bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 9
Romans 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 10 →
1
Kristo anajua: nasema kweli, sisemi uwongo; hata moyo wangu unaoyajua hunishuhudia katika Roho takatifu,
2
ya kuwa masikitiko yangu ni makubwa, nao uchungu haukomi moyoni mwangu.
3
Kwa hiyo naliomba mara kwa mara, mimi mwenyewe niapizwe, niondolewe kwake Kristo, kama hivyo vingeweza kuwaponya ndugu zangu, ambao tulizaliwa nao kimtu.
4
Kweli ndio Waisiraeli, tena ni wana, hata utukufu wanao, walipewa maagano na maonyo na tambiko lililo la kweli na viagio.
5
Wanao hata baba, namo miongoni mwao ndimo, Kristo alimozaliwa kimtu; huyu ni mkubwa kuwapita wote, ni Mungu, atukuzwe kale na kale! Amin.
6
Lakini sisemi hivyo, kwamba Neno lake Mungu limetenguka. Kwani walio kizazi chake Isiraeli sio wote Waisiraeli.
7
Wala walio wa uzao wake Aburahamu sio wote hata watoto. Ila imeandikwa: Watakaoitwa uzao wako ni wa Isaka tu.
8
Ni kwamba: Walio watoto wa kimtu hao sio watoto wake Mungu; ila walio watoto wa kiagio huwaziwa kuwa uzao.
9
Kwani neno la kiagio ni hilo la kwamba: Nitakapokuja siku zizi hizi za mwaka ujao, ndipo, Sara atakapokuwa mwenye mtoto wa kiume.
10
Lakini hivyo haikuwa hapo tu, ilikuwa napo hapo, Rebeka alipopata mimba kwake yule mmoja aliye baba yetu Isaka.
11
Kwani hapo, watoto walipokuwa hawajazaliwa, wala hawajafanya mema au maovu, hapo ndipo, Mungu alipowachagulia kwa hivyo, alivyowawekea kale, viwepo.
12
Vikawapo, si kwa ajili ya matindo yao, ila kwa wito wake yeye. Kwa hivyo Rebeka aliambiwa: Mkubwa atamtumikia nduguye.
13
Ndivyo, ilivyoandikwa: Nilimpenda Yakobo, lakini Esau nilimchukia.
14
Basi, tusemeje? Kwa Mungu uko upotovu? La, sivyo!
15
Kwani anamwambia Mose: Nitakayemhurumia, nitamhurumia kweli; nitakayemwonea uchungu, nitamwonea uchungu wa kweli.
16
Kwa hiyo kutaka kwa mtu siko, wala mbio zake sizo, ila Mungu mwenye huruma ndiye yeye tu.
17
Kwani Maandiko yanamsema Farao: Kwa sababu hiihii nimekuweka, niionyeshe nguvu yangu kwako wewe, Jina langu lipate kutangazwa katika nchi zote.
18
Kwa hiyo humhurumia, anayemtaka; tena humshupaza, anayemtaka.
19
Labda utaniambia: Mbona hutukamia? Kwani yuko nani ayapingaye mapenzi yake?
20
Mwenzangu, u mtu gani ukitaka kubishana na Mungu? Je? Kiko chombo kitakachomwambia muumbaji: Mbona umenifanya hivi?
21
Mfinyanzi haufanyishi udongo, kama anavyotaka? Donge lililo moja upande mmoja haliumbi kuwa chombo kizuri, nao upande mwingine kuwa kibaya?
22
Inakuwaje? Ni kweli, Mungu anataka kuyaonyesha makali yake, tena anataka kuutambulisha uwezo wake, lakini kwa uvumilivu wake mwingi aliwavumilia walio vyombo vitakavyo makali tu, vilivyotengenezwa, viangamie tu.
23
Kisha anataka kuutambulisha hata wingi wa utukufu wake kwao walio vyombo vitakavyo huruma, ndio, aliowapatia utukufu kale;
24
nao ndio, aliowaita kwenye Wayuda nako kwenye wamizimu, nasi tumo.
25
Ndivyo, anavyosema hata kinywani mwa Hosea: Aliitwa: Si ukoo wangu nitamwita: Ukoo wangu, naye asiyependwa nitamwita Mpendwa.
26
Itakuwa hapo, hao wanaoambiwa sasa: Ninyi ham ukoo wangu, waambiwe: M wanawe Mungu aliye Mwenye uzima.
27
Naye Yesaya anawasemea Waisiraeli na kupaza sauti: Wana wa Waisiraeli ijapo wawe wengi kama mchanga wa ufukoni, watakaookoka watakuwa sao tu.
28
Kwani Bwana ndiye atakayevimaliza, atakapolitimiza Neno lake nchini kwa kulikata.
29
Navyo ndivyo, Yesaya alivyosema kale: Bwana Mwenye vikosi kama asingalitusazia uzao, tungalikuwa kama Sodomu, tungalifanana na Gomora.
30
Basi, tusemeje? Ni hivi: Wamizimu wasiofuata wongofu wamepata wongofu; ni wongofu ule unaopatikana kwa kumtegemea Mungu.
31
Lakini Waisiraeli walioyafuata Maonyo yenye wongufu hawakuyafikia hayo Maonyo.
32
Kwa sababu gani? Kwa sababu walikataa kumtegemea Mungu, wakafanya mambo yao tu. Wakajigonga katika lile jiwe la kujigongea,
33
kama ilivyoandikwa: Tazama, naweka humo Sioni jiwe la kujigongea na mwamba wa kujikwalia. Naye alitegemeaye hatatwezeka.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16