bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 14
Romans 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 15 →
1
Aliye mnyonge wa kumtegemea Bwana mpokeeni pasipo kubishana naye mawazo ya moyo!
2
Mwingine anayategemea ya kwamba: Vyote vinaliwa; mwingine aliye mnyonge hula maboga tu.
3
Mwenye kula asimbeze asiyekula! Wala asiyekula asimwumbue mwenye kula! Kwani Mungu amempokea.
4
Wewe u nani ukimwumbua mtumishi wa mwingine? Akiwa amesimama au akiwa ameanguka, yote humfanyizia Bwana wake mwenyewe. Lakini atainuliwa, kwani Bwana anaweza kumwinua.
5
Mwingine huchagulia siku za kuzitakasa, mwingine huzitakasa siku zote. Kila mtu sharti afulize kuyafuata, aliyoyatambua yeye kuwa ya kweli!
6
Anayezishika siku humshikia Bwana; naye asiyezishika hazishiki kwa ajili yake Bwana. Naye anayekula humlia Bwana, kwani humshukuru Mungu. Naye asiyekula hali kwa ajili yake Bwana, maana naye humshukuru Mungu.
7
Kwani kwetu hakuna anayejikalia mwenyewe, wala hakuna anayejifia mwenyewe.
8
Kwani tunapokaa humkalia Bwana, tena tunapokufa humfia Bwana. Basi, ikiwa twakaa au ikiwa twafa, sisi tu wa Bwana.
9
Kwani kwa hiyo Kristo alikufa, akawa mzima tena, apate kuwatawala waliokufa nao wanaoishi.*
10
Lakini wewe unamwumbuaje ndugu yako? Au wewe unambezaje ndugu yako? Kwani sisi sote tutatokezwa mbele ya kiti cha uamuzi cha Mungu.
11
Kwani imeandikwa: Bwana anasema: Kwa hivyo, nilivyo Mwenye uzima, wote watanipigia magoti, nazo ndimi zote zitamwungama Mungu.
12
Basi, kwa hiyo sisi sote kila mmoja atajisemea mwenyewe mbele ya Mungu.
13
Basi, tusiumbuane wenyewe tena, ila mjue, ya kuwa ni kuumbua, mtu akimtegea ndugu yake, ajigonge au ajikwae!
14
Nimeyajua, nikayashika kabisa moyoni kwa kuwa na Bwana Yesu, ya kuwa: hakuna kilicho chenye mwiko hivyo, kilivyo; lakini mtu akikiwazia kuwa chenye mwiko, basi, kwake yeye ni chenye mwiko.
15
Lakini ndugu yako akisikitishwa, wewe ukila, basi, umekwisha kuuacha upendo. Tena ukila usimponze mwenzio, ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
16
Yaliyo mema kwenu yaangalieni, yasibezwe!
17
Kwani ufalme wake Mungu sio kula na kunywa, ila wongofu na utengemano na ushangilio unaopatikana katika Roho takatifu.
18
Kwani anayemtumikia Kristo na kuyatenda mambo haya humfalia Mungu, tena hupendwa na watu.
19
Basi, kwa hiyo tukaze kuyafuata mambo yanayopatanisha, ni yaleyale yanayotujenganisha!
20
Usiitengue kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula! Kweli, vyote hutakata; lakini mtu akivila na kujikwaa, vimekwisha kumponza.
21
Ni vizuri, usile nyama, wala usinywe pombe, wala usifanye cho chote kinachomkwaza ndugu yako.
22
Wewe unayoyategemea moyoni, yategemee hata mbele ya Mungu! Mwenye shangwe ni yule asiyejipatia hukumu kwa ajili yao yale, aliyoyaona kuwa ya kufaa.
23
Lakini mtu akila mwenye mashaka amekwisha kujipatia hukumu, kwani hakula kwa kumtegemea Mungu. Nayo yote, mtu anayoyafanya pasipo kumtegemea Mungu, ndiyo makosa.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16