bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 9
Hosea 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 10 →
1
Usifurahi, Isiraeli ukishangilia kama makabila mengine! Kwani umefanya ugoni, ulipomwacha Mungu wako, ukaupenda mshahara wa ugoni po pote, ngano zilipopurwa.
2
Lakini wala purio la ngano wala kamulio la zabibu hayatawachunga, nazo pombe zitawadanganya tu.
3
Hawatakaa katika nchi ya Bwana, Efuraimu atarudi Misri, nako Asuri watakula yenye uchafu.
4
Hawatamtolea Bwana mvinyo za tambiko, wala vipaji vyao vingine vya tambiko havitamfurahisha, kwao wenyewe vitakuwa kama vilaji vya matanga, wote watakaovila watajipatia uchafu, kwani ni vilaji vyao vya kukomesha njaa tu, haviingii Nyumbani mwa Bwana.
5
Mtafanya nini, itakapokuwa siku ya mkutano au sikukuu ya Bwana?
6
Kwani mtaona: waliokwenda zao kwa kukimbia maangamizo Misri itawakusanya, namo Mofu (Memfisi) watawazika, mapambo yao mazuri ya fedha yatatwaliwa na viwawi, mangugi nayo yatakuwa mahemani mwao.
7
Siku za mapatilizo zitafika! Siku za malipizi zitafika! Ndipo, Waisiraeli watakapojua, kama mfumbuaji ni mpumbavu, kama mtu wa kiroho ni mwenye wazimu, kwani manza, ulizozikora, ni nyingi, nao upingani wako ni mwingi.
8
Efuraimu ananivizia, Mungu wangu alipo, tanzi la mtega ndege mfumbuaji huliona katika njia zake zote, ndio upingani uliomo nyumbani mwa mungu wake.
9
Wamejitosa katika matendo mabaya kama siku zile za Gibea; atazikumbuka manza zao, atayapatiliza makosa yao.
10
nilipomvumbua Isiraeli, alikuwa kama zabibu nyikani; kama lilivyo tunda la limbuko la mkuyu unaoanza kuzaa, ndivyo, baba zenu walivyokuwa nilipowaona; lakini walipomfikia Baali-Peori, wakajitenga kwangu, watumikie mambo yenye soni, wakawa matapisho kama hayo mambo, waliyoyapenda.
11
Utukufu wao wa Efuraimu utatoweka kwa kuruka kama ndege, kwa kuwa hapatakuwako atakayezaa wala mwenye mimba wala atakayepata mimba.
12
Ijapo wawakuze wana wao, na niwanyang'anye hao wana wao, asisalie hata mtu mmoja atakayekuwapo. Nao wenyewe wataona mambo, nitakapoondoka kwao.
13
Nilipomwona Efuraimu, alikuwa amepandwa pazuri paelekeapo Tiro, lakini Efuraimu naye hana budi kumtolea muuaji watoto wake.
14
Nikisema: Bwana, wape! utawapa nini? Wape matumbo yasiyozaa na maziwa yaliyokauka!
15
Ubaya wao wote ulitimia Gilgali; ndiko, nilikochukizwa nao; kwa huo ubaya wa matendo yao nitawafukuza Nyumbani mwangu, sitaendelea kuwapenda, wakuu wao wote hukataa kutii.
16
Efuraimu alipopigwa, mizizi yao ikanyauka, hawatazaa tena; ijapo wazae, nitawaua nao wapendwa wao, matumbo yao yaliowazaa.
17
Mungu wangu atawatupa, kwani hawakumsikia; ndipo, watakapokuwa wakitangatanga kwa mataifa.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14