bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 3
Romans 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 4 →
1
Ikiwa hivyo, Wayuda wanapitaje wengine? Au kutahiriwa kunafaaje?
2
Hufaa sana hapo na hapo. Kwanza waliagiziwa maneno yake Mungu.
3
Au mwawazaje? Wengine wao wakikataa kuyategemea, huo ukatavu wao utautangua welekevu wake Mungu?
4
La, sivyo! Sharti Mungu ajulikane kuwa mwenye kweli, lakini kila mtu sharti ajulikane kuwa mwenye uwongo, kama ilivyoandikwa: Sharti wongofu wako utokezwe na maneno yako, upate kushinda utakapobishiwa.
5
Lakini upotovu wetu ukiutokeza wongofu wake Mungu, tutasemaje? Je? Mungu naye siye mpotovu akitutolea makali? (Nasema kimtu.)
6
La, sivyo! Mungu angaliwezaje kuuhukumu ulimwengu?
7
Lakini kweli ya Mungu ikiongezwa utukufu na uwongo wangu, mimi tena ninahukumiwaje kama mkosaji?
8
Hivyo sivyo, tunavyosingiziwa, wengine wakitusema sisi, kwamba tumesema: Na tuyafanye yaliyo maovu, yaliyo mema yapate kutokea? Hao hukumu yao inapasa kabisa.
9
Sasa Je? Tumewapita? Hapana, hata kidogo tu. Kwani hapo mbele tumewasuta wote, Wayuda na Wagriki, kwamba: Wote ni wakosaji,
10
kama ilivyoandikwa: Hakuna aliye mwongofu hata mmoja.
11
Hakuna aliye mwenye akili, hakuna anayemtafuta Mungu.
12
Wote pamoja wamepotelewa na njia, wote ni waovu. Hakuna anayefanya mema, hakuna hata mmoja.
13
Makoo yao huwa makaburi yaliyo wazi, ndimi zao huzitumia uwongo tu, sumu ya pili imo midomoni mwao.
14
Vinywa vyao hujaa matusi na uchungu,
15
miguu yao hupiga mbio kuja kumwaga damu.
16
Maangamizo na mavunjiko huzijulisha njia zao,
17
lakini njia ya utengemenao hawaijui.
18
Kumwogopa Mungu hakupo machoni pao.
19
Lakini sisi twajua: Yote, Maonyo yanayosema, huwaambia wenye kuyashika Maonyo, kila kinywa kifumbwe, nao ulimwengu wote uwe umepaswa na hukumu ya Mungu.
20
Kwa hiyo hapo, alipo, hapana mwenye mweli wa kimtu atakayepata wongofu kwa kwamba: Ameyafanya Maonyo, kwa sababu Maonyo huleta utambuzi tu wa makosa.
21
*Lakini sasa wongofu wa Kimungu umefunuliwa pasipo Maonyo; nao unashuhudiwa na Maonyo pamoja na Wafumbuaji kwamba:
22
Wongofu wa Kimungu ndio huu: mwanzo ni kumtegemea Yesu Kristo, nao mwisho: wote wanaomtegemea huupata. Kwani hawapitani,
23
kwa sababu wote wamekosa, wakalipoteza fungu lao la utukufu wa Mungu.
24
Kwa hiyo wanapata wongofu bure tu, kwani ni gawio, Yesu Kristo alilowapatia hapo, alipoyalipa makombozi yao.
25
Ndiye, Mungu aliyemtoa, kusudi wenye kumtegemea wajipatie Kiti cha Upozi katika damu yake; hapo ndipo, alipoonyesha, wongofu wake ulivyo, akiwaondolea makosa ya kale,
26
ambayo Mungu alikuwa akiyavumilia. Hivi ndivyo, alivyouonyesha siku hizi za sasa wongofu wake kuwa hivyo: Mwenyewe ni mwongofu, tena mwenye kumtegemea Yesu humpa wongofu.
27
Basi, majivuno yako wapi? Yamefungiwa! Kwa nguvu ya maonyo gani? Ni yale yanayotaka matendo? Hapana, ni Maonyo yanayotaka kutegemewa tu.
28
Kwani tunalishika hili la kwamba: Mtu hupata wongofu kwa kumtegemea Mungu tu, ijapo asiyatimize Maonyo.*
29
Au je? Mungu ni Mungu wao Wayuda tu? Siye Mungu wa wamizimu nao? Kweli, ni Mungu wa wamizimu nao,
30
kwani Mungu ni mmoja tu; waliotahiriwa huwapatia wongofu, wakiwa wanamtegemea; vilevile wasiotahiriwa huwapatia wongofu, wakiwa wanamtegemea.
31
Je? Ikiwa hivyo, tutayatangua Maonyo kwa kule kumtegemea? Sivyo, tutayasimamisha.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16