bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 7
Hosea 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 8 →
1
Ninapotaka kumponya Isiraeli, ndipo, panapotokea wazi manza za Efuraimu na mabaya ya Samaria, kwani hutenda ya uwongo, nao wezi hujipenyeza nyumbani, nako nje huenea wanyang'anyi.
2
Hawasemi mioyoni mwao, ya kama nayakumbuka mabaya yao yote; sasa matendo yao yanawazunguka, yako wazi usoni pangu.
3
Kwa mabaya yao huwafurahisha wafalme wao, nao wakuu wao kwa kuongopa kwao.
4
Wao wote ni wazinzi, hufanana na jiko lililowashwa moto na mchoma mikate, naye akiisha kukanda unga, hupumzika kwa kuchochea moto, hata unga uwe umechachuka.
5
Wakisema: Leo ni sikukuu ya mfalme wetu, ndipo, wakuu wanapojiwasha kwa ukali wa mvinyo; naye mwenyewe hushikana mikono na wafyozaji.
6
Kwa hivyo, wanavyomvizia, humkaribishia mioyo yao, ikiwa yenye moto ulio kama wa jiko la mikate: mchocheaji akiwa amelala usiku kucha, asubuhi huwaka kama moto wenye miali.
7
Hivyo wao wote hupata moto ulio kama wa jiko la mikate, wakawala waamuzi wao, wafalme wao wote wakaangushwa nao, lakini kwao hao hakuonekana aliyenililia mimi.
8
Efuraimu hujichanganya na mataifa mengine, Efuraimu huwa kama andazi lisilogeuzwa.
9
Wageni wamezila nguvu zake, mwenyewe asipovijua; mvi zimemtoka mojamoja, lakini mwenyewe havijui.
10
Majivuno yao Waisiraeli yanawasuta machoni pao, lakini hawarudi kwake Bwana Mungu wao, wala hawamtafuti katika mambo hayo yote.
11
Efuraimu huwa kama hua pumbavu, asiye na akili: mara anamwita Mmisri, mara anakwenda Asuri.
12
Kila mara walipokwenda, niliwatandia wavu wangu, niwanase kama ndege wa angani, kisha nikawapatiliza, kama mkutano wao ulivyoambiwa.
13
Yatawapata, kwa kuwa wamenikimbia! Maangamizo yatawapata, kwa kuwa wamenikosea! Nami nilipotaka kuwakomboa, wao waliniambia ya uwongo tu,
14
hawakunilalamikia kwa mioyo yao, walipolia vitandani kwao. Ni ngano na pombe tu, wanazozikusanyikia, lakini kwangu mimi wameondoka.
15
Tena ni mimi niliyewafunza kuitumia mikono, nikaitia nguvu, lakini huniwazia mabaya tu.
16
Wanaporudi, hawaji kwangu nilioko huku juu, hufanana na upindi uliolegea. Wakuu wao wataangushwa na panga kwa ajili ya ukali wa ndimi zao; kwa hiyo watafyozwa katika nchi ya Misri.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14