bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hosea 13
Hosea 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 14 →
1
Efuraimu aliposema, watu walitetemeka; kwani alikuwa mkuu kwao Waisiraeli. kisha akakora manza kwa kumtumikia Baali, basi akafa.
2
Na sasa wanaendelea kukosa wakijifanyizia vinyago kwa fedha zao, vingine wanavichonga, kama wanavyojua; vyote pia ni kazi za mafundi. Kwa ajili yao wenyewe husema: Watoao watu kuwa ng'ombe zao za tambiko sharti wanonee ndama!
3
Kwa sababu hiyo watakuwa kama wingu la asubuhi na kama umande ukaukao upesi, au kama makapi yanayopeperushwa penye kupuria au kama moshi utokao katika bomba.
4
Lakini mimi Bwana ni Mungu wako tangu hapo, nilipokutoa katika nchi ya Misri; nawe usijue mungu mwingine ila mimi, hakuna mwokozi, nisipokuwa mimi.
5
Mimi nilikujua ulipokuwa nyikani katika nchi kavu yenye kiu.
6
Lakini walipoona malisho mema wakashiba; napo waliposhiba, mioyo yao ikajikuza, kwa hiyo wamenisahau.
7
Ndipo, nilipowageukia kuwa kama simba, nikawavizia kama chui njiani,
8
niwarukie kama nyegere aliyenyang'anywa watoto, niwapasue vifua vifunikavyo mioyo yao, niwale hapo hapo kama simba jike, kisha nyama wa porini wawanyafuenyafue,
9
Haya ndiyo yanayokuangamiza, Isiraeli, ya kuwa unanikataa mimi niliye msaada wako
10
Mfalme wako yuko wapi, akuokoe katika miji yako yote? Wako wapi waamuzi wako, uliowaambia: Nipeni mfalme na wakuu!
11
Mimi nilikupa mfalme kwa kukasirika kwangu, tena nikamwondoa kwa makali yangu yenye moto.
12
Manza zake Efuraimu zimefungwa pamoja, makosa yake yakawekwa fichoni.
13
Uchungu wa mzazi utamjia, lakini yeye ni mwana asiyejua kitu; saa yake itakapofika, haji kusimama hapo, wana wanapotokea tumboni mwa mama.
14
Nitawakomboa katika nguvu za kuzimuni na kuwaokoa kufani. Wewe Kifo, magonjwa yako yauayo yako wapi? Wewe Kuzimu, uchungu wako uko wapi? Ndipo, yawezayo kujutisha yatakapokuwa yamefichwa, macho yangu yasiyaone.
15
Lakini ijapo awe mwenye kuzaa miongoni mwa ndugu zake, pumzi ya Bwana itamjia kuwa upepo utokao maawioni kwa jua upande wa nyikani, kisima chake kikauke, nacho kijito chake kipwe. Yule ndiye atakayeviteka vilimbiko vyote vya vyombo vyote pia vipendezavyo.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14