bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Samuel 6
2 Samuel 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 7 →
1
Dawidi akawakusanya tena wapiga vita wote waliochaguliwa kwao Waisiraeli, watu 30000.
2
Kisha Dawidi akaondoka, akaenda nao hao watu wote waliokuwa naye kwenda Bale wa Yuda kulichukua huko Sanduku la Mungu lililoitwa jina lake kwa Jina la Bwana Mwenye vikosi akaaye juu ya Makerubi.
3
Wakalipandisha Sanduku la Mungu katika gari jipya wakilitoa katika nyumba ya Abinadabu iliyokuwa kilimani juu; nao Uza na Ayo, wana wa Abinadabu, wakaliendesha hilo gari jipya.
4
Walipokwisha kulitoa katika nyumba ya Abinadabu iliyokuwa kilimani juu, wakalipeleka Sanduku la Mungu, Ayo akilitangulia Sanduku.
5
Dawidi mwenyewe nao watu walio wa mlango wa Isiraeli wakalitangulia na kucheza mbele ya Bwana na kupiga vyombo vyote vya kuchezea vilivyotengenezwa kwa mivinje kama mazeze na mapango na patu na njuga na matoazi.
6
Walipofika pake Nakoni pa kupuria, Uza akalipelekea Sanduku la Mungu mkono, alishike, kwa kuwa ng'ombe walijikwaa.
7
Ndipo, makali ya Bwana yalipomwakia Uza, naye Mungu akampiga huko kwa ajili ya hilo kosa, akafa papo hapo penye Sanduku la Mungu.
8
Hapo Dawidi akaingiwa na uchungu, ya kuwa Bwana amempiga Uza pigo kama hilo, wakapaita mahali pale Peresi-Uza (Pigo la Uza) mpaka siku hii ya leo.
9
Siku hiyo Dawidi akashikwa na woga wa kumwogopa Bwana kwamba: Sanduku la Bwana litawezaje kufika kwangu?
10
Kwa hiyo Dawidi hakutaka kuliingiza Sanduku la Bwana kwake mjini kwa Dawidi, Dawidi akashika njia nyingine, akaliweka nyumbani mwa Obedi-Edomu wa Gati.
11
Humo nyumbani mwa Obedi-Edomu wa Gati Sanduku la Bwana likakaa miezi mitatu, naye Bwana akambariki Obedi-Edomu na mlango wake wote.
12
Mfalme Dawidi alipopashwa habari kwamba: Bwana ameubariki mlango wa Obedi-Edomu nayo yote yaliyo yake kwa ajili ya Sanduku la Mungu, Dawidi akaenda, akalitoa Sanduku la Mungu nyumbani mwa Obedi-Edomu, akalipandisha mjini kwa Dawidi kwa furaha.
13
Ikawa, wao wachukuzi wa Sanduku la Bwana walipokwisha kwenda hatua sita, akachinja ng'ombe ya tambiko na ndama aliyenona.
14
Dawidi akawa akicheza kwa nguvu zote mbele ya Bwana, naye Dawidi alikuwa amevaa kisibau cheupe cha ukonge.
15
Ndivyo, Dawidi na mlango wote wa Waisiraeli walivyolipandisha Sanduku la Bwana kwa kushangilia na kupiga mabaragumu.
16
Ikawa, Sanduku la Bwana lilipoingia mjini kwa Dawidi, Mikali, binti Sauli, alichungulia dirishani; naye alipomwona mfalme Dawidi, alivyorukaruka na kuchezacheza mbele ya Bwana, ndipo, alipombeza moyoni mwake.
17
Walipokwisha kuliingiza Sanduku la Bwana wakaliweka mahali pake katikati ya lile hema, Dawidi alilolipigia. Kisha Dawidi akamtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za kumshukuru.
18
Dawidi alipokwisha kuzitoa hizo ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za shukrani akawabariki watu katika Jina la Bwana Mwenye vikosi.
19
Kisha akawagawia watu wote wa huo mkutano wote wa Waisiraeli, waume kwa wake, kila mtu kipande kimoja cha mkate na kipande kimoja cha nyama na andazi moja la zabibu, kisha watu wote wakaenda zao kila mtu nyumbani kwake.
20
Dawidi naye aliporudi kuwabariki walio wa mlango wake, Mikali, binti Sauli, akamwendea Dawidi njiani, akasema: Kweli leo mfalme wa Waisiraeli amejitukuza alipojivua nguo machoni pa vijakazi wa watumishi wake, kama mmoja wao walio wa ovyoovyo tu anavyojivika uchi.
21
Lakini Dawidi akamwambia Mikali: Bwana ndiye aliyenichagua na kumwacha baba yako na mlango wake wote, aliponiagiza mimi kuwa mkuu wao walio ukoo wake Bwana nao wao Waisiraeli, naye yeye Bwana ndiye, ambaye ninataka kucheza mbele yake.
22
Tena ninataka kujipunguza kupapita hapo pa leo, niwe mnyenyekevu machoni pangu mwenyewe; ndivyo, nitakavyojipatia utukufu kwao vijakazi, uliowasema.
23
Lakini Mikali, binti Sauli, hakuwa na mwana mpaka siku hiyo, alipokufa.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24