bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 11
Hosea 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 12 →
1
Isiraeli alipokuwa kijana, nilimpenda; huko Misri ndiko, nilikomwitia mwanangu.
2
Lakini walipowaita halafu, ndipo, walipokwenda zao na kutoka kwao hao, wakayatambikia Mabaali na kuvukizia vinyago.
3
Nami mwenyewe nalimfundisha Efuraimu kwenda kwa miguu kama mtoto, nikawashika mikono, lakini hawakutambua, ya kuwa ninawaponya.
4
Naliwavuta kwa kamba zimfaazo mtu na kwa vigwe vya upendo, nikawa nikiwatua mizigo mabegani pao, nikawainamia, nipate kuwalisha chakula.
5
Hawatarudi katika nchi ya Misri, ila Mwasuri ndiye atakayekuwa mfalme wao, kwani wamekataa kurudi kwangu.
6
Nazo panga zitazunguka mijini mwao, ziyamalize makomeo yao kwa kuyala kwa ajili ya mashauri yao.
7
Walio ukoo wangu hujipingia kuniacha; wakiitwa kurudi kwake Alioko huko juu, kwao wote hakuna atakayemtukuza.
8
Nitawezaje kukutoa Efuraimu au kukuacha, Isiraeli? Nitawezaje kukutoa, uwe kama Adima (Sodomu), au kukugeuza, uwe kama Seboimu (Gomora)? Moyo wangu ungefudikizwa kifuani mwangu, ungechafuka sana kwa kukuonea uchungu.
9
Sitayafanya, ukali wangu wenye moto uyatakayo, sitamwangamiza tena Efuraimu, kwani mimi ni Mungu, si mtu; namo katikati yenu mimi ni mtakatifu, nisije kuingia kwenu kwa machafuko.
10
Watakuja kumtafuta Bwana, atakaponguruma kama simba; kweli atakaponguruma, ndipo, watakapokuja kwa kutetemeka wao watoto watokao upande wa baharini.
11
Watamkimbilia kama ndege kwa kutetemeka wakitoka Misri, au kama hua wakiitoka nchi ya Asuri; ndipo, nitakapowakalisha nyumbani mwao; ndivyo, asemavyo Bwana.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14