bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 1
Hosea 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 2 →
1
Hili ni neno la Bwana lililomjia Hosea, mwana wa Beri, Uzia na Yotamu na Ahazi na Hizikia walipokuwa wafalme wa Wayuda, naye Yoroboamu, mwana wa Yoasi, alipokuwa mfalme wa Waisiraeli.
2
Hapo, Bwana alipoanza kusema na Hosea, Bwana akamwambia Hosea: Nenda, ujichukulie mwamamke mgoni, ujipatie nao watoto wa ugoni! Kwani nchi hii inafuata ugoni kwa kumwacha Bwana.
3
Akaenda, akamchukua Gomeri, binti Dibulemu; naye akapata mimba, akamzalia mwana wa kiume.
4
Bwana akamwambia: Mwite jina lake Izireeli! Kwani kiko bado kitambo kidogo, ndipo, nitakapoulipisha mlango wa Yehu damu za Izireeli na kuukomesha ufalme wa Isiraeli.
5
Siku ile ndipo, nitakapouvunja upindi wa Isiraeli katika bonde la Izireeli.
6
Kisha akapata mimba tena, akazaa mwana wa kike. Bwana akamwambia: Mwite jina lake Hahurumiwi! Kwani sitawahurumia tena walio mlango wa Isiraeli nikiendelea kuwaondolea mabaya yao.
7
Lakini walio mlango wa Yuda nitawahurumia na kuwaokoa kwa nguvu za Bwana Mungu wao, nisiwaokoe kwa nguvu za pindi wala za panga wala za mapigano wala za farasi, wala kwa nguvu za wapanda farasi.
8
Alipokuwa amemzoeza Hahurumiwi, asinyonye maziwa, akapata mimba tena, akazaa mwana wa kiume.
9
Bwana akamwambia: Mwite jina lake Si ukoo wangu! Kwani ninyi ham ukoo wangu, nami sitakuwa tena wenu.
10
Lakini tena hesabu ya wana wa Isiraeli itakuwa kama mchanga wa ufukoni usiopimika wala usiohesabika; itakuwa hapo, hao wanaoambiwa sasa: Ninyi ham ukoo wangu waambiwe: M wanawe Mungu aliye Mwenye uzima.
11
Ndipo, wana wa Yuda na wana wa Isiraeli watakapokusanyika pamoja, wajiwekee kichwa kimoja, wakitoka kwao, waje hapo, kwani siku ile ya Izireeli itakuwa kuu.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14