3
Dawidi akatuma mtu kuuliza, huyo mwanamke kama ni wa nani, akaambiwa: Huyo siye Bati-Seba, binti Eliamu, mkewe Mhiti Uria?
4
Kisha Dawidi akatuma wajumbe, akamchukua; alipofika kwake, akalala naye. Naye huyu alipokwisha kujieua kwa ajili ya huo uchafu wake akarudi nyumbani mwake.
5
Huyu mwanamke alipopata mimba akatuma kumpasha Dawidi habari kwamba: Mimi ni mwenye mimba.
6
Ndipo, Dawidi alipotuma kwa Yoabu kwamba: Mtume Mhiti Uria, aje kwangu! Naye Yoabu akamtuma Uria kwake Dawidi.
7
Uria alipofika kwake Dawidi akamwuliza, kama Yoabu hajambo, kama watu hawajambo, tena jinsi vita vinavyoendelea.
8
Kisha Dawidi akamwambia Uria: Shuka kwenda nyumbani mwako kuiosha miguu yako! Uria alipotoka nyumbani mwa mfalme, chakula cha kifalme kikatoka nacho kumfuata.
9
Lakini Uria akalala mlangoni penye nyumba ya mfalme pamoja na watumishi wote wa bwana wake, hakushuka kwenda nyumbani mwake.
10
Watu walipompasha Dawidi habari hizo kwamba: Uria hakushuka kwenda nyumbani mwake, Dawidi akamwuliza Uria: Je? Hukutoka njiani? Mbona hushuki kwenda nyumbani mwako?
11
Ndipo, Uria alipomwambia Dawidi: Lile Sanduku na Waisiraeli na Wayuda wanakaa vibandani; naye bwana wangu Yoabu na watumishi wa bwana wangu wanalala porini; basi, mimi nitawezaje kuingia nyumbani mwangu, nile, ninywe, kisha nilale na mke wangu? Hivyo, ulivyo mzima, tena hivyo, roho yako ilivyo nzima, sitafanya kabisa jambo kama hilo.
12
Dawidi akamwambia Uria: Kaa huku hata leo! Kesho nitakupa ruhusa, uende zako. Kwa hiyo Uria akakaa Yerusalemu siku hiyo. Kesho yake,
13
Dawidi alipomwita, akala, akanywa kwake; ndipo, alipomlewesha. Jioni akatoka kulala penye kilalo chake pamoja na watumishi wa bwana wake, asishuke kwenda nyumbani mwake.
14
Kulipokucha, Dawidi akamwandikia Yoabu barua, akaipeleka mkononi mwa Uria.
15
Namo katika barua ameandika kwamba: Mwekeni Uria mahali pa mbele, mapigano yanapozidi kuwa makali! Kisha rudini nyuma na kumwacha, apigwe, afe!
16
Yoabu alipoyaangalia mambo ya huo mji, akamweka Uria mahali, alipopajua, ya kuwa hapo watatokea watu wenye nguvu.
17
Watu wa huo mji walipotoka kupigana na Yoabu, wakauawa watu miongoni mwao walio watu wake na watumishi wa Dawidi, hata yule Mhiti Uria akafa naye.
18
Kisha Yoabu akatuma kumpasha Dawidi habari za mambo yote ya vita.
19
Akamwagiza yule mjumbe kwamba: Utakapokwisha kumwambia mfalme habari zote za vita,
20
labda machafuko yatampata mfalme, akuulize: Mbona mmeukaribia huo mji kupigana nao? Hamkujua, ya kuwa watapiga mishale toka juu ukutani?
21
Ni nani aliyempiga Abimeleki, mwana wa Yerubeseti? Siye mwanamke aliyemtupia jiwe la sago toka juu ukutani, afe huko Tebesi? Mbona mmeukaribia mji hivyo? Basi, ndipo, utakapomwambia: Hata mtumishi wako yule Mhiti Uria, amekufa naye.
22
Kisha yule mjumbe akaenda, akaja kumpasha Dawidi habari hizo zote, Yoabu alizomtuma.
23
Huyo mjumbe akamwambia Dawidi: Wale watu wakatutolea nguvu na kututokea kwetu porini, nasi tukawaendea hata hapo pa kuliingilia lango la mji.
24
Ndipo, wapiga mishale walipowapiga watumishi wako toka juu ukutani, watu wakafa miongoni mwa watumishi wa mfalme, hata mtumishi wako, yule Mhiti Uria, akafa.
25
Naye Dawidi akamwambia huyo mjumbe: Hivyo umwambie Yoabu: Jambo hili lisiwe baya machoni pako! Kwani upanga hula huku na huko; jipe moyo, upigane na huo mji, mpaka uubomoe! Hivyo ndivyo, umshikize moyo.
26
Mkewe Uria aliposikia, ya kuwa mumewe Uria amekufa, akamwombolezea bwana wake.
27
Siku za matanga zilipopita, Dawidi akatuma kumchukua nyumbani mwake, akawa mkewe, akamzalia mwana. Lakini jambo hili, Dawidi alilolifanya, likawa baya machoni pake Bwana.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24