bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 2
Hosea 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 3 →
1
Hapo waiteni ndugu zenu Ukoo wangu na maumbu zenu Huhurumiwa!
2
Mgombezeni mama yenu! Haya! Mgombezeni! Kwani yeye siye mke wangu, nami si mumewe. Na auondoe ugoni wake, usiwe mbele yake, nao uzinzi wake, usiwe penye maziwa yake,
3
nisije kumvua, akawa mwenye uchi, na kumweka, awe, kama alivyokuwa siku ile, alipozaliwa, nikamgeuza kuwa kama nyika, nikamfanya kuwa kama nchi kavu nikimwua kwa kiu.
4
Nao wanawe sitawahurumia, kwani ndio wana wa ugoni;
5
kwa kuwa mama yao amefanya ugoni, akatenda yenye soni yeye aliyewachukua mimba, maana alisema: Nitawafuata wapenzi wangu wanipao chakula changu na maji yangu, nayo manyoya yangu ya kondoo na pamba zangu, nayo mafuta yangu na vinywaji vyangu.
6
Kwa hiyo utaniona, nikiiziba njia yako kwa miiba, nitajenga hata ukuta, asione pake pa kupitia.
7
Atakapowakimbilia wapenzi wake, asiwafikie, atakapowatafuta, asiwaone; ndipo, atakaposema: Na nije kumrudia mume wangu wa kwanza, kwani hapo naliona mema kuliko sasa.
8
Naye hajui, ya kuwa ni mimi niliyempa zile ngano na zile pombe na yale mafuta, ya kuwa ni mimi niliyemzidishia fedha na dhahabu, walizomtolea Baali.
9
Kwa hiyo na nirudi kuzichukua ngano zangu, siku zitakapotimia, nazo pombe zangu, pangu patakapotimia, nitampokonya nguo zangu za manyoya ya kondoo na za pamba, alizo nazo za kuufunika uchi wake.
10
Sasa nitayafunua yake yenye soni machoni pa wapenzi wake, tena hakuna mtu atakayemponya mkononi mwangu.
11
Nitazikomesha furaha zake zote na sikukuu zake za miandamo ya mwezi nazo za mapumziko na mikutano yake yote.
12
Nitaiharibu mizabibu yake na mikuyu yake, aliyoisema: Hii ndiyo kipaji, wapenzi wangu walichonipa; nitaigeuza kuwa misitu, nyama wa porini waile.
13
Nitampatilizia siku za kuvitambikia vinyago vya Baali, alivyovivukizia uvumba alipojipamba na kuvaa pete zake na ushanga wake akiwafuata wapenzi wake kwa kunisahau mimi; ndivyo, asemavyo Bwana.
14
Kwa hiyo mtaniona, nikimbembeleza na kumpeleka nyikani, niseme naye kimoyomoyo.
15
Ndiko, nitakakompa mizabibu yake, akitoka huko, nalo Bonde la Akori nitaligeuza kuwa mlango wa kingojeo; ndipo, atakapoitika kama hapo, alipokuwa kijana, alipotoka katika nchi ya Misri kuja huku.
16
Ndivyo asemavyo Bwana: Siku hiyo ndipo, utakaponiita Mume wangu, usiniite tena Bwana wangu.
17
Ndipo, nitakapoyaondoa majina ya vinyago vya Baali kinywani mwako, visitajwe tena kwa majina yao.
18
Siku hiyo nitawafanyia agano nao nyama wa porini n ndege wa angani na wadudu wa nchini, nitayavunja mata na panga na magombano, yatoke katika nchi hiyo, niwakalishe salama.
19
Nitakuposa, uwe wangu kale na kale, nitakuposa, uwe wangu kwa mashauri yaongokayo na kwa huruma zenye upole.
20
Nitakuposa, uwe wangu kwa kweli; ndipo, utakapomjua Bwana.
21
Siku hiyo ndipo, nitakapoitikia; ndivyo, asemavyo Bwana; nitaziitikia mbingu nazo zitaiitikia nchi hii.
22
Nayo nchi hii itaziitikia ngano, nazo pombe na mafuta, nayo hayo yatamwitikia Izireeli (Mungu mpanzi).
23
Nami nitampanda katika nchi hii, awe wangu, nimhurumie Hahurumiwi, tena nitamwambia Si ukoo wangu: Ndiwe Ukoo wangu, naye atasema: Ndiwe Mungu wangu.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14