bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 22
2 Samuel 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 23 →
1
Dawidi akamwambia Bwana maneno ya wimbo huu, Bwana alipomponya mikononi mwa adui zake wote, namo mikononi mwa Sauli.
2
Akasema: Bwana ni ngome yangu na boma langu, tena mponya wangu;
3
ni Mungu aliye mwamba wangu, kwa hiyo ninamjetea, ni ngao yangu na pembe yangu ya kunipatia wokovu, kisha ni kingo langu, nipate pa kukimbilia, ni mwokozi wangu aniokoaye, nisije kukorofishwa.
4
Bwana atukuzwaye ndiye, ninayemwitia; ndipo, ninapookolewa mikononi mwao walio adui zangu.
5
Kwani mafuriko ya maji yauayo yalikuwa yameniasamia, nayo majito yaangamizayo yalinistusha,
6
kamba zivutiazo kuzimuni zilikuwa zimenizunguka, nayo mafungo yauayo yalikuwa mbele yangu.
7
Hapo niliposongeka nalimwita Bwana, yeye aliye Mungu wangu nikamlalamikia, akaisikia sauti yangu Jumbani mwake, malamamiko yangu yakamwingia masikioni mwake.
8
Nchi ikatukutika na kutetemeka, nayo misingi ya mbingu ikatikisika kwa kutukuswa, kwani aliitolea makali yake yenye moto.
9
Moshi ukapanda puani mwake, moto ulao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yakamulikamulika mbele yake.
10
Akatanda mbingu ya kushukiapo, mawingu meusi yakawa chini ya miguu yake.
11
Akapanda gari, nalo likarushwa, akaonekana mabawani mwa upepo.
12
Akatumia giza kuwa kao, limfunike pande zote, ndio mawingu yenye mvua kali na kimbunga.
13
Kwa nguvu ya kumulika mbele yake yakawashwa makaa ya moto.
14
Bwana akapiga ngurumo kule mbinguni, Alioko huko juu akaivumisha sauti yake.
15
Alipopiga mishale, akawatawanya, ngurumo zilipozidi, wakapigwa bumbuazi.
16
Ndipo, vilipoonekana vilindi vya baharini, nayo misingi ya nchi ikafunuliwa kwa nguvu ya makaripio yake yeye Bwana na kwa ukali wa pumzi ya pua yake.
17
Akakunjua mkono toka juu, akanikamata, mle mlimo na maji mengi akanichopoa.
18
Akaniponya mikononi mwa adui yangu mwenye nguvu namo mwao walionichukia kwa kuwa na uwezo kuliko mimi.
19
Walikuwa wamenijia mbele ile siku, nilipokuwa nimeshindwa, lakini Bwana akanijia kuwa shikizo.
20
Akanitoa kwao, akanikalisha palipo papana; ndivyo, alivyoniopoa kwa kupendezwa nami.
21
Bwana alinipa yaupasayo wongofu wangu, akanipatia tena yaupasayo ung'avu wa mikono yangu.
22
Kwani naliziangalia njia zake Bwana, nisifanye kilicho kiovu mbele yake Mungu wangu.
23
Kwani maamuzi yake yote yako mbele yangu, nayo maongozi yake sikuacha kuyafuata.
24
Nikawa wake pasipo kuonywa, nikajiangalia, nisimkosee.
25
Bwana akanipatia tena yaupasayo wongofu wangu, kwa kuwa nilikuwa nimeng'aa machoni pake.
26
Wewe humwia mpole aliye mpole, naye aliye mkweli wote nawe humwia mkweli wote.
27
Wewe humwia mng'avu aliye mng'avu, lakini aliye mpotovu nawe humpotokea.
28
Walio wanyonge huwaokoa, lakini macho yako huwapingia wajivunao, uwanyenyekeze.
29
Kwani wewe, Bwana, u taa yangu, naye Bwana huliangaza nalo giza langu.
30
Kwani nitashambulia vikosi vizima kwa nguvu yako, kwa nguvu ya Mungu wangu narukia napo ukutani.
31
Njia yake Mungu haipindiki, Neno lake Bwana limeng'azwa, yeye ni ngao yao wote wamkimbiliao.
32
Kwani yuko nani aliye Mungu, asipokuwa Bwana? Tena yuko nani aliye mwamba, asipokuwa Mungu wetu?
33
Mungu ni ngome yangu yenye nguvu, njia yangu huifanya po pote, iwe imenyoka kabisa.
34
Hunipatia miguu ikimbiayo kama ya kulungu, anisimamishe kwangu vilimani juu.
35
Huifundisha mikono yangu kupiga vita, mpaka mikono yangu iweze kupinda hata uta wa shaba.
36
Hunipa ngao ya kuniokoa, napo hapo, unaponinyenyekeza, hunikuza.
37
Huipanulia miguu yangu, ipate pa kupitia, viwiko vya miguu yangu visiteleze.
38
Na niwakimbize adui zangu, mpaka niwaangamize; sitarudi nisipokwisha kuwamaliza.
39
Nitawamaliza na kuwaponda, wasiinuke tena, sharti waanguke miguuni pangu.
40
Hunivika nguvu ya kupiga vita, huwalaza chini yangu wao waniinukiao.
41
Hunipa adui zangu, niwaone migongo, nipate kuwanyamazisha wachukivu wangu.
42
Hakuna mwokozi, wanapolalamika, wanapomwitia Bwana, hawaitikii.
43
Nitawaponda, mpaka wabunguke kama mavumbi ya nchi, nikiisha kuwaseta, niwazoe kama mataka viwanjani.
44
Kwenye magomvi yao walio ukoo wangu ulinitoa, ukaniangalia, nipate kuwa kichwa chao wao wamizimu, watu, ambao nilikuwa siwajui, wanitumikie.
45
Hao watokao mbali hunipongeza, masikio yao yanaponisikia, hunitii.
46
Hao watokao mbali walikuwa wamenyauka walipotoka mabomani kwao na kutetemeka.
47
Bwana Mwenye uzima ni mwamba wangu upasao kusifiwa, yeye Mungu wa mwamba wangu aliyeniokoa sharti atukuke!
48
Mungu ndiye aliyenipatia malipizi na kushurutisha makabila ya watu, wanitii,
49
Ndiye aliyenitoa mikononi mwao walio adui zangu, kwao waniinukiao ukaniweka kuwa mkuu wao, kwao waliozidi kunikorofisha ukaniponya.
50
Kwa hiyo nitakushukuru, Bwana, kwenye wamizimu, nalo Jina lako nitaliimbia.
51
Mfalme wake alimpatia wokovu mwingi, aliyempaka mafuta humfanyizia yenye upole; huyo ni Dawidi naye aliye uzao wake kale na kale.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24