bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 8
Hosea 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 9 →
1
Weka baragumu midomoni pako kwamba: Yuko atakayeijia Nyumba ya Bwana kama tai! Wamelivunja Agano langu, wakayakosea Maonyo yangu.
2
Watanililia kwamba: Mungu wetu, sisi Waisiraeli tunakujua!
3
Lakini Isiraeli ameyatupa yaliyo mema, kwa hiyo adui atamkimbiza.
4
Wameweka wafalme, nisiowaagiza mimi, wakaweka wakuu, nisiowajua! Kwa fedha zao na kwa dhahabu zao wakajitengenezea vinyago, kusudi viangamizwe tu.
5
Ndama yako, Samaria, nimeitupa, makali yangu yakapata kuwaka kwa ajili yao. Mpaka lini wataweza kuendelea hivyo pasipo kutakaswa?
6
Ilitokea kwao Waisiraeli, ni fundi aliyeitengeneza, siyo Mungu, kwani itakuwa vumbi hiyo ndama ya Samaria.
7
Kwa kuwa hupanda upepo, watavuna kimbunga, mbegu zao hazioti majani, hazileti unga; kama zingeuleta, wageni wangeula.
8
Waisiraeli wamekwisha kumezwa: wako kwa wamizimu, wanafanana na chombo kisichopendeza.
9
Kwani ndio walioondoka kwenda Asuri, wakawa kama punda wa porini anayejitembelea peke yake. Efuraimu akajinunulia huko wagoni wampendao;
10
lakini ijapo wawanunue kwa wamizimu, nitawapata na kuwakusanya, nao bado kidogo watagaagaa kwa kuumizwa na mizigo, ambayo mfalme na wakuu waliwapagaza.
11
Kwani Efuraimu amejipatia pengi pa kutambikia kwa ajili ya kukosa kwao, napo hapo pa kutambikia pakawa pao pa kukosea.
12
Ijapo nimwandikie mara elfu Maonyo yangu, huwaziwa kwake kuwa mambo mageni tu.
13
Wakitoa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima hula nyama, Bwana hapendezwi nao; sasa atazikumbuka manza zao, awapatilizie makosa yao, nao watarudi Misri.
14
Isiraeli alipomsahau Muumbaji wake, alijenga majumba makuu; Yuda naye akajenga miji mingi yenye maboma. Nami nitatia moto mijini mwake, uyale yale majumba yake matukufu.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14