bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 15
Romans 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 16 →
1
Sisi tulio wenye nguvu imetupasa kuyavumilia manyonge yao wenye kukosa nguvu, tusijipendeze wenyewe.
2
Kwetu kila mmoja sharti ampendeze mwenziwe, tusaidiane kujengana vizuri!
3
Kwani naye Kristo hakujipendeza mwenyewe; ila ilikuwa, kama ilivyoandikwa: Masimango yao wanaokusimanga yameniguia mimi.
4
*Kwani yote yaliyoandikwa kale yamendikwa, yatufundishe, tupate kukishika kingojeo chetu tukivumilia, tena tukitulizwa mioyo na yale Maandiko.
5
Naye Mungu mwenye uvumilivu na mwenye kuituliza mioyo ya watu awape, mioyo yenu nyote iwe mmoja tu, kama inavyowapasa walio wa Kristo Yesu!
6
Hivyo mtamtukuza Mungu, Baba ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja.
7
Kwa hiyo mpokeane, kama Kristo alivyotupokea na sisi, Mungu atukuzwe!
8
Kwani nasema: Kristo aliwatumikia waliotahiriwa, ajulishe, ya kuwa Mungu ni mkweli, navyo viagio, baba walivyopewa, akavipatia nguvu.
9
Tena anasema: Wamizimu humtukuza Mungu kwa ajili ya kuhurumiwa, kama ilivyoandikwa: Kwa hiyo nitakuungama kwenye wamizimu, nalo Jina lako na niliimbie.
10
Tena anasema: Furahini, enye wamizimu, pamoja nao walio ukoo wake!
11
Na tena: Mshangilieni Bwana, ninyi wamizimu wote, makabila yote ya watu yamsifu!
12
Tena Yesaya anasema: Shinani mwa Isai ataondokea mwenye kuwatawala wamizimu; huyo ndiye, wamizimu watakayemngojea.
13
Naye Mungu, mnayemngojea, awajaze ninyi nyote furaha na utengemano kwa hivyo, mnavyomtegemea, kingojeo chenu kiongezwe nguvu itokayo kwa Roho Mtakatifu!*
14
Nami mwenyewe, ndugu zangu, nayashika moyoni, kama yalivyo kweli, ya kuwa mema yenu ninyi ni mengi, tena utambuzi wenu ni mwingi, mkaweza hata kuonyana wenyewe.
15
Kwa hiyo nimejipa moyo wa kuwaandikia neno mojamoja na kutokeza maana kama mtu anayewakumbusha. Kwani hiki ndicho kipaji changu, nilichogawiwa na Mungu,
16
nimtumikie Kristo Yesu nikiwatangazia wamizimu Utume mtakatifu wa Mungu na kuwaombea, kusudi wawe kipaji cha tambiko kipendezekacho, kwa kuwa kimetakaswa katika Roho Mtakatifu.
17
Basi, kwa hivyo, ninavyoshikamana na Kristo Yesu, ninaweza kujivunia kazi zake Mungu.
18
Kwani sitajipa moyo wa kusema neno au tendo lo lote, asilolitenda Kristo hapo, nilipoleta wamizimu, wapate kumtii;
19
kwani nguvu iliyowashinda ilikuwa ya vielekezo na ya vioja vyake, tena ile ya Roho takatifu. Hivyo nimeutangaza Utume mwema wa Kristo po pote, nikaanza Yerusalemu, nikaifikisha hata Iliriko na kuzieneza nchi zote zilizoko pembenipembeni.
20
Nikajitunukia, nisiipige hiyo mbiu njema mahali, Kristo alipokwisha kutangazwa, maana nisiujengee msingi wa mtu mwingine,
21
ila yawe, kama yalivyoandikwa: Watakaomwona ndio wasioambiwa Neno lake nao wasiolisikia watalijua maana.
22
Kwa ajili hiyo nalizuiliwa mara nyingi kuja kwenu.
23
Lakini sasa katika nchi za upande huu hakuna, nilikosaza, tena tangu miaka mingi ninatunukia, nije kwenu;
24
nitawafikia hapo, nitakapokwenda Spania. Kwani natazamia kuonana nanyi, nitakapopita, nisindikizwe nanyi kwenda huko; lakini kwanza tupeane kikomo cha maneno na kufurahishana kitambo.
25
Lakini sasa ninakwenda Yerusalemu, niwatumikie watakatifu.
26
Kwani Wamakedonia na Waakea wamependezwa kuchanga machango ya kuwasaidia watakatifu walio maskini huko Yerusalemu.
27
Nao walichanga kwa kupendezwa, tena ndio wadeni wao. Maana wamizimu wakigawiwa nao mali za Kiroho, imewapasa nao kuwatumikia hao na kuwagawia mali za kimtu.
28
Basi, nitakapolimaliza jambo hilo, nikiwapa pato hilo na kulishuhudia, nitaondoka kwenda Spania na kupitia kwenu.
29
Nami najua, ya kuwa nitakapokuja kwenu nitakuja mwenye mema yote, Kristo anayotupa.
30
Lakini ndugu, nawahimiza kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo na kwa hivyo, tunavyopendana Rohoni, mnipiganie na kuniombea kwa Mungu,
31
nipate kupona katika wale wasiotii huko Yudea, tena huu utumishi wangu upendezeke kwao watakatifu huko Yerusalemu,
32
nami nipate kuja kwenu na kufurahi, tupatiane vituo, Mungu akitaka.
33
Naye Mungu mwenye utengemano awe pamoja nanyi nyote! Amin.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16