bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 13
2 Samuel 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 14 →
1
Hayo yalipokwisha kufanyika, Abisalomu, mwana wa Dawidi, alikuwa na umbu lake, jina lake Tamari, naye alikuwa mzuri; kwa hiyo Amunoni, mwana wa Dawidi, akampenda.
2
Naye Amunoni akasongeka moyoni, akapata kuwa mgonjwa kwa ajili ya umbu lake Tamari, kwani alikuwa mwanamwali, naye Amunoni akaviona kuwa vigumu sana kumfanyizia lo lote.
3
Lakini Amunoni alikuwa na mwenzake, jina lake Yonadabu, mwana wa Simea, kaka yake Dawidi; huyu Yonadabu alikuwa mwerevu sana.
4
Huyu akamwuliza: Mbona wewe, mwana wa mfalme, unanyongeka hivyo kila kunapokucha? Huwezi kunisimulia sababu yake? Ndipo, Amunoni alipomwambia: Mimi nampenda Tamari, umbu lake ndugu yangu Abisalomu.
5
Yonadabu akamwambia: Lala kitandani pako kuwa kama mgonjwa sana! Kisha baba yako akija kukutazama, umwambie: Kama umbu langu Tamari angekuja kuniandalia chakula na kukitengeneza hicho chakula machoni pangu, nipate kuviona, basi, ningekula na kuvipokea mkononi mwake.
6
Kwa hiyo Amunoni akalala kitandani kuwa kama mgonjwa. Mfalme alipokuja kumtazama, Amunoni akamwambia mfalme: Kama umbu langu Tamari angekuja kuandalia machoni pangu vikate viwili, ningevila na kuvipokea mkononi mwake.
7
Ndipo, Dawidi alipomtuma Tamari kwenda mle nyumbani kwamba: Nenda nyumbani mwa umbu lako Amunoni, umtengenezee chakula!
8
Ndipo, Tamari alipokwenda nyumbani mwa umbu lake Amunoni, naye alikuwa amelala; akachukua unga, akaukanda, akautengeneza machoni pake kuwa vikate, akavioka hivyo vikate.
9
Kisha akakichukua kikaango, akavitia katika sahani machoni pake, lakini Amunoni akakataa kuvila, akasema: Watoeni watu wote humu mwangu! Walipokwisha kuwatoa watu wote mwake,
10
Amunoni akamwambia Tamari: Kilete hicho chakula chumbani humu, nikile na kukipokea mkononi mwako! Tamari akavichukua hivyo vikate, alivyovitengeneza, akampelekea umbu lake Amunoni mle chumbani.
11
Alipompa, avile, akamshika na kumwambia: Njoo, umbu langu, ulale kwangu!
12
Lakini akamwambia: Sivyo, umbu langu, usinichukue kwa nguvu. Kwani mambo kama hayo hayafanywi kwao Waisiraeli, nawe usiufanye upumbavu huu!
13
Mimi nami nitakwenda wapi nikitwezwa hivyo? Wewe nawe utakuwa mpumbavu mwenzao walio hivyo kwao Waisiraeli. Ila sema na mfalme sasa, kwani hatakukataza kunioa.
14
Lakini hakutaka kuyasikia, aliyomwambia, akamkamata kwa nguvu na kumshurutiza, mpaka akimpata, alale naye.
15
Kisha Amunoni akaingiwa na machukizo makubwa sana ya kuchukizwa naye, nayo hayo machukizo yake ya kuchukizwa naye yakawa makubwa kuliko ule upendo wake wa kwanza wa kumpenda; kwa hiyo Amunoni akamwambia: Ondoka, uende zako!
16
Naye akamwambia: La, sivyo! Kibaya hiki cha kunifukuza kingekuwa kikubwa kuliko kile, ulichonifanyizia, lakini akakataa kumsikia,
17
akamwita kijana aliyemtumikia, akamwambia: Mtoeni huyu humu mwangu, aende nje! Tena funga mlango, akiisha kutoka.
18
Naye alikuwa amevaa rinda refu la nguo za rangi, kwani ndiyo mavazi, watoto wa kike wa mfalme waliyoyavaa siku za kuwa wanawali. Yule mtumishi wake alipomtoa nje na kufunga mlango, alipokwisha kutoka,
19
Tamari akachukua uvumbi, akautia kichwani pake, akalirarua lile rinda la nguo za rangi, alilokuwa amelivaa, akabandika mkono kichwani pake, akaenda zake na kulia.
20
Ndipo, Abisalomu alipomwuliza umbu lake: Umbu lako Amunoni amekuwa kwako? Umbu langu, sasa nyamaza tu! Ndiye umbu lako. Neno hili usiliweke moyoni mwako! Basi, Tamari akakaa na ukiwa wake nyumbani mwa Abisalomu, umbu lake.
21
Mfalme Dawidi alipoyasikia mambo haya, akachafuka sana.
22
Lakini Abisalomu hakusema na Amunoni wala neno baya wala jema, kwani Abisalomu alimchukia Amunoni, kwa kuwa alimchukua umbu lake Tamari kwa nguvu.
23
Miaka miwili ilipopita, Abisalomu akajipatia watu wa kukata manyoya ya kondoo kule Baali-Hasori upande wa Efuraimu; ndipo, Abisalomu alipowaalika wana wote wa mfalme.
24
Abisalomu akaja hata kwa mfalme, akamwambia: Tazama, wako wenye kukata manyoya ya kondoo kwa mtumishi wako, mfalme naye na aje pamoja na watumishi wake kwa mtumishi wako!
25
Mfalme akamwambia Abisalomu: Sivyo, mwanangu, tusije sote kwako, tusikulemee. Hata alipomhimiza, hakutaka kwenda, ila akambariki.
26
Abisalomu akamwambia: Kama huji, ndugu yangu Amunoni na aende na sisi. Mfalme akamwuliza: Unamtakia nini kwenda na wewe?
27
Abisalomu alipomhimiza, akampa Amunoni ruhusa kwenda pamoja naye pamoja na wana wote wa mfalme.
28
Kisha Abisalomu akawaagiza vijana wake kwamba: Angalieni! Moyo wa Amunoni utakapochangamka kwa kunywa mvinyo, nitawaambieni: Mpigeni Amunoni! Ndipo, mtakapomwua pasipo kuogopa. Kwani ni mimi ninayewaagiza ninyi kuvifanya. Jipeni mioyo, mpate kuwa wenye nguvu!
29
Vijana wa Abisalomu wakamfanyizia Amunoni, kama Abisalomu alivyowaagiza. Ndipo, wana wote wa mfalme walipoondoka, wakapanda kila mmoja nyumbu wake, wakakimbia.
30
Hao walipokuwa njiani, Dawidi akapata habari kwamba: Abisalomu amewaua wana wote wa mfalme, asisalie kwao hata mmoja.
31
Ndipo, mfalme alipoinuka, akayararua mavazi yake, akajilaza chini, nao watumishi wake wote wakawa wamesimama wenye mavazi yaliyoraruliwa.
32
Naye Yonadabu, mwana wa Simea, kaka yake Dawidi, akaanza kusema kwamba: Bwana wangu asiwaze, ya kwamba wamewaua vijana wote walio wana wa mfalme, kwani Amunoni amekufa peke yake, kwani shauri hili lilikuwa limekatwa na kinywa chake Abisalomu tangu siku ile, yule alipomchukua umbu lake Tamari kwa nguvu.
33
Sasa bwana wangu mfalme asiliweke neno hili moyoni mwake la kwamba: Wana wote wa mfalme wamekufa! Ila ni Amunoni peke yake aliyekufa.
34
Lakini Abisalomu alikuwa amekimbia. Kijana wa mfalme aliyekuwa mlinzi alipoyainua macho yake, aone vema, mara akaona watu wengi wanaotelemka katika njia iliyoko mgongoni kwake upande wa milimani.
35
Ndipo, Yonadabu alipomwambia mfalme: Tazama, wana wa mfalme wanakuja! Kama mtumishi wako alivyosema, ndivyo, inavyokuwa.
36
Alipokwisha kusema, ndipo, wana wa mfalme walipofika, wakapaza sauti zao, wakalia; naye mfalme na watumishi wake wote wakalia kilio kikubwa sana.
37
Abisalomu alipokimbia akaenda kwa Talmai, mwana wa Amihudi, mfalme wa Gesuri. Naye Dawidi akamlilia mwanawe kila siku.
38
Naye Abisalomu akakaa miaka mitatu kule Gesuri, alikokwenda kwa kukukimbilia.
39
Naye mfalme Dawidi akatamani sana kwenda kumtokea Abisalomu, alipokwisha kuutuliza moyo wake kwa ajili ya kufa kwake Amunoni.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24