bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 7
Romans 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 8 →
1
Na niseme nanyi, kwa kuwa mnayatambua Maonyo: Hamjui, ndugu: Maonyo humshika mtu siku zote za maisha yake?
2
Kwani mwanamke aliye na mume siku za kuishi kwake mumewe ana mwiko kwa ajili ya Maonyo; lakini nguvu ya hayo Maonyo hukoma, mumewe anapokufa, hana mwiko tena wa mwanamume mwingine.
3
Siku za kuishi kwake mumewe, yeye akiwa wa mume mwingine, huitwa mzinzi. Lakini mumewe anapokufa, amefunguliwa na Maonyo, asiwe tena mzinzi akiwa wa mume mwingine.
4
Ndugu zangu, hapo Kristo alipokufa, mliuawa nanyi, mkayafia Maonyo; kwa hiyo mmefunguliwa nanyi kuwa wa mwingine, maana ni wa yule aliyefufuliwa katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.
5
Kwani hapo, mwenendo wetu ulipokuwa wa kimtu, tamaa mbaya zikatuumiza sana, nazo nguvu zao zikaongezeka tu katika viungo vyetu kwa kukatazwa na Maonyo, tukakizalia kifo matunda.
6
Lakini sasa tumefunguliwa, hiyo nguvu ya Maonyo isitushike, tukamfia yule aliyetupinga; hivyo ndivyo, utumikizi wetu ulivyopata kuwa mpya wa kiroho, wa kale uliokuwa wa utumwa wa maandiko ukome.
7
*Sasa tusemeje? Maonyo hukosesha? La, sivyo! Lakini kosa singelitambua pasipo Maonyo. Kwani hata tamaa singeijua, kama Maonyo yasingesema: Usitamani!
8
Lakini ukosaji ulianzia hapohapo penye agizo hilo, ukakuza moyoni tamaa yo yote, ukaitia nguvu; kwani pasipo Maonyo ukosaji ni mfu.
9
Nami kale nilikuwa ninaishi pasipo Maonyo; lakini agizo lilipokuja, ukosaji ukafufuka,
10
nami nikafa; hivyo agizo lililotokea, linipe uzima, likaonekana, ya kuwa ni lilo hilo lililoniua.
11
Kwani ukosaji ulianzia hapohapo penye agizo hilo, ukanidanganya, ukaniua kwa hilo agizo.
12
Kwa hiyo Maonyo ni matakatifu, nalo agizo ni takatifu lenye wongofu na wema.
13
Basi, inakuwaje? Lililo jema ndio lililoniua mimi? La, sivyo! Ila ukosaji ndio ulioniua; lakini kusudi uonekane kuwa ukosaji, ukaniua kwa lile lililo jema; kwa hivyo, ukosaji ulivyolitumia lile agizo, ukatokea wazi kuwa ukosaji wenyewe usiozuilika kabisa.
14
Kwani Maonyo tunayajua, ya kuwa ni ya Kiroho; lakini mimi ni wa kimtu, nikauzwa kuwa mtumwa wa ukosaji.
15
Kwani siyatambui, ninayoyatenda: kwani ninachokitaka sikifanyi, ila ninachokichukia, ndicho, ninachokifanya.
16
Nami nisichokitaka, ninapokifanya hichohicho, basi, ninayaitikia Maonyo kuwa mazuri.*
17
Sasa si mimi ninayekifanyiza hicho, ila ndio ukosaji unaonikalia moyoni.
18
Kwani najua: Humu ndani yangu, maana mwilini mwangu, hamna chema cho chote; kama ni kutaka, ninako, lakini kama ni kukifanya kilicho kizuri, sinako.
19
Kwani kilicho chema, ninachokitaka, sikifanyi; ila kilicho kiovu, nisichokitaka, ndicho, ninachokifanyiza.
20
Lakini mimi nisichokitaka, ninapokifanya hichohicho, basi, si mimi tena ninayekifanya, ila ndio ukosaji unaonikalia moyoni.
21
Hivyo mimi ninayetaka kukifanya kilicho kizuri, ninaona nguvu ngeni kwangu inayonishurutisha kukifanya kilicho kiovu.
22
Kwani ninayaitikia Maonyo yake Mungu na kuyashangilia huku ndani moyoni.
23
Lakini naona, yamo maonyo mengine viungoni mwangu yanayoyagombeza Maonyo yaliyomo rohoni mwangu, yakaniteka kuwa mtumwa wa maonyo yanayonikosesha, ndiyo yale yaliyomo viungoni mwangu.
24
Yamenipata mimi mtu mkiwa! Yuko nani atakayenikomboa utumwani mwa mwili huu wa kufa?
25
Mungu atolewe shukrani kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo! Basi, kwa akili zangu mimi mwenyewe nayatumikia kitumwa Maonyo yake Mungu, lakini mwilini ni mtumwa wa maonyo ya ukosaji.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16