bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 14
Hosea 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
1
Samaria atalipishwa manza, alizozikora kwa kumpingia Mungu wake: kwa hiyo wataangushwa kwa panga, watoto wao wachanga watapondwa, nao wanawake wenye mimba watatumbuliwa.
2
Rudi, Isiraeli, kwa Bwana Mungu wako! Kwani umejikwaa kwa maovu, uliyoyafanya.
3
Yashikeni maneno haya kwenda nayo, mkirudi kwake Bwana, ya kumwambia: Ziondoe manza zote pia, tulizozikora, ututolee wema! Ndipo, tutakapotoa shukrani za midomo yetu, ziwe ng'ombe za tambiko.
4
Mwasuri hawezi kutuokoa, nasi hatujui kupanda farasi; hatutaziita tena kazi za mikono yetu kwamba: Ni mungu wetu! Kwani kwako ndiko, wafiwao na wazazi wanakojipatia huruma.
5
Watakaporudi hivyo, nitawaponya, nitawapenda kwa moyo, kwani ndipo, makali yangu yatakapokuwa yamewaondokea.
6
Ndipo, nitakapokuwa kwake Isiraeli kama umande, apate kuchanua kama maua ya shambani, ashushe mizizi yake kama miti ya Libanoni.
7
Matawi yake yatakuwa marefu, uzuri wake uwe kama wa mchekele, nao utanuka vizuri kama mti wa Libanoni.
8
Watakaokaa kivulini kwake watarudia kupanda ngano, watachanua kama mizabibu, sifa yao itakuwa kama sifa ya mvinyo za Libanoni.
9
Ndipo, Efuraimu atakaposema: Vinyago vinanifaliaje tena? Nami nitamjibu na kumtazama kwa kupendezwa: Mimi ni kama mvinje mbichi, kwangu mimi kutaonekana yaliyo mazao yako.
10
Yuko nani aliye mwerevu wa kweli, ayatambue hayo? Yuko nani aliye mtambuzi, ayajue maana yao hayo? Kwani njia za Bwana hunyoka, nao waongofu huzishika, lakini wapotovu hukwazwa nazo.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14