bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 4
Hosea 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 5 →
1
lisikieni neno la Bwana, ninyi wana wa Isiraeli! Kwani Bwana yuko na neno la kuwagombeza wakaao katika nchi hii, kwa kuwa hakuna welekevu wala huruma, wala ujuzi wa Mungu katika nchi hii.
2
Huapiza, huongopa, huua, huiba, huvunja unyumba, hukorofisha; ndivyo, damu zinavyoshikamana na damu nyingine.
3
Kwa hiyo nchi hii inasikitika, wakafifia wote wakaao humo, nyama wa porini na ndege wa angani, nao samaki wa baharini wanatoweka.
4
Lakini hawataki, mtu awagombeze, wala mtu awaonye, walio ukoo wako hufanana nao, wanaowagombeza watambikaji.
5
Kwa hiyo utajikwaa mchana, naye mfumbuaji atajikwaa pamoja na wewe usiku, nami nitamwangamiza mama yako.
6
Walio ukoo wangu wanaangamia kwa kukosa ujuzi, kwa kuwa wewe umeukataa ujuzi, nami nakukataa, usinitambikie tena; kwa kuwa umeyasahau Maonyo ya Mungu wako, nami nitawasahau wanao.
7
Hivyo, walivyoendelea kuwa wengi, ndivyo, walivyoendelea kunikosea, kwa sababu hii nitaugeuza utukufu wao kuwa mambo yatiayo soni.
8
Hujilisha makosa yao walio ukoo wangu, namo rohoni mwao hutamani kukora manza kama wao.
9
Kwa hiyo watu na watambikaji watapatwa na mambo yaleyale, nitawapatilizia njia zao, nayo matendo yao nitawarudishia.
10
Watakapokula, hawatashiba; watakapofanya ugoni hawatapata wana, kwa kuwa wameacha kushikana na Bwana.
11
Ugoni na mvinyo na pombe huichukua mioyo yao.
12
Walio ukoo wangu huzipiga mbao zao, nazo fimbofimbo zao huziagulia, kwani roho ya ugoni imewapoteza, wakafanya ugoni papo hapo walipomwacha Mungu wao.
13
Hutambika milimani juu, kwenye vilima huvukiza kuliko na mvule au mgude au mkwaju, kwani kivuli chake ni chema. Kwa hiyo wana wenu wa kike huzini, nao wachumba wenu huvunja unyumba.
14
Sitawapatiliza wana wenu wa kike, ya kuwa huzini, wala wachumba wenu, ya kuwa huvunja unyumba; kwani wenyewe hujitenga, wawe nao wanawake wagoni, hutambika pamoja na wanawali watakatifu wa kimizimu; ndivyo, watu wasiotambua maana wanavyoponzwa.
15
Wewe Isiraeli, ukiwa unafanya ugoni, usimkoseshe Yuda! Msije Gilgali! Wala msipande kwenda Beti-Aweni! Wala msiape na kusema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima!
16
Ikiwa Isiraeli ameshupaa vibaya kama ndama wenye ushupavu, je? Bwana atamchunga kama kondoo penye lisho pana?
17
Efuraimu ni mpenda vinyago, mwache tu!
18
Wakiisha kulewa hufuata ugoni, nao watu wake walio washika ngao hupenda sana mambo yenye soni.
19
Upepo utawakamata kwa ajili ya matambiko yao.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14