bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 6
Romans 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 7 →
1
Sasa tusemeje? Tufulize kukosa, magawio nayo yafurike?
2
La, sivyo! Sisi tulioyafia makosa tutawezaje kuishi nayo tena?
3
*Au hamjui, ya kuwa sote tuliobatiziwa, tuwe wake Kristo Yesu, tulibatiziwa, tufe naye?
4
Hivyo tulizikwa pamoja naye tulipobatiziwa, tufe naye, ni kwamba: Kama Kristo alivyofufuliwa katika wafu kwa nguvu ya utukufu wa Baba, vivyo nasi sharti tupate upya wa maisha, tuendelee nao.
5
Kwani tulivyounganika naye tulipokufa, kama alivyokufa, vivyo tutafufuka nasi, kama alivyofufuka yeye.
6
Kwani tunalitambua neno hili: mtu wetu wa kale amewambwa msalabani pamoja naye, miili yetu yeye kukosa ipate kukomeshwa, sisi tusiyatumikie tena makosa kama watumwa.
7
Kwani aliyekufa amekwisha kupata wongofu kwa kuondolewa kwenye makosa.
8
Nasi kama tumekufa pamoja na Kristo, tunalitegemea la kwamba: Tutaishi pamoja naye.
9
Kwani twajua, ya kuwa Kristo hafi tena kwa hivyo, alivyofufuliwa katika wafu, kifo hakina ufalme tena wa kumshika.
10
Kwani hivyo, alivyokufa, aliyafia makosa na kuyashinda papo hapo; lakini hivyo, anavyoishi, anaishi, amtumikie Mungu.
11
Nanyi jiwazieni hivyo: makosa mmekwisha kuyafia, lakini sasa mnaishi, mmtumikie Mungu katika Kristo Yesu!*
12
Kwa hiyo ukosaji usishike ufalme katika miili yenu yenye kufa, mzitii tamaa zao!
13
Wala msivitoe viungo vyenu, viwe mata ya upotovu ya kuyatumikia makosa! Ila mjitoe wenyewe kumtumikia Mungu kwa hivyo, mnavyoishi, tena mlikuwa mmekwisha kufa! Navyo viungo vyenu mvitoe, viwe mata ya wongofu ya kumtumikia Mungu!
14
Kwani ukosaji hautashika ufalme, uwatawale, maana nguvu yenu siyo ya Maonyo, ila ya upole.
15
Basi, inakuwaje? Tukose vivyo hivyo, kwa sababu nguvu yetu siyo ya Maonyo, ila ya upole? La sivyo!
16
Hamjui, vilivyo? Ni hivi: mnapojitoa wenyewe kumtumikia mtu kitumwa na kumtii, basi, mmekwisha kuwa watumwa wake yeye, mnayemtii. Ikiwa ni wa ukosaji, mnakwenda kufa; ikiwa ni wa wito, mnakwenda kupata wongofu.
17
Lakini Mungu atolewe shukrani, kwa sababu ninyi mliokuwa watumwa wa ukosaji mmegeuzwa mioyo, mkaja kuyatii mafundisho, kama mlivyoyapata!
18
Napo hapo, mlipokombolewa katika utumwa wa ukosaji, mmegeuka kuwa watumwa wa wongofu.
19
*Nasema kimtu kwa ajili ya unyonge wa miili yenu: Kama mlivyovitoa viungo vyenu kuutumikia kitumwa uchafu na upotovu, mkajifikisha penye kupotolewa, vivyo hivyo vitoeni sasa viungo vyenu kuutumikia kitumwa wongofu, mjifikishe penye kutakaswa!
20
Kwani mlipokuwa watumwa wa ukosaji, siku zile mlikuwa hamna wongofu hata kidogo.
21
Basi, siku zile mlikuwa na mapato gani? Sasa hivi mnayaonea soni, kwani mwisho wao ni kufa.
22
Lakini sasa kwa kuwa mmekwisha kukombolewa katika utumwa wa ukosaji, mkawa watumwa wake Mungu, mnayo mapato yenu kwa kujifikisha penye kutakaswa, tena mwisho mtapata uzima wa kale na kale.
23
Kwani mshahara wa ukosaji ni kufa; lakini gawio, Mungu analotupa katika Bwana wetu Kristo Yesu, ni uzuma wa kale na kale.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16