bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 10
Romans 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 11 →
1
*Ndugu, moyo wangu unayapenda sana, ninayomwomba Mungu kwamba: Waisiraeli waokoke.
2
Kwani nawashuhudia, ya kuwa waona wivu kwa ajili yake Mungu, lakini hawamtambui.
3
Kwani wongofu, Mungu anaoutaka, hawaujui, wakajaribu kujiongoza wenyewe, lakini hivyo hawakuutii ule wongofu, Mungu anaoutaka.
4
Kwani timilizo la Maonyo ni Kristo, kila mwenye kumtegemea ajipatie wongofu!
5
Kwani Mose aliandika: Anayeufanya wongofu ulioagizwa na Maonyo mtu huyo atapata uzima kwa njia hiyo.
6
Lakini wongofu unaopatikana kwa kumtegemea Mungu unasema hivyo: Usiseme moyoni mwako: Yuko nani atakayepaa kwenda mbinguni? Huko ndiko kumshusha Kristo.
7
Wala usiseme: Yuko nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? Huko ndiko kumpaza Kristo na kumtoa kwenye wafu.
8
Tena unasema: Neno hilo linakukalia karibu, limo kinywani mwako, namo moyoni mwako. Hilo ndilo neno la kumtegemea Mungu, ni hilihili, tunalolitangaza.
9
Kwani ukiungama kwa kinywa chako kwamba: BWANA NI YESU, ukamtegemea kwa moyo wako kwamba: Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
10
Kwani ukimtegemea kwa moyo unapata wongofu; ukimwungama kwa kinywa unaokoka.
11
Kwani Maandiko yasema: Kila anayemtegemea hatatwezeka.
12
Kwani hapa hawachaguliwi Wayuda na Wagriki; kwani aliye Bwana wao wote ni yuyu huyu mmoja, ni mwenye magawio yanayowatoshea wote wanaomtambikia.
13
Kwani; Kila atakayelitambikia Jina la Bwana ataokoka.
14
Basi, watamtambikiaje, wasiyemtegemea? Tena watamtegemeaje, ambaye hawajamsikia Neno lake? Tena watasikiaje, pasipokuwapo mwenye kutangaza?
15
Tena watatangazaje, wasipotumwa? Ndivyo ilivyoandikwa: Tazameni, miguu yao wapiga mbiu njema jinsi inavyopendeza!*
16
Lakini walioutii huo Utume mwema sio wote. Kwani Yesaya anasema: Bwana, yuko nani anayeutegemea utume wetu?
17
Basi, kumtegemea Mungu huletwa na matangazo, lakini matangazo hutoka katika Neno la Kristo.
18
Lakini niseme: Hawakusikia? Kusikia wamesikia. Uvumi wao ulitokea katika nchi zote; nayo maneno yao yalifika hata mapeoni kwa ulimwengu.
19
Au niseme: Waisiraeli hawakulitambua? Kwanza Mose anasema: Mimi na niwachokoze ninyi nikiwaletea watu wasio watu, na niwakasirishe ninyi nikiwaletea taifa la watu wasiojua maana.
20
Kisha Yesaya anajipa moyo wa kusema: Nimeonwa nao wasionitafuta, nikawatokea wasioniuliza.
21
Lakini Waisiraeli anawaambia: Mchana kutwa naliikunjua mikono yangu, nipungie ukoo wa watu wasioonyeka, walio wabishi tu.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16