bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 10
Hosea 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 11 →
1
Isiraeli ni mzabibu uchipukao vema, uzaao matunda mema; lakini kama matunda yake yalivyo mengi ndivyo, walivyojitengenezea pengi pa kutambikia, kwa wema wa nchi yako waliulinganya wema wa vinyago.
2
Mioyo yao ni midanganyifu, sasa watalipishwa! Yeye atapavunja pao pa kutambikia, aviangamize vinyago vyao.
3
Kwani sasa husema kweli kwamba: Hatuna mfalme! Bwana hatukumcha, naye mfalme atatufanyizia nini?
4
Husema maneno tu, huapa bure wakifanya maagano; basi, nayo mapatilizo yatakua kama mimea yenye uchungu shambani kwenye matuta.
5
Wakaao Samaria huihangaikia ng'ombe ya Beti-Aweni, kweli watu wa huko wanaiombolezea, nao watambikaji wake wanatetemeka kwa ajili yake, kwa ajili ya utukufu wake, kwa kuwa umeondolewa kwao.
6
Nayo yenyewe itapelekwa Asuri kuwa tunzo la mfalme Yarebu; ndipo, soni zitakapomshika Efuraimu, naye Isiraeli atatwezwa kwa ajili ya shauri lake.
7
Mfalme wa Samaria ataangamizwa, awe kama kibanzi majini juu.
8
Navyo vilima vya Aweni vitaangamizwa, Isiraeli alikomkosea Mungu; miti yenye miiba na mibigili itakulia hapo pao pa kutambikia; ndipo, watakapoiambia milima: Tufunikeni! nayo machuguu: Tuangukieni!
9
Kuanzia zile siku za Gibea umekosa wewe Isiraeli! Huko walisimama, vita vya kuwapiga wapotovu visiwafikie huko Gibea.
10
Nitawapiga, kama itakavyonipendeza; makabila mengine yatawakusanyikia, watakapofungiwa manza zao mbili, walizozikora.
11
Efuraimu anafanana na ndama aliyefundishwa, apendaye kupura; nami nitautumia uzuri wa shingo yake na kumfundisha kuvuta gari; hata Yuda atalima mahali pa ng'ombe, naye Yakobo atajipondea mwenyewe madongo.
12
Kwa hiyo jipandieni yatakayoleta wongofu, mpate kuvuna yenye utu! jilimieni shamba jipya, siku zingaliko bado za kumtafuta Bwana, mpaka aje na kuwafundisha yanyokayo!
13
Lakini ninyi hulimia mabaya, mkavuna mapotovu, mkala mazao ya uwongo. Kwa kuwa unajishikiza kwa njia yako na kwa wingi wa watu walio na nguvu za kupiga vita,
14
kwa hiyo makelele ya vita yatatokea kwa watu wako, nayo miji yako yote yenye maboma itaangamizwa, kama Salmani alivyouangamiza Beti-Arbeli siku, walipopigana, ni hapo wamama waliposetwa na kuuawa pamoja na watoto.
15
Mambo kama hayo ndiyo, Beteli utakayowapatia ninyi, kwa ajili ya ubaya wenu ulio mwingi; siku moja kutakapopambazuka, mfalme wa Isiraeli atakuwa ameangamia kabisa.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14