bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 12
Romans 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 13 →
1
*Nawaonya, ndugu, kwa hivyo, Mungu alivyowaonea uchungu, mtoe miili yenu, iwe vipaji vitakatifu vya tambiko vyenye uzima vya kumpendeza Mungu; huko ndiko kumtumikia Mungu kunakoelekea.
2
Msijifananishe nao walio wa siku hizi tu, ila mgeuke, mpewe mawazo mapya, mpate kuyapambanua, Mungu ayatakayo kwamba: Ni mema ya kumpendeza hapo, yatakapotimilika.
3
Kwa kipaji, nilichogawiwa, namwambia kila mmoja wa kwenu, asiwaze makuu yanayopapita hapo panapopasa kuwaza. Ila awaze, jinsi atakavyopata kuerevuka, kila mtu, kama Mungu alivyomgawia kumtegemea.
4
Kwani ni vivyo hivy: tunavyo viungo vingi katika mwili mmoja, lakini viungo vyote havina kazi moja.
5
Vivyo sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa maana tu wa Kristo, tena kila mmoja na mwenzake tu viungo tu.
6
Tena vipaji, tulivyopewa ni vingi, kila mtu anacho chake, kama alivyogawiwa.* *Mwenye ufumbuaji sharti aupatanishe na kumtegemea Mungu.
7
Mwenye utumishi sharti atumike kweli! Mfunzi na aushike ufundisho wake!
8
Mwenye kuonya sharti aonyeke! Mwenye kugawia sharti anyenyekee! Aliye mkuu sharti ajihimize! Mwenye kutunza wengine sharti avifurahie!
9
Mapendano yasiwe ya uwongo! Yachukieni yaliyo mabaya mkigandamiana nayo yaliyo mema!
10
Mpendane kindugu kwa mioyo, tena mwongozane na kuheshimiana ninyi kwa ninyi!
11
Msilegee, panapotakwa wenye kujikaza! Roho zenu ziwe zenye moto mnapomtumikia Bwana!
12
Furahini, ya kwamba mnacho kingojeo! Yavumilieni maumivu! Fulizeni kuomba!
13
Changeni bia, mwapatie watakatifu, wanavyovikosa! Wageni wapokeeni pasipo kunung'unika!
14
Changeni bia, mwapatie watakatifu, wanavyovikosa! Wageni wapokeeni pasipo kunung'unika!
15
Furahini pamoja nao wafurahio! Lieni pamoja nao waliao!
16
Mioyo yenu nyote sharti iwe mmoja! Msiyatunukie yaliyo makuu, ila yaliyo manyonge, mfuatane nayo! Msijiwazie wenyewe kuwa wenye akili!*
17
*Msimlipe mtu maovu kwa maovu! Yawazeni yaliyo mazuri mbele ya watu wote!
18
Kwa hivyo, mlivyo, mwe wenye kupatana na watu wote, ikiwezekana!
19
Wapendwa, msijilipize wenyewe, ila jitengeni, makali (ya Mungu) yapate kutokea! Kwani imeandikwa: Bwana anasema: Lipizi ni langu mimi, ni mimi nitakayelipisha.
20
Lakini mchukivu wako akiwa ana njaa, mpe chakula! Akiwa ana kiu, mpe cha kunywa! Kwani ukivifanya hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
21
Usishindwe nayo yaliyo maovu, ila maovu uyashinde kwa mema!*
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16