bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 16
2 Samuel 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 17 →
1
Dawidi alipokwisha kupita kidogo hapo kilimani juu, mara Siba, kijana wa Mefiboseti, akamwendea njiani, anao punda wawili waliotandikwa kuchukua mikate 200 na maandazi 100 ya zabibu na maandazi 100 ya kuyu na kiriba cha mvinyo.
2
Mfalme alipomwuliza: Haya unanileteaje? Siba akasema: Punda ni wa kuchukua walio wa mlango wa mfalme, nayo mikate na maandazi ni ya kula ya vijana, nayo mvinyo ni ya kunywa, mtu akichoka nyikani.
3
Mfalme akamwuliza: Naye mwana wa bwana wako yuko wapi? Ndipo, Siba alipomwambia mfalme: Tazama, anakaa Yerusalemu, kwani amesema: Leo wao wa mlango wa Isiraeli watanirudishia ufalme wa baba yangu.
4
Ndipo, mfalme alipomwambia Siba: Tazama, mali zote za Mefiboseti ni zako! Siba naye akasema: Ninakuangukia, nione tena upendeleo machoni pako, bwana wangu mfalme!
5
Mfalme Dawidi alipofika Bahurimu, mara mle akatoka mtu wa ukoo wao walio mlango wa Sauli, jina lake Simei, mwana wa Gera; alipotoka alikwenda akitukana.
6
Tena akamtupia Dawidi mawe nao watumishi wote wa mfalme Dawidi, nao watu wote na mafundi wa vita wote walikuwa kuumeni na kushotoni kwake.
7
Hivi ndivyo, Simei alivyosema akitukana: Toka! Toka, wewe mtu wa damu, wewe mtu usiyefaa!
8
Bwana anakulipisha damu zao wote walio wa mlango wa Sauli, ambaye umejifanya kuwa mfalme mahali pake. Yeye Bwana ameutia ufalme mkononi mwa mwanao Abisalomu, wewe nawe umepatwa na mabaya, kwa kuwa wewe u mtu wa damu.
9
Ndipo, Abisai, mwana wa Seruya, alipomwambia mfalme: Mbona mbwa mfu huyu anamtukana bwana wangu mfalme? Acha, nimwendee, nimkate kichwa mara moja!
10
Lakini mfalme akasema: Tuna bia gani mimi nanyi, wana wa Seruya? Na atukane hivyo; kama Bwana amemwagiza: Mtukane Dawidi! yuko nani awezaye kusema: Mbona unafanya hivyo?
11
Kisha Dawidi akamwambia Abisai na watumishi wake wote: Tazameni, mwanangu aliyetoka kiunoni mwangu anaitaka roho yangu! Sasa huyu mtu wa Benyamini anafanya nini? Mwacheni, atukane, kwani Bwana amemwagiza hivyo.
12
Labda Bwana atautazama ukiwa wangu, yeye Bwana anirudishie mema kwa hivyo, huyu anavyonitukana leo hivi.
13
Kisha Dawidi akaenda zake na watu wake, Simei naye akaenda kandokando ya mlima karibu yake akiendelea kutukana na kumtupia mawe na kumpiga kokotokokoto.
14
Mfalme na watu wote waliokuwa naye walipofika mahali fulani walikuwa wamechoka, wakapumzika hapo.
15
Abisalomu na Waisiraeli wote walipoingia Yerusalemu, Ahitofeli alikuwa naye.
16
Ikawa, Mwarki Husai, yule rafiki yake Dawidi, alipofika kwa Abisalomu, Husai akamwambia Abisalomu: Pongezi, mfalme! Pongezi, mfalme!
17
Abisalomu akamwuliza Husai: Huu ndio welekevu, unaomfanyizia rafiki yako? Mbona hukuenda pamoja na rafiki yako?
18
Husai akamwambia Abisalomu: Sivyo! Ila yule, Bwana aliyemchagua na watu hawa wote na waume wote wa Waisiraeli, basi, nami ni mtu wake, nikae naye!
19
Tena nimtumikie nani? Siye mwanawe? Kama nilivyomtumikia baba yako, ndivyo, nitavyokutumikia.
20
Abisalomu akamwambia Ahitofeli: Haya! Nipeni shauri, jinsi tutakavyofanya!
21
Ahitofeli akamwambia Abisalomu: Ingia kwao masuria wa baba yako, aliowaacha kuiangalia nyumba! Hapo, Waisiraeli wote watakaposikia, ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako, ndipo, mikono yao wote waliorudi upande wako itakapopata nguvu.
22
Kisha wakampigia Abisalomu hema darini, naye Abisalomu akaingia kwao masuria wa baba yake machoni pao Waisiraeli wote.
23
Siku zile shauri, alilolitoa Ahitofeli likawa sawa na neno, mtu aliloliuliza kwake Mungu. Ndivyo, mashauri yote ya Ahitofeli, yalivyowaziwa kuwa, kama siku za Dawidi, vivyo hivyo hata siku za Abisalomu.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24