bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 8
Romans 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 9 →
1
*Sasa hakuna tena kinachowapatiliza walio katika Kristo Yesu, wasioendelea kimtu, ila Kiroho.
2
Kwani Maonyo ya Roho inayotupatia uzima katika Kristo Yesu yamenikomboa utumwani mwa maonyo ya ukosaji yaliyoniua.
3
Kwani vile, ambavyo Maonyo hayakuweza kuvimaliza kwa ajili ya unyonge wa miili ya kimtu, Mungu alivifanya alipomtuma Mwana wake mwenyewe; akaja mwenye mwili wa makosa, akakamatwa kuwa kole ya makosa; hivyo ndivyo, alivyoyapatiliza makosa katika mwili ulio wa kimtu,
4
wongofu unaotakwa na yale Maonyo utimilizike mioyoni mwetu sisi, tusioendelea kimtu, ila Kiroho.
5
Kwani walio wa kimtu huyawaza mambo ya kimtu, lakini walio wa Kiroho huyawaza mambo ya Kiroho.
6
Kwani mawazo ya kimtu huleta kufa; lakini mawazo ya Kiroho huleta uzima na utengemano.
7
Kwa sababu hiyo mawazo ya kimtu humchukia Mungu; kwani hayataki kuyatii Maonyo ya Mungu, wala hayawezi kuyatii;
8
kwa hiyo walio wa kimtu hawawezi kumpendeza Mungu.
9
Lakini ninyi ham wa kimtu, ila wa Kiroho, kama Roho ya Mungu inawakalia mioyoni; lakini asiye na Roho ya Kristo huyo si wake.
10
Lakini Kristo akiwakalia mioyoni, kweli miili itakufa kwa ajili ya makosa, lakini roho zitaishi kwa ajili ya wongofu.
11
Lakini Roho yake yule aliyemfufua Yesu katika wafu ikiwakalia mioyoni, yuyu huyu aliyemfufua Yesu Kristo katika wafu atairudisha uzimani hata miili yenu, itakapokwisha kufa; atayafanya kwa nguvu ya Roho yake inayowakalia mioyoni.
12
*Kwa hiyo, ndugu, hatumo tena katika udeni wa miili yetu ya kimtu, tuendelee kimtu;
13
kwani mnapoendelea kimtu mtakufa. Lakini mnapoyaua matendo ya miili yenu ya kimtu kwa nguvu ya Roho mtapata kuishi.
14
Kwani wote wanaoongozwa na Roho ya Mungu hao ndio wana wa Mungu.
15
Kwani hamkupewa tena roho ya kitumwa, mshikwe na woga, ila mmepewa Roho ya kimwana, ndiyo inayotufundisha kuomba: Ee, Baba yetu!
16
Hiyo Roho yake yenyewe huzishuhudia roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wake Mungu.
17
Lakini tukiwa watoto, basi, tunakuwa hata warithi, maana warithi wake Mungu watakaopata urithi pamoja na Kristo; tukiwa tunateswa pamoja naye tutapata hata kutukuzwa pamoja naye.
18
*Kwani naona, ya kuwa mateso ya siku hizi za sasa si kitu, tukiyafananisha na ule utukufu, tutakaofunuliwa sisi.
19
Kwani viumbe vyote vinavumilia na kuyachungulia matokeo ya wana wa Mungu.
20
Kwani viumbe vimewekwa, vioze, si kwa mapenzi yao wenyewe, ila kwa ajili yake aliyeviweka hivyo; navyo viko na kingojeo chao.
21
Kwani viumbe navyo vitakombolewa katika utumwa wa kuoza, viingie navyo uungwana uliomo katika utukufu wa watoto wake Mungu.
22
Kwani twajua, ya kuwa viumbe vyote vipo pamoja nasi vikipiga kite kwa kuona uchungu mpaka sasa hivi.
23
Tena sivyo hivyo tu, ila na sisi wenyewe tuliokwisha pata malimbuko ya Roho twapiga kite ndani mioyoni tukichungulia kuwa wana, kwani ndipo, miili yetu nayo itakapokombolewa.
24
*Kwani kingojeo, ambacho tuliokolewa, tuwe nacho, hicho ndicho; lakini kingojeo kinachoonekana machoni sicho kingojeo. kwani hilo, mtu analoliona, analingojeaje?
25
Lakini tusiloliona, tukilingojea, tunalichungulia kwa kuvumilia.
26
Hivyo hata Roho hutusaidia sisi tulio wanyonge. Kwani tusipojua maombo yanayopasa, hapo Roho mwenyewe hutuombea, tukipiga kitekite tu kisichosemekana.
27
Lakini yeye nayeipeleleza mioyo ameyajua mawazo ya Roho, kwani huwasemea watakatifu Kimungu.*
28
Tunajua, ya kuwa: Kwao wanaompenda Mungu mambo yote husaidiana kuwapatia mema; ndio hao, aliowaita kwa yale, aliyowawekea kale.
29
Kwani aliowatambua kale, ndio, aliowachagua kale, wafanane na Mwana wake wakiwa sura moja naye, yeye apate kuwa Kibwana katika wanduguze wengi.
30
Nao aliowachagua kale, hao ndio, aliowaita; nao aliowaita, hao ndio aliowapa wongofu; nao aliowapa wongofu, hao ndio, aliowatukuza.
31
Hayo yote tuyasemeje? Mungu akiwa upande wetu, yuko nani atakayetushinda?
32
Hakumwonea Mwana wake mwenyewe uchungu, ila alimtoa kwa ajili yetu sisi sote; kwa hiyo asitupatie sisi magawio yote kwake yeye?*
33
*Yuko nani atakayewasuta waliochaguliwa na Mungu? Mungu yuko anayewashuhudia kuwa waongofu.
34
Yuko nani atakayewahukumu? Kristo Yesu yuko aliyekufa kwa ajili yao, na kupita hapo amefufuka, yuko kuumeni kwa Mungu na kutusemea sisi.
35
Yuko nani atakayetutenga na upendo wake Kristo? Maumivu au masongano au mafukuzo au njaa au uchi au maponzo au panga?
36
Ndivyo vilivyoandikwa kwamba: Kumbe ni kwa ajili yako wewe, tukiuawa kila siku tukihesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa tu!
37
Lakini katika mambo hayo yote tunazidi kushinda kabisa kwa nguvu yake yeye aliyetupenda sisi.
38
Kwani hili nimelitambua kuwa kweli kabisa: Kukiwa kufa au kuishi, wakiwa malaika au wenye nguvu, yakiwa ya leo au ya kale, zikiwa nguvu
39
za mbinguni juu au za kuzimuni chini, vikiwa viumbe vyo vyote vingine, hakuna kitakachoweza kututenga sisi na upendo wake Mungu uliotutokea katika Kristo Yesu, Bwana wetu.*
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16