bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 2
2 Samuel 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 3 →
1
Ikawa, Dawidi alipomwuliza Bwana baadaye kwamba: Nipande kukaa katika mji mmoja wa Yuda? Bwana akamwambia: Panda! Dawidi akauliza tena: Nipande kukaa wapi? Akamwambia: Heburoni.
2
Ndipo, Dawidi alipopanda kukaa huko pamoja na wakeze wawili, Ahinoamu wa Izireeli na Abigaili, mkewe Nabali wa Karmeli.
3
Nao wale watu waliokuwa naye Dawidi akawapandisha kila mtu na mlango wake, wakakaa katika miji ya Heburoni.
4
Kisha waume wa Yuda wakaja, wakampaka Dawidi mafuta, awe mfalme wa mlango wa Yuda. Nao wakampasha Dawidi habari, ya kuwa watu wa Yabesi wa Gileadi wamemzika Sauli.
5
Dawidi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabesi wa Gileadi, akawaambia: Na mbarikiwe na Bwana ninyi, kwa kuwa bwana wenu Sauli mmemfanyizia tendo lililo jema la kumzika!
6
Sasa Bwwana na awafanyizie nanyi matendo yanayoelekea kuwa mema kweli, mimi nami na niwarudishie wema huo, kwa kuwa mmefanya jambo hilo.
7
Sasa na mwikaze mikono yenu, mpate nguvu, kwani bwana wenu Sauli amekufa, tena mimi nami wao wa mlango wa Yuda wamenipaka mafuta, niwe mfalme wao.
8
Naye Abineri, mwana wa Neri, aliyekuwa mkuu wa vikosi vya Sauli, akamchukua Isiboseti, mwana wa Sauli, akampeleka Mahanaimu,
9
akamfanya kuwa mfalme wa Gileadi na wa Asuri na wa Izireeli na wa Efuraimu na wa Benyamini na wa Waisiraeli wote.
10
Isiboseti, mwana wa Sauli, alikuwa mwenye miaka 40 alipoupata ufalme wa Waisiraeli, akawa mfalme miaka 2; ni wao wa mlango wa Yuda tu waliomfuata Dawidi.
11
Nayo hesabu ya siku, Dawidi alizokuwa mfalme wa mlango wa Yuda huko Heburoni, ikawa miaka 7 na miezi 6.
12
Abineri, mwana wa Neri, akatoka Mahanaimu na watumishi wa Isiboseti, mwana wa Sauli, kwenda Gibeoni.
13
Ndipo, Yoabu, mwana wa Seruya, alipotoka naye na watumishi wake Dawidi, wakakutana penye ziwa la Gibeoni; hao wakakaa ng'ambo ya huku ya hilo ziwa, nao wale wakakaa ng'ambo ya pili ya hilo ziwa.
14
Abineri akamwambia Yoabu: Na waondokee vijana, wacheze mbele yetu! Yoabu akaitikia: Haya! Na waondokee!
15
Basi, wakaondoka, wakaja kusimama huku na huko kwa kuhesabiwa: 12 wa Benyamini na wa Isiboseti, mwana wa Sauli, tena 12 watumishi wa Dawidi.
16
Wakakamatana kila mtu kichwa cha mwenzake, wakachomana panga kila mtu ubavuni mwa mwenzake, kwa hiyo wakaanguka wote pia, wakafa. Wakapaita mahali pale Fungu lenye Mapanga Makali lililoko Gibeoni.
17
Kisha mapigano yakawa makali sanasana siku hiyo, Abineri na watu wa Waisiraeli wakashindwa na watumishi wake Dawidi.
18
Wakawako wana watatu wa Seruya, Yoabu na Abisai na Asaheli; naye Asaheli alikuwa mwepesi kwa kupiga mbio kama paa wanaokaa porini.
19
Naye Asaheli akamkimbiza Abineri na kumfuata, hakujielekeza kwenda kuumeni wala kushotoni, asiache kumfuata Abineri.
20
Abineri akageuka nyuma, akamwuliza: Wewe siwe Asaheli? Akasema: Ndimi!
21
Abineri akamwambia: Geuka kuumeni kwako au kushotoni kwako, ukamate kijana mmoja, uchukue mata yake! Lakini Asaheli akakataa kuondoka kwake na kuacha kumfuata.
22
Abineri akamwambia Asaheli mara ya pili: Ondoka, uache kunifuata! Kwa nini nikupige, uanguke chini? Nitawezaje kutokea usoni pa kaka yako Yoabu?
23
Alipokataa kabisa kumwondokea, Abineri akamchoma tumboni kwa ncha ya chini ya mkuki, mkuki ukatokea mgongoni; ndipo, alipoanguka chini, akafa papo hapo. Ikawa, wote waliofika hapo, Asaheli alipoanguka chini akifa, wakasimama hapo.
24
Kisha Yoabu na Abisai wakamkimbiza Abineri; jua lilipokuchwa walikuwa wamefika kwenye kilima cha Ama kielekeacho Gia penye njia ya kwenda nyikani kwa Gibeoni.
25
Ndipo, wana wa Benyamini walipokusanyika, wamfuate Abineri, wakawa kikosi kimoja, wakasimama juu ya kilima kimoja.
26
Hapo Abineri akamwita Yoabu kwamba: Je? Upanga na ule kale na kale? Hujui, ya kuwa mwisho wake utakuwa uchungu? Utangoja mpaka lini, uwaambie hao watu, warudi na kuacha kuwafuata ndugu zao?
27
Yoabu akasema: Hivyo, Mungu alivyo Mwenye uzima, kama ungalisema hivyo asubuhi, watu wangalikwenda zao na kuacha kukimbizana kila mtu na ndugu yake.
28
Kisha Yoabu akapiga baragumu; ndipo, watu wote waliposimama, hawakuwakimbiza tena Waisiraeli, wala hawakuendelea kupigana nao.
29
Abineri na watu wake wakashika njia ya kupita jangwani usiku kucha, kisha wakavuka Yordani, wakapita Bitironi yote, kisha wakafika Mahanaimu.
30
Yoabu naye akarudi, akaacha kumfuata Abineri, akawakusanya watu wake wote; ndipo, ilipoonekana kwa watumishi wa Dawidi, ya kuwa watu 19 hawako, tena Asaheli.
31
Lakini watumishi wa Dawidi walipiga kwao Wabenyamini na kwa watu wa Abineri watu 360; ndio waliokufa.
32
Wakamchukua Asaheli, wakamzika katika kaburi la baba yake lililoko Beti-Lehemu; kisha Yoabu na watu wake wakaenda usiku kucha, nao walipofika Heburoni, kukapambazuka.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24