bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 1
Romans 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 2 →
1
Mimi Paulo nilye mtumwa wa Kristo Yesu nimeitwa kuwa mtume kwa hivyo, nilivyochaguliwa, niutangaze Utume mwema wa Mungu.
2
Huo aliuagia kale kwa vinywa vya Wafumbuaji wake waliouandika katika barua takatifu;
3
ni mambo ya Mwana wake Yesu Kristo, Bwana wetu. Huyu alizaliwa kimtu katika uzao wa Dawidi,
4
tena hapo, alipofufuliwa katika wafu, ikatokea waziwazi, ya kuwa ni Mwana wa Mungu kwa nguvu ya Kiroho iliyo yenye kutakasa.
5
Yeye ndiye aliyetugawia kuwa mitume, tuwafundishe wamizimu wote usikivu wa kumtegemea, Jina lake litukuzwe.
6
Miongoni mwao mlikuwa nanyi, mkaitwa na Yesu Kristo.
7
Nawaandikia nyote mnaokaa Roma, mlio wapenzi wa Mungu, mlioitwa kuwa watakatifu: Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo!
8
Kwanza ninamshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu ninyi nyote, kwa kuwa hivyo, mnavyomtegemea, hutangazwa ulimwenguni mote.
9
Kwani Mungu, ninayemtumikia moyoni mwangu kwa kuutangaza Utume mwema wa Mwana wake, huyu Mungu ni shahidi wangu, ya kuwa sikuacha kuwakumbuka ninyi
10
siku zote po pote, ninapoomba. Ninalojiombea ni hili: Mungu apendezwe kunifungulia ile njia nzuri ya kuja kwenu,
11
kwani ninatunukia kuonana nanyi, nipate kuwagawia nanyi kipaji chochote cha Kiroho, mshupazwe vizuri.
12
Hivyo tutatulizana mioyo pamoja nanyi na kuonyeshana mategemeo yetu, tunayoyakalia ninyi na mimi.
13
*Lakini ndugu zangu, sitaki, mkose kujua, ya kuwa nilijielekeza mara nyingi, nije kwenu, nione pato hata kwenu, kama nilivyoliona kwa wamizimu wengine; lakini nimezuiliwa mpaka leo hivi.
14
Nimeingia udeni kwa Wagriki hata kwa washenzi, kwa wajuzi hata kwa wapuzi.
15
Kwa hivyo, nilivyo mimi, nimekwisha kujifunga, niwapigie nanyi ile mbiu njema huko Roma.
16
Maana sioni soni ya kuutangaza Utume mwema wa Kristo, kwani unayo nguvu ya Mungu ya kuwaokoa wo wote wanaoutegemea, kwanza Wayuda, kisha Wagriki nao.
17
Kwani humo unafunuliwa wongufu wa Kimungu, wanaopewa wenye kumtegemea, wajikaze kumtegemea. Ndivyo vilivyoandikwa ya kuwa: Mwongofu atapata uzima kwa kumtegemea Mungu.
18
Kwani makali ya Mungu yanashuka toka mbinguni, yawatokee watu wote wasiomcha Mungu nao wenye upotovu, wanaoyazuia yaliyo ya kweli kwa upotovu wao;
19
kwani mambo ya Mungu yametambulikana kwao, maana yalifumbuliwa, naye Mungu ndiye aliyewafumbulia.
20
Kwani hivyo, ambavyo macho ya watu hayajaviona, maana nguvu yake ya kale na kale na Kimungu chake, hujulikana, tena huonekana, mtu akivitazama, Yeye alivyovifanya tangu hapo, alipouumba ulimwengu; kwa hiyo hawana la kujikania.*
21
Wangawa walimtambua Mungu, hawakumtukuza kwamba: Ni Mungu, wala hawakumshukuru, Kwa hiyo mawazo yao yakawa ya bure, nayo mioyo yao isiyoyajua yaliyo ya kweli ikaingiwa na giza.
22
Walipojiwazia kuwa werevu wa kweli, ndipo, walipopumbazika.
23
Wakaugeuza utukufu wa Mungu asiyeoza, wakamfananisha na mfano wa sura ya mtu anayeoza na wa ndege na wa nyama na wa wadudu.
24
Kwa hiyo Mungu akawatupa, wajichafue wakizifuata tamaa za mioyo yao na kujipujua, mpaka wakifujiana miili yao wao kwa wao;
25
ni wao hao walioigeuza kweli ya Mungu kuwa uwongo, wakakitambikia kiumbe na kukitumikia kuliko Muumbaji aliye mwenye kutukuzwa kale na kale. Amin.
26
Kwa hiyo Mungu aliwatupa, waingiwe na tamaa za upujufu. Kwani hata wanawake wao wakayageuza matumikio yao ya kimtu, wakazusha mengine yasiyo ya kimtu.
27
Vile vile hata waume wakaacha kuwatumia wanawake kimtu, tena kwa hivyo, tamaa zao zilivyowachoma kama moto, wakatumiana waume na waume wenzao; wakafanya hayo yasiyopasa kamwe, wakapata malipo ya upotevu wao yaliyowapasa.
28
Tena kwa hivyo, walivyokataa kumshika Mungu na kumtambua, Mungu aliwatupa, wafuate mawazo ya ujinga na kufanya yasiyompasa mtu.
29
Wakaenea upotovu wote na ubaya na choyo na uovu, wakajaa kijicho na uuaji na magombano na manyatio na mazoezo maovu.
30
Ndio watetaji, wabishi, wasingiziaji, wenye kumbeza Mungu na kubeza watu, wenye kujivuna na kujitukuza, wenye maoneo maovu na wenye kuwakataa wazee.
31
Hawana utambuzi wala welekevu wala upendo wala huruma.
32
Nao walikuwa wameyambua yaliyoongoka mbele ya Mungu kwamba: Wanaoyatenda mambo hayo wamepaswa na kuuawa; tena hawayafanyi tu hayo, lakini nao wengine wakiyatenda, wanapendezwa.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16