bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 5
Hosea 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 6 →
1
Yasikieni haya, ninyi watambikaji! Yasikilizeni, nanyi mlio mlango wa Isiraeli! Nanyi wa mlango wa mfalme, yategeni masikio! Kwani liko shauri linalowataka, kwa maana mmekuwa tanzi la kuwanasa Wamisipa na wavu uliotegwa Tabori juu.
2
Wakachimba mwina mrefu Setimu, lakini mimi nitawachapa wote.
3
Mimi ninamjua Efuraimu, naye Isiraeli hafichiki, nisimwone, kwani hata sasa, wewe Efuraimu, unaufuata ugoni, naye Isiraeli amejipatia uchafu.
4
Matendo yao yanawazuia kurudi kwa Mungu wao, kwani roho ya ugoni imo mioyoni mwao, lakini Bwana hawamjui.
5
Majivuno ya Isiraeli huwaumbua usoni pake; Isiraeli na Efuraimu watajikwaa kwa ajili ya manza, walizozikora, naye Yuda atajikwaa pamoja nao.
6
Huchukua kondoo na ng'ombe kwenda kumtafuta Bwana, lakini hawamwoni, amekwisha kutengana nao.
7
Bwana wamemwacha kwa udanganyifu, wakazaa wana wasio wake. Sasa mwezi utakaoandama utawala pamoja na fungu lao.
8
Pigeni mabaragumu huko Gibea! Pigeni matarumbeta huko Rama! Pigeni yowe Beti-Aweni: Ni nyuma yako, Benyamini!
9
Siku, Efuraimu atakapochapwa, atageuzwa kuwa mapori yaliyo peke yao; niliyoyajulisha mashina ya Isiraeli yatatimia kweli.
10
Wakuu wa Yuda wanafanana nao wanaosogeza mawe ya mipakani; wao hao nitawamwagia machafuko yangu kama maji.
11
Efuraimu anakorofishwa, amepondwa na hukumu, kwani alikuwa amependezwa kufuata maagizo ya watu.
12
Mimi kwake Efuraimu ni kama mende, nako kwao walio mlango wa Yuda kama ugonjwa wa ubovu.
13
Efuraimu alipouona ugonjwa wake, Yuda naye alipouona usaha wa madonda yake, ndipo, Efuraimu alipokwenda Asuri, naye akatuma kwa mfalme Yarevu (Mgombeaji), lakini hataweza kuwaponya, wala hataukausha usaha wenu.
14
Kwani mimi kwake Efuraimu ni kama simba, nako kwao walio mlango wa Yuda kama mwana wa simba, mimi, kweli mimi mwenyewe nitanyafua, kisha nitakwenda zangu; nitakapochukua, hapatakuwapo atakayeopoa.
15
Nitakwenda kurudi mahali pangu, mpaka watakapojutia, wautafute uso wangu; kwa kusongeka kwao watanichungulia usiku kucha.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14