bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 7
2 Samuel 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 8 →
1
Ikawa, mfalme alipokaa nyumbani mwake, kwa kuwa Bwana alikuwa amemtuliza akiwanyamazisha adui zake zote waliomzunguka,
2
ndipo, mfalme alipomwambia mfumbuaji Natani: Tazama, mimi ninakaa katika nyumba iliyojengwa kwa miangati, lakini Sanduku la Mungu linakaa katika mapazia tu.
3
Natani akamwambia mfalme: Yote yaliyomo moyoni mwako nenda, uyafanye! Kwani Bwana yuko pamoja na wewe.
4
Lakini usiku uleule neno la Bwana likamjia Natani kwamba:
5
Nenda, umwambie mtumishi wangu Dawidi: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Wewe unijengee nyumba, nikae?
6
Kwani sikukaa nyumbani tangu siku ile, nilipowatoa wana wa Isiraeli huko Misri nikiwaleta huku, mpaka siku hii ya leo, nikawa nikienda na kukaa katika hema lililokuwa Kao langu.
7
Je? Hapo pote, nilipokwenda pamoja na wana wote wa Isiraeli, nilimwambia hata mmoja wao wa mashina ya Waisiraeli, niliowaagiza kuwachunga walio ukoo wangu wa Waisiraeli, na kumwuliza neno la kwamba: Mbona hamnijengei nyumba ya miangati?
8
Kwa hiyo umwambie sasa mtumishi wangu Dawidi: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Mimi nilikuchukua malishoni, ulipowafuata kondoo, uwe mwenye kuwatawala walio ukoo wangu wa Waisiraeli.
9
Nikawa pamoja na wewe po pote, ulipokwenda, nikawaangamiza adui zako wote mbele yako; nitakupatia jina kubwa lililo sawa na majina ya wakubwa walioko huku nchini.
10
Nao walio ukoo wangu wa Waisiraeli nitawapatia mahali, nitakapowapanda, wapate kukaa hapo pasipo kuhangaika tena, wala watu waovu wasiwakorofishe tena kama huko kwanza
11
tangu siku zile, nilipowaagiza waamuzi, wawatawale walio ukoo wangu wa Waisiraeli. Lakini wewe nitakupa kutulia nikiwanyamazisha adui zako wote, nawe wewe Bwana anakupasha habari, ya kuwa yeye Bwana atakutengenezea nyumba.
12
Kwani siku zako zitakapotimia, uende kulala pamoja na baba zako, ndipo, nitakapoinua nyuma yako mzao wako atakayetoka mwilini mwako, niusimike ufalme wake.
13
Yeye ndiye atakayelijengea Jina langu nyumba, nami nitakisimamisha kiti cha ufalme wake, kipate kuwapo kale na kale.
14
Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; atakapofanya kiovu, nitamchapa kwa fimbo ya kiwatu na kwa mapigo yapasayo wana wa watu.
15
Lakini upole wangu hautaondoka kwake, kama nilivyouondoa kwake Sauli, nilipomwondoa usoni pako.
16
Mlango wako na ufalme wako utakuwa umeshupaa kale na kale machoni pako, nacho kiti chako cha kifalme kitakuwa kimesimamishwa kale na kale.
17
*Natani akamwambia Dawidi haya maneno yote sawasawa, kama alivyoambiwa mwenyewe na kuonyeshwa.
18
Kisha mfalme Dawidi akaingia pake Bwana, akakaa hapo akisema: Bwana Mungu, mimi ni nani? nao mlango wangu ni nini, ukinileta, nifike hapa?
19
Lakini hayo yakawa madogo machoni pako, Bwana Mungu, kwa hiyo umeyasema yatakayoujia mlango wa mtumishi wako katika siku zilizo mbali bado, hayo nayo umeyasema kimtu, Bwana Mungu.
20
Dawidi akuambie nini tena? Maana wewe unamjua mtumishi wako, Bwana Mungu.
21
Kwa ajili ya Neno lako na kwa mapenzi ya moyo wako umeyafanya hayo makubwa yote, umjulishe mtumishi wako.
22
Kwa hiyo u mkubwa, Bwana Mungu, kwani hakuna anayefanana na wewe, hakuna Mungu, asipokuwa wewe, kwa hayo yote, tuliyoyasikia kwa masikio yetu.
23
Tena liko taifa moja tu huku nchini linalofanana na ukoo wako wa Waisiraeli? Hao ndio, Mungu aliokwenda kuwakomboa, wawe ukoo wake, ajipatie Jina kwa kufanya kwao katika nchi yako matendo makubwa yanayoogopesha, ulipofukuza wamizimu na miungu yao mbele yao walio ukoo wako, uliowakomboa, wawe wako, ulipowatoa huko Misri.
24
Ukajiwekea ukoo wako wa Waisiraeli kuwa ukoo wako kale na kale, wewe Bwana ukawa Mungu wao.
25
Sasa, Bwana Mungu, neno hilo, ulilolisema la mtumishi wako na la mlango wake, lisimamishe kuwapo kale na kale ukifanya, kama ulivyosema!
26
Ndivyo, Jina lako litakavyokuwa kubwa kale na kale kwamba: Bwana Mwenye vikosi ni Mungu wa Isiraeli, tena ndivyo, mlango wa mtumishi wako Dawidi utakavyokuwa wenye nguvu mbele yako.
27
Kwani wewe Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, umelifunua sikio la mtumishi wako, asikie ya kwamba: Mimi nitakujengea nyumba. Kwa hiyo mtumishi wako amejipa moyo wa kukuomba maombo haya.
28
Sasa Bwana Mungu, wewe ndiwe Mungu; kwa hiyo maneno yako yatatimia kweli, hayo mema, uliyomwambia mtumishi wako, yapate kuwa.
29
Sasa na ikupendeze kuubariki mlango wa mtumishi wako, uwepo kale na kale usoni pako! Kwani wewe, Bwana Mungu, umeyasema; kwa hiyo mlango wa mtumishi wako utakuwa umebarikiwa kale na kale kwa kuipata mbaraka yako.*
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24