bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 15
2 Samuel 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 16 →
1
Hayo yalipokwisha, Abisalomu akajipatia magari na farasi na watu 50, wamtangulie na kupiga mbio.
2
Kila siku Abisalomu hujidamka, kisha husimama mjini kando kwenye lango la mji. Basi, kila mtu aliyepita mwenye shauri la kwenda kwa mfalme kuamuliwa, Abisalomu humwita kwake na kumwuliza: Wewe unatoka mji gani? Aliposema: Mtumishi wako ni mmoja wao wa mashina ya Waisiraeli,
3
Abisalomu humwambia: Tazama, shauri lako ni zuri, linapasa, lakini kwa mfalme hakuna atakayekusikiliza.
4
Kisha Abisalomu husema: Kama wangeniweka mimi kuwa mwamuzi katika nchi hii, ningeyakata vema mashauri ya kila mtu atakayekuja kwangu mwenye neno la kugombana na mwenye shauri lo lote.
5
Napo, mtu alipomkaribia, amwangukie, hukunjua upesi mkono wake, apate kumnonea.
6
Hivyo ndivyo, Abisalomu alivyowafanyizia Waisiraeli wote waliokwenda shaurini kwa mfalme, navyo ndivyo, alivyoiiba mioyo ya waume wa Waisiraeli.
7
Miaka 40 ilipokwisha, Abisalomu akamwambia mfalme: Na niende kumlipa Bwana huko Heburoni, niliyomwapia ya kumtolea.
8
Kwani mtumishi wako ameapa kiapo, nilipokaa Gesuri kwa Washami, cha kwamba: Kama Bwana atanirudisha Yerusalemu, nitamtumikia Bwana.
9
Mfalme akamwambia: Nenda na kutengemana! Basi, akaondoka, akaenda Heburoni.
10
Kisha Abisalomu akatuma wapelelezi kwa mashina yote ya Waisiraeli kwamba: Mtakaposikia, mabaragumu yakilia, semeni: Abisalomu amepata ufalme Heburoni!
11
Pamoja na Abisalomu walikwenda toka Yerusalemu watu 200 walioalikwa naye, waliokwenda pasipo mawazo mabaya yo yote, maana hawakujua neno lo lote.
12
Abisalomu akatuma kumchukua Ahitofeli wa Gilo aliyekuwa mmoja wao waliomwongoza Dawidi mashaurini; akamtoa huko Gilo mjini kwake, alipochinja ng'ombe za tambiko. Hivyo lile fujo likapata nguvu, nao watu waliorudi upande wa Abisalomu wakaendelea kuwa wengi zaidi.
13
Mtu alipofika kwa Dawidi na kumpasha habari ya kwamba: Mioyo ya waume wa Waisiraeli imegeuka kumfuata Abisalomu,
14
Dawidi akawaambia watumishi wake wote, aliokuwa nao Yerusalemu: Haya! Ondokeni, tukimbie! Kwani hatutapata kupona, Abisalomu akitujia. Pigeni mbio, twende, asitukamate upesi na kutufanyizia mabaya, akiwaua waliomo humu mjini kwa ukali wa panga.
15
Watumishi wa mfalme wakamwambia mfalme: Yote yampendezayo bwana wetu mfalme, basi, sisi watumishi wako tuko.
16
Kisha mfalme akatoka pamoja nao wote waliokuwamo nyumbani mwake, wakienda kwa miguu yao; mfalme akaacha masuria kumi tu wa kuiangalia nyumba.
17
Mfalme alipokwisha kutoka hivyo pamoja na watu wake wote, wakienda kwa miguu, wakasimama penye nyumba ya mwisho.
18
Ndipo, watumishi wake wote walipopita kando yake, nao Wakreti wote na Wapuleti wote na Wagati wote, watu 600 waliotoka Gati wakienda kwa miguu, wote pia wakapita hapo mbele ya mfalme.
19
Mfalme akamwuliza Itai wa Gati: Mbona wewe nawe utakwenda pamoja na sisi? Rudi, ukae kwa mfalme! Kwani wewe u mgeni aliyefukuzwa kwao; haya! Nenda zako!
20
Umefika jana; basi, leo nitawezaje kukusumbua na kukuchukua kwenda na sisi? Mimi ninakwenda na kutangatanga po pote, nitakapokwenda, lakini wewe rudi! Nao ndugu zako warudishe pamoja na wewe, nao upole na welekevu na uwakalie!
21
Itai akamjibu mfalme akisema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, tena bwana wangu mfalme alivyo mzima, mahali, bwana wangu mfalme atakapokuwa, kama ni pa kufia, au kama ni pa kuponea, ndipo, mtumishi wako naye atakapokuwa.
22
Ndipo, Dawidi alipomwambia Itai: Basi, nenda nawe, upite! Naye Itai wa Gati akapita na watu wake wote na wake na watoto wote waliokuwa naye.
23
Watu wote wa nchi hiyo wakalia na kuzipaza sauti zao pamoja na watu wote walipita hapo, mfalme alipouvuka mto wa Kidoroni pamoja na wale watu wote waliopita mbele yake, wakajielekeza kushika njia ya kwenda nyikani.
24
Mara akaja naye Sadoki pamoja na Walawi wote waliolichukua Sanduku la Agano la Mungu; wakalitua Sanduku la Agano, naye Abiatari akatambika, mpaka watu wote walipokwisha kupita na kutoka mjini.
25
Mfalme akamwambia Sadoki: Lirudishe mjini Sanduku la Mungu! Kama nitaona upendeleo machoni pa Bwana, atanirudisha, nipate kuliona tena napo mahali, linapokaa.
26
Lakini kama ataniambia hivi: Sipendezwi na wewe, basi, niko, anifanyizie atakayoyaona kuwa mema.
27
Kisha mfalme akamwambia mtambikaji Sadoki: Je? Wewe siwe mtazamaji? Rudi mjini na kutengemana pamoja na mwanao Ahimasi na Yonatani, mwana wa Abiatari, hawa wana wenu wawili waende nanyi.
28
Tazameni, mimi nitakawilia penye mbuga za nyikani, mpaka itafika kwangu habari toka kwenu.
29
Kwa hiyo Sadoki na Abiatari wakalirudisha Sanduku la Mungu Yerusalemu, wakakaa huko.
30
Dawidi akapapanda pa kuukwelea mlima wa michekele, akaenda akilia, nacho kichwa chake kilikuwa kimefunikwa, naye mwenyewe alikwenda pasipo kuvaa viatu; hata watu wote waliokuwa naye walikuwa wamekifunika kila mtu kichwa chake, nao wakawa wakipanda na kulia.
31
Walipompasha Dawidi habari ya kwamba: Ahitofeli yuko kwa Abisalomu pamoja nao waliovunja maagano, Dawidi akasema: Bwana na aligeuze shauri la Ahitofeli kuwa ujinga!
32
Dawidi alipofika pale juu, watu wanapomtambikia Mungu, mara akaja Mwarki Husai akimwendea njiani mwenye kanzu iliyoraruliwa na mwenye mchanga kichwani pake.
33
Dawidi akamwambia: Ukienda pamoja nami safari yangu, ndipo, utakaponilemea.
34
Lakini ukirudi mjini na kumwambia Abisalomu: Mimi nitakuwa mtumishi wako, mfalme; kama nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tangu kale, ndivyo, nitakavyokuwa sasa mtumishi wako. Basi, ndivyo, utakavyolitengua shauri la Ahitofeli.
35
Je? Mle mjini hunao wale watambikaji Sadoki na Abiatari? Iwe hivyo: kila neno, utakalolisikia nyumbani mwa mfalme, uwasimulie wale watambikaji Sadoki na Abiatari.
36
Tazama, wanao mle mjini wana wao wawili: Sadoki anaye Ahimasi, Abiatari anaye Yonatani. Kwa kuwatumia hao mtaweza kuniletea kila neno, mtakalolisikia.
37
Ndipo, Husai aliyekuwa rafiki yake Dawidi aliporudi mjini, Abisalomu alipoingia Yerusalemu.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24