bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 23
2 Samuel 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 24 →
1
Haya ndiyo maneno ya mwisho ya Dawidi: Hivyo ndivyo, asemavyo Dawidi, mwana wa Isai, haya ndiyo, aliyoyasema mtu aliyetukuka sana, Mungu wa Yakobo alimpaka mafuta, kwa kuwatungia Waisiraeli nyimbo alipendeza.
2
Roho ya Bwana hunitumia kuwa wa kusema, Neno lake limo kinywani mwangu.
3
Mungu wa Isiraeli aliniambia neno, aliye mwamba wa Waisiraeli alisema kwamba: Awatawalaye watu kwa wongofu, awatawalaye kwa kumcha Mungu,
4
hufanana na mwanga wa asubuhi, jua linapokucha, huwa kama mapema ya asubuhi yasiyo na mawingu, majani mabichi huchipuka nchini, mvua ikiisha kuanuka; ni kwa nguvu za kuangaza kwake, vikiwa hivyo.
5
Kumbe sivyo, mlango wangu ulivyo kwake Mungu? Kwani aliniwekea agano kuwa la kale na kale, lilitengenezwa, yote yawe sawa, lipate kuangaliwa. Kwa hiyo asiyachipuze yote yawezayo kuniokoa, nayo yote pia yapendezayo?
6
Lakini wao wote wasiofaa ni kama miiba inayotupwa tu, kwani haishikiki mikononi mwa watu.
7
Mtu atakaye kuwajia hutumia vyuma tele na uti wa mkuki, kisha huteketezwa kwa moto papo hapo, walipokuwa.
8
Haya ndiyo majina ya mafundi wa vita, Dawidi alio kuwa nao: Yosebu-Basebeti wa Takemoni, mkuu wa thelathini; yeye aliuchezesha mkuki wake juu ya watu 800; ndio, aliowaua kwa mara moja.
9
Aliyemfuata ni Elazari, mwana wa Dodo, mwana wa mtu wa Ahohi; huyu alikuwa mmoja wao wale mafundi wa vita watatu waliokuwa na Dawidi, Wafilisti walipowatukana na kujipanga huko kupigana nao. Watu wa Waisiraeli walipokwenda zao mahali pa juu,
10
yeye akainuka, akawapiga Wafilisti, mpaka mkono wake ukimlegea kwa kugandamana na upanga. Ilikuwa siku hiyo, Bwana alipowapatia wokovu mkubwa, kisha watu wakarudi na kumfuata, wateke nyara.
11
Aliyefuata ni Sama, mwana wa Age, wa Harari. Wafilisti walipokusanyika wengi mno mahali palipokuwa na kipande cha shamba lenye kunde, watu wakawakimbia Wafilisti;
12
ndipo, yeye alipokuja kusimama katikati ya hicho kipande cha shamba, akakiponya akiwapiga Wafilisti. Ndivyo, Bwana alivyowapatia wokovu mkubwa.
13
Ikawa, hawa wakuu watatu waliomo miongoni mwao wakuu wa 30 wakashuka siku za mavuno, wafike kwa Dawidi penye pango la Adulamu; navyo vikosi vya Wafilisti vilikuwa vimepiga makambi Bondeni kwa Majitu.
14
Naye Dawidi siku zile alikuwa ngomeni, nacho kikosi cha walinzi wa Wafilisti kilikuwamo Beti-Lehemu.
15
Hapo Dawidi akaingiwa na tamaa, akasema: Yuko nani atakayeninywesha maji ya kisima cha Beti-Lehemu kilichoko langoni?
16
Ndipo, wale mafundi wa vita watatu walipojipenyeza makambini mwa Wafilisti, wakachota maji katika kisima cha Beti-Lehemu kilichoko langoni, wakayachukua, wakamletea Dawidi, lakini hakutaka kuyanywa, akammwagia Bwana kuwa kinywaji cha tambiko,
17
akasema: Bwana na anizuie, nisifanye kama hayo! Kumbe siyo damu za waume hao waliokwenda kwa kujitoa wenyewe? Kwa hiyo hakutaka kuyanywa. Haya waliyafanya wale mafundi wa vita watatu.
18
Naye Abisai, ndugu yake Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu miongoni mwa watu watatu; yeye ndiye aliyeuchezesha mkuki wake juu ya watu 300; ndio, aliowaua, akawa mwenye macheo kwa hao watatu.
19
Kwao hao watatu aliheshimiwa kweli kuliko wengine, akawa mkuu wao, lakini wale watatu wa kwanza hakuwa sawa nao.
20
Benaya, mwana wa Yoyada, mwana wa mtu mwenye nguvu, alifanya matendo makuu, nako kwao kulikuwa Kabuseli. Yeye aliwaua wana wawili wa Arieli wa Moabu, tena siku moja, theluji ilipokuwa imeanguka, akashuka shimoni, akaua simba mlemle.
21
Naye ndiye aliyemwua mtu wa Misri aliyetisha kwa kutazamwa tu; namo mkononi mwake huyu Mmisri alishika mkuki. Lakini akamshukia na kushika fimbo tu, akampokonya yule Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa huo mkuki wake.
22
Haya aliyafanya Benaya, mwana wa Yoyada, kwa hiyo alipata macheo kwa hao mafundi wa vita watatu.
23
Kwa wale 30 aliheshimiwa kuliko wenziwe, lakini wale watatu wa kwanza hakuwa sawa nao. Naye Dawidi akamweka kuwa mkuu wa walinzi wake.
24
Miongoni mwao wakuu wa 30 walikuwa: Asaheli, ndugu yake Yoabu; Elihanani, mwana wa Dodo wa Beti-Lehemu;
25
Sama wa Harodi, Elika wa Harodi;
26
Helesi wa Palti, Ira, mwana wa Ikesi, wa Tekoa;
27
Abiezeri wa Anatoti, Mebunai wa Husa;
28
Salmoni wa Ahohi, Maharai wa Netofa;
29
Helebu, mwana wa Baana, wa Netofa, Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini;
30
Benaya wa Piratoni, Hidai wa Nahale-Gasi;
31
Abi-Alboni wa Araba, Azimaweti wa Barihumu;
32
Eliaba wa Salaboni, Yonatani wa wana wa Yaseni;
33
Sama wa Harari, Ahiamu, mwana wa Sarari, wa Arari;
34
Elifeleti, mwana wa Ahasibai, mwana wa mtu wa Maka, Eliamu, mwana wa Ahitofeli, wa Gilo;
35
Hesirai wa Karmeli, Parai wa Arabu;
36
Igali, mwana wa Natani wa Soba, Bani wa Gadi;
37
Mwamoni Seleki, Naharai wa Beroti aliyekuwa mchukua mata wa Yoabu, mwana wa Seruya;
38
Mwitiri Ira, Mwitiri Garebu;
39
Mhiti Uria. Wote pamoja ni 37.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24