bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 12
Hosea 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 13 →
1
Efuraimu amenizingia uwongo, walio mlango wa Isiraeli wamenizingia udanganyifu; Yuda naye hata sasa hujiendea na kumwacha Mungu aliye mtakatifu na mwelekevu.
2
Efuraimu hujilisha upepo, huukimbilia upepo utokao maawioni kwa jua, siku kwa siku huongeza uwongo na uangamizo: hufanya maagano na Asuri, tena mafuta hupelekwa Misri.
3
Lakini Bwana yuko na shauri na Yuda, ampatilizie Yakobo njia zake na kumlipisha matendo yake.
4
Tumboni mwa mama alimshika kaka yake kisigino, napo, alipokuwa mtu mzima, alishindana na Mungu.
5
Akashindana na malaika, akamshinda kwa kulia na kumlalamikia; Beteli ndiko, alikomwona, ndiko, alikosema na sisi
6
yeye Bwana Mungu Mwenye vikosi; Bwana ni Jina lake la kumtukuza.
7
Nawe sharti urudi kwa Mungu wako, ushikamane na upole, ufanye yapasayo, umngojee Mungu wako pasipo kukoma.
8
Kwa kushika mizani ya kudanganyia mikononi mwake Mkanaani hupenda kukorofisha.
9
Efuraimu husema: Kumbe ni tajiri! Nimejipatia mali! Tena kwa hivyo vyote, nilivyovisumbukia, hawataniona, ya kuwa nimefanya kiovu cha kumkosea mtu.
10
Lakini mimi Bwana ni Mungu wako tangu hapo, nilipokutoa katika nchi ya Misri, mimi nitakukalisha tena katika mahema kama penye sikukuu za mkutano.
11
Mimi nilisema na wafumbuaji, nikawatokea mara nyingi, nikawaonya kwa vinywa vya wafumbuaji na kusema mifano.
12
Kwa kuwa huko Gileadi walifanya yasiyofaa, basi, nao watageuzwa kuwa si kitu; kwa kuwa huko Gilgali walitoa ng'ombe za tambiko, napo pao pa kutambikia patakuwa kama chungu za mawe penye matuta.
13
Yakobo alikimbilia mashamba ya Aramu, Isiraeli akatumikia kupata mwanamke, hakuwa na budi kuchunga kondoo na mbuzi, ampate mkewe.
14
Lakini kwa mkono wa mfumbuaji Bwana alimtoa Isiraeli huko Misri, kisha wakachungwa na mfumbuaji.
15
Efuraimu amemsikitisha masikitiko yenye uchungu; kwa hiyo zile damu, alizozimwaga, atamtupia, zimkalie, nayo matusi yake ndiyo, Bwana wake atakayomlipisha.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14