bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 16
Romans 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
1
Nawaagiziani ndugu yetu Febe aliye mtumishi mke wa wateule wa Kenkerea,
2
mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu, tena mmsaidie jambo lo lote, atakalopaswa nanyi. Kwani mwenyewe alitunza wengi, hata mimi.
3
Nisalimieni Puriska na Akila waliofanya kazi ya Kristo Yesu pamoja nami!
4
Hao walijitoa wenyewe, wakatwe vichwa, nisiuawe mimi. Mwenye kuwashukuru si mimi peke yangu, ila hata wateule wote walioko kwenye wamizimu.
5
Nisalimieni hata wateule waliomo nyumbani mwao! Nisalimieni mpenzi wangu Epeneto! Ndiye aliyeanza kumtegemea Kristo katika Asia.
6
Nisalimieni Maria aliyetusumbukia sana!
7
Nisalimieni ndugu zangu Andoroniko na Yunia waliokuwa wamefungwa pamoja nami! Nao ni waelekevu machoni pa mitume, tena walinitangulia kumtegemea Kristo.
8
Nisalimieni Ampuliato aliye mpenzi wangu katika Bwana!
9
Nisalimieni Urbano, mwenzetu wa kazi katika Kristo, na mpenzi wangu Staki!
10
Nisalimieni Apele aliyejulikana kuwa Mkristo wa kweli! Nisalimieni wale wa Aristobulo!
11
Nisalimieni ndugu yangu Herodio! Nisalimieni wale wa Narkiso wanaomkalia Bwana!
12
Nisalimieni Tirifena na Tirifosa wanaosumbuka kwa ajili ya Bwana! Nisalimieni mpendwa Persisi kwa kuwa mwanamke aliyesumbuka sana kwa ajili ya Bwana!
13
Nisalimieni Rufo aliyechaguliwa na Bwana, naye mama yake aliye hata mama yangu!
14
Nisalimieni Asinkrito na Fulego na Herme na Patiroba na Herma na ndugu walio pamoja nao!
15
Nisalimieni Filologo na Yulia na Neri na dada yake na Olimpa nao watakatifu wote walio pamoja nao!
16
Msalimiane ninyi kwa ninyi na kunoneana, kama watakatifu wanavyozoea! Wateule wote wa Kristo wanawasalimu.
17
Lakini nawahimiza, ndugu, mwakague wenye matata na makwazo! Hawaushiki ufundisho, mliofundishwa, mwaepuke na kuwaacha!
18
Kwani watu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, ila huyatumikia matumbo yao wenyewe. Nao kwa maneno yao yaliyo mazuri na matamu mno huidanganya mioyo yao wale wasiojua ujanja.
19
Kwani usikivu wenu umejulikana kwa watu wote; hivyo ninawafurahia. Lakini nataka, mwe werevu wa kweli, mambo yenu yawe mema, tena mwe wachanga wasioingia maovu.
20
Naye Mungu mwenye utengemano atamponda Satani miguuni penu upesi. Upole wa Bwana wetu Yesu uwakalie ninyi!
21
Wanaowasalimu ninyi ni Timoteo aliye mwenzangu wa kazi na Lukio na Yasoni na Sosipatiro walio ndugu zangu.
22
Mimi Tertio niliyeiandika barua hii nami ninawasalimu ninyi kwa hivyo, ninavyomkalia Bwana.
23
Anawasalimu Gayo aliye mwenyeji wangu mimi na mwenyeji wa wateule wote. Naye Erasto aliye mshika mali za mji na ndugu Kwarto wanawasalimu.
24
Upole wa Bwana wetu Yesu Kristo uwakalie ninyi nyote! Amin.
25
Mungu ndiye anayeweza kuwashikiza ninyi kwa nguvu ya Utume mwema wa Yesu Kristo, ninaoutangaza, kwani nimefumbuliwa mambo ya fumbo yasiyosemwa kale na kale.
26
Yayo hayo yamefumbuliwa sasa na Maandiko ya Wafumbuaji kwa agizo lake Mungu, mwenye kuwapo kale na kale, wamizimu wote wafunzwe huo usikivu wa kumtegemea.
27
Yeye Mungu aliye peke yake mwenye werevu wa kweli atukuzwe kwa ajili ya Yesu Kristo kale na kale pasipo mwisho! Amin.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16