bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 21
2 Samuel 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 22 →
1
Katika siku za Dawidi kulikuwa na njaa mwaka kwa mwaka, miaka mitatu; naye Dawidi alipoutafuta uso wa Bwana, Bwana akasema: Ziko manza za damu, Sauli nao wa mlango wake walizozikora walipowaua watu wa Gibeoni.
2
Ndipo, mfalme alipowaita Wagibeoni kusema nao; nao Wagibeoni hawakuwa wana wa Isiraeli, ila walikuwa masao yao Waamori, nao wana wa Isiraeli walikuwa wamefanya maagano nao na kuapa, lakini Sauli alitaka kuwaua kwa kuona wivu kwa ajili ya wana wa Isiraeli na wa Yuda.
3
Ndipo, Dawidi alipowauliza Wagibeoni: Niwafanyizie nini? Tena yale makosa niyalipe namna gani, mpate kuwabariki walio fungu lake Bwana?
4
Wagibeoni wakamwambia: Sisi hatutaki fedha wala dhahabu kwake Sauli, wala kwao walio wa mlango wake, tena haitupasi kuua watu wa kwao Waisiraeli. Alipouliza tena: Mwasemaje? Niwafanyizie nini?
5
wakamwambia mfalme: Yule mtu aliyetumaliza kwa kutaka kutuangamiza kabisa, tusikae tena katika mipaka yote ya Waisiraeli,
6
basi, na tupewe wanawe saba, tuwanyonge machoni pa Bwana kule Gibea kwa Sauli aliyekuwa mteule wa Bwana. Mfalme akawaambia: Mimi nitawapa.
7
Mfalme akamhurumia Mefiboseti, mwana wa Yonatani, mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo, alichokiapa na kumtaja Bwana, awe shahidi wao, yeye Dawidi naye Yonatani, mwana wa Sauli.
8
Kwa hiyo mfalme akachukua wana wawili wa Risipa, binti Aya, aliomzalia Sauli, ndio Armoni na Mefiboseti, na wana watano wa Mikali, binti Sauli aliomzalia Adirieli, mwana wa Barzilai wa Mehola.
9
Akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawanyonga mlimani juu machoni pa Bwana; nao wote saba wakauawa pamoja; walipouawa, ni siku za kwanza za mavuno, watu walipoanza kuvuna mawele.
10
Kisha Risipa, binti Aya, akachukua gunia, akalitandika la kulalia mwambani juu tangu hapo, watu walipoanza kuvuna, mpaka mvua zitokazo mbinguni zikawanyeshea wale wafu, hakuacha ndege wa angani kuwakalia mchana, wala nyama wa porini kuwafikia usiku.
11
Dawidi alipopashwa habari za mambo hayo, Risipa, binti Aya, suria yake Sauli, aliyoyafanya,
12
Dawidi akaenda akaichukua mifupa ya Sauli nayo mifupa ya mwanawe Yonatani kwa wenyeji wa Yabesi wa Gileadi walioiiba uwanjani kwa Beti-Sani; ndiko, Wafilisti walikoitungika siku hiyo, Wafilisti walipomwua Sauli huko Gilboa.
13
Alipoichukua huko mifupa ya Sauli na mifupa ya mwanawe Yonatani, wakaikusanya nayo mifupa yao hao walionyongwa,
14
wakaizika mifupa ya Sauli nayo ya mwanawe Yonatani katika nchi ya Benyamini kule Sela kaburini kwa baba yake Kisi. Walipokwisha kuyafanya yote, mfalme aliyoyaagiza, baadaye Mungu akasikia alipoombwa kwa ajili ya nchi hiyo.
15
Baadaye Wafilisti walipokuja tena kupigana na Waisiraeli, Dawidi akashuka pamoja na watumishi wake. Walipopigana na Wafilisti, Dawidi akachoka.
16
Ndipo, alipotokea Isibi-Benobu aliyekuwa mmoja wao yale Majitu marefu; huyu alikuwa na mkuki wenye ncha ya shaba, nayo ilipopimwa, uzito wake ulikuwa sekeli 300, ndio nusu ya frasila; naye alikuwa amejifunga mata mapya, akataka kumwua Dawidi.
17
Ndipo, Abisai, mwana wa Seruya, alipomsaidia na kumpiga yule Mfilisti, hata akafa. Hapo ndipo, watumishi wa Dawidi walipomwapia kwamba: Wewe hutatoka tena pamoja na sisi kwenda vitani, usiizime taa ya waisiraeli!
18
Hayo yalipokwisha yakawa mapigano mengine nao Wafilisti kule Gobu; ndiko, Sibekai wa Husa alikomwua Safu aliyekuwa naye mmoja wao yale Majitu marefu.
19
Kisha kule Gobu yakawa mapigano mengine na Wafilisti; ndiko, Elihanani wa Beti-Lehemu, mwana wa Yare-Orgimu, alikomwua Goliati wa Gati; huyu uti wa mkuki wake ulikuwa kama majiti ya wafuma nguo.
20
Kisha yakawa mapigano tena kule Gati; huko kulikuwa na mtu mrefu sana, vidole vya mikono yake na vidole vya miguu yake vilikuwa sita sita, vyote pamoja ni 24, naye alikuwa amezaliwa kwao yale Majitu marefu.
21
Alipowatukana Waisiraeli, Yonatani, mwana wa Simea, kaka yake Dawidi, akamwua.
22
Hawa wanne walizaliwa Gati kwao yale Majitu marefu, wakauawa kwa mikono ya Dawidi na kwa mikono ya watumishi wake.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24