bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 20
2 Samuel 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 21 →
1
Ikatukia, ya kama kulikuwa na mtu asiyefaa, jina lake Seba, mwana wa Bikri, mtu wa Benyamini. Akapiga baragumu kwamba: Sisi hatuna fungu kwake Dawidi, wala hatuna lililo letu kwake mwana wa Isai. Ninyi Waisiraeli, kila mtu na aende hemani kwake.
2
Ndipo, watu wote wa Waisiraeli walipopanda kwenda kwao wakiacha kumfuata Dawidi, ila wakamfuata Seba, mwana wa Bikri. Lakini Wayuda wakaandamana na mfalme wao toka mto wa Yordani hata mji wa Yerusalemu.
3
Dawidi alipoingia nyumbani mwake huko Yerusalemu, mfalme akawachukua wale masuria kumi, aliowaweka kuiangalia nyumba, akawatia katika nyumba ya kulindwa, akawatunza humo, lakini hakuingia kwao. Basi, wakawa wafungwa mpaka siku ya kufa kwao, siku zao zikawa kama za wajane.
4
Mfalme akamwambia Amasa: Waite watu wa Yuda, waje kwangu katika siku hizi tatu, kisha nawe uje kusimama hapa!
5
Amasa akaenda kuwaita Wayuda; lakini alipokawia na kuupita muda, aliowekewa,
6
Dawidi akamwambia Abisai: Sasa Seba, mwana wa Bikri, atatupatia mabaya kuliko Abisalomu; wewe wachukue watumishi wa bwana wako, umfukuze, asijipatie miji yenye maboma ya kuponea humo, macho yetu yasimwone tena.
7
Ndipo, watu wa Yoabu walipotoka, wakamfuata nao Wakreti na Wapuleti na mafundi wote wa vita. Wakatoka Yerusalemu kwenda kumfukuza Seba, mwana wa Bikri.
8
Wao walipofika kwenye lile jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akawatokea usoni. Naye Yoabu alikuwa amejifunga nguo zake za vitani, alizozivaa kila mara, juu yao alikuwa amejifunga upanga uliofungwa kiunoni, nao ulikuwa ndani ya ala yake; lakini alipokwenda huko na huko, ukaanguka.
9
Yoabu akamwamkia Amasa kwamba: Hujambo, ndugu yangu? Kisha Yoabu akamshika Amasa udevu kwa mkono wake wa kulia, anoneane naye.
10
Amasa asipouangalia upanga uliomo mkononi mwa Yoabu, akamchoma nao tumboni, matumbo yake yamwagike chini, hakumchoma mara ya pili, akafa tu. Kisha Yoabu na ndugu yake Abisai wakaenda kumfukuza Seba, mwana wa Bikri.
11
Naye mmoja wao vijana wa Yoabu akaja kusimama kwake Amasa na kusema: Apendezwaye na Yoabu, naye aliye upande wa Dawidi na amfuate Yoabu!
12
Lakini Amasa alikuwa anagaagaa katika damu yake katikati ya barabara; yule mtu alipoona, ya kuwa watu wote wanasimama hapo barabarani, akamwondoa Amasa hapo barabarani na kumtupa porini, kisha akamfunika kwa nguo, kwani aliona, ya kuwa kila aliyefika hapo alipo husimama.
13
Alipokwisha kumwondoa hapo barabarani, watu wote wakapapita tu, waende kumfuata Yoabu, wamfukuze Seba, mwana wa Bikri.
14
Huyo akapita kwa mashina yote ya Waisiraeli mpaka Abeli na Beti-Maka nao Haberimu wote; ndipo, watu walipokusanyika, wakaja kufuatana naye.
15
Lakini wale walipokuja wakamsonga na kumzinga kule Abeli kwa Beti-Maka, wakiujengea mji huo boma la mchanga la kuuzunguka, nalo kikasimama papo hapo, mfereji wa boma la mji ulipokuwa. Nao watu wote waliokuwa na Yoabu wakachimba chini ya ukuta wa boma lao, wauangushe.
16
Ndipo, mwanamke mwenye werevu wa kweli alipoita toka mjini kwamba: Sikieni! Sikieni! Mwambieni Yoabu, aje hapa karibu, niseme naye!
17
Yoabu alipofika karibu yake, yule mwanamke akamwuliza: Wewe ndiwe Yoabu? Aliposema: Ndimi, akamwambia: Yasikilize maneno ya kijakazi wako! Akasema: Mimi nitayasikia.
18
Akasema kwamba: Kale watu husema kwamba: Waulizeni watu wa Abeli! Ndivyo, walivyoyamaliza mashauri.
19
Sisi tu Waisiraeli watulivu na welekevu, nawe unataka kuwaua watu wa humu mjini waliozaa makundi kwao Waisiraeli. Ni kwa nini, ukitaka kuwameza walio fungu lake Bwana?
20
Yoabu akajibu kwamba: Hili linikalie mbali kabisa kwamba: Ninataka kumeza na kuangamiza!
21
Hivi haviko kabisa, ila yuko mtoro wa milima ya Efuraimu, jina lake Seba, mwana wa Bikri; huyu ameuinua mkono wake, amwue mfalme Dawidi. Mtoeni huyu peke yake tu! Ndipo, nitakapoondoka penye mji huu. Naye yule mwanamke akamwambia Yoabu: Utakiona kichwa chake, kikitupwa kwako toka ukutani juu.
22
Kisha huyu mwanamke akaja kuonana na watu wote na kuwatolea huo werevu wake wa kweli. Ndipo, walipokikata kichwa chake Seba, mwana wa Bikri, wakakitupia huko kwa Yoabu. Kisha akapiga baragumu, nao watu wakatawanyika wakiondoka kwenye ule mji, wakaenda kila mtu hemani kwake, naye Yoabu akarudi Yerusalemu kwa mfalme.
23
Yoabu alikuwa mkuu wa vikosi vyote vya Waisiraeli, naye Benaya, mwana wa Yoyada, alikuwa mkuu wa Wakreti na wa Wapuleti.
24
Naye Adoramu alikuwa mkuu wa kazi za nguvu, naye Yosafati, mwana wa Ahiludi, alikuwa mwandishi wa mambo yaliyopasa kukumbukwa.
25
Naye Sewa alikuwa mwandishi, nao Sadoki na Abiatari walikuwa watambikaji.
26
Naye Ira wa Yairi alikuwa mtambikaji wa Dawidi.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24