bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 8
2 Samuel 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 9 →
1
Hayo yalipokwisha, Dawidi akawapiga Wafilisti, akawashinda; kisha Dawidi akaishika mwenyewe hatamu ya mji mkuu, isishikwe tena na Wafilisti.
2
Nao Wamoabu akawapiga, akawapima kwa kamba akiwalaza chini, akapima hivyo: wa kamba mbili wakawa wa kuuawa, nao wote wa kamba moja wakawa wa kuachwa uzimani; nao Wamoabu wakawa watumishi wa Dawidi, wakamletea mahongo.
3
Kisha Dawidi akampiga Hadadezeri, mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, alipokwenda kuusimika tena ufalme wake huko kwenye jito la Furati.
4
Dawidi akateka kwake wapanda farasi 1700 na askari waliokwenda kwa miguu 20000, nao farasi wote wa kuvuta magari Dawidi akawakata mishipa, akajisazia farasi wa magari mia tu.
5
Washami Wa Damasko walipokuja kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Dawidi akapiga kwao Washami watu 22000.
6
Dawidi akaweka askari kwao Washami wa Damasko, hao Washami wakawa watumishi wa Dawidi, wakamletea mahongo, ndivyo, Bwana alivyompa Dawidi kushinda po pote, alipokwenda.
7
Dawidi akazichukua ngao za dhahabu, watumishi wa Hadadezeri walizokuwa nazo, akazipeleka Yerusalemu.
8
Namo mle Beta na Berotai iliyokuwa miji ya Hadadezeri Dawidi akachukua shaba nyekundu nyingi mno.
9
Toi, mfalme wa Hamati, aliposikia, ya kuwa Dawidi amevipiga vikosi vyote vya Hadadezeri,
10
Toi akamtuma mwanawe Yoramu kwake mfalme Dawidi kumpongeza na kumbariki, kwa kuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda, kwani Toi na Hadadezeri walikuwa wakipigana vita, naye akampelekea mkononi mwake vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu na vyombo vya shaba.
11
Hivi navyo mfalme Dawidi akavitakasa kuwa mali za Bwana, kama alivyozitakasa nazo fedha na dhahabu, alizozichukua kwa mataifa yote, aliyoyashinda,
12
kama kwao Washami na Wamoabu na wana wa Amoni na Wafilisti na Waamaleki, hata nyara za Hadadezeri, mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.
13
Dawidi aliporudi kwa kuwapiga Washami akajipatia jina kuu kwa kuua watu 18000 Bondeni kwa Chumvi.
14
Kisha Dawidi akaweka askari kwa Waedomu, kwao Waedomu akaweka askari po pote, nao Waedomu wote wakawa watumishi wa Dawidi. Ndivyo, Bwana alivyompa Dawidi kushinda po pote, alipokwenda.
15
Dawidi akawa mfalme wa Waisiraeli wote, naye Dawidi akawatengenezea watu wake wote mashauri yaliyokuwa sawa, maana yaliongoka.
16
Naye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa vikosi, naye Yosafati, mwana wa Ahiludi, alikuwa mwandishi wa mambo yaliyopasa kukumbukwa.
17
Naye Sadoki, mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki, mwana wa Abiatari, walikuwa watambikaji, naye Seraya alikuwa mwandishi.
18
Naye Benaya, mwana wa Yoyada, alikuwa mkuu wao Wakreti na Wapuleti, nao wana wa Dawidi walikuwa watambikaji.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24