bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 13
Romans 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 14 →
1
*Kila mtu na autii ukuu! Maana uko na nguvu kumpita yeye. Kwani hakuna ukuu usiotoka kwa Mungu; nao wote ulioko umewekwa na Mungu.
2
Kwa hiyo mwenye kuubisha ukuu hulibisha tengenezo lake Mungu. Lakini wabishi watajipatia hukumu.
3
Kwani wenye nguvu hawaogopeshi, ukifanya mema, ila ukifanya maovu. Nawe usipotaka kuuogopa ukuu, fanya yaliyo mema! Hivyo utapata kusifiwa nao.
4
Kwani ukuu humtumikia Mungu, ukupatie mema. Lakini unapofanya maovu ogopa! maana haushiki upanga bure tu. Kwani humtumikia Mungu, humlipiza kwa ukali kila afanyaye kiovu.
5
Kwa hiyo inatupasa kutii, si kwa ajili ya ukali tu, ila hata kwa ajili ya mioyo, itung'ae.
6
Kwa hiyo mnatoa hata kodi, kwani wao ni watumishi wa Mungu wanaoifuliza kazi hiihii tu.
7
Basi, walipeni wote yawapasayo: Mtoza kodi mpeni kodi yake! Mwenye kuchanga mpeni chango lake! Mwenye kuogopesha mwogopeni! Mwenye kuheshimiwa mheshimuni!
8
Msiwe wadeni wa mtu ye yote, isipokuwa wa kupendana! Kwani anayempenda mwenziwe ameyatimiza Maonyo.
9
Kwani kule kwamba: Usizini! Usiue! Usiibe! Usishuhudie uwongo! Usitamani! na kama liko agizo jingine, yanaunganika yote katika neno hili: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe!
10
Ukimpenda mwenzio huwezi kumfanyia kiovu. Kwa hiyo kupendana ndiko kuyatimiza Maonyo.*
11
*Fanyeni hivyo mkizijua siku hizi, kwamba saa imekwisha fika ya kuamka katika usingizi! Maana wokovu wetu sasa uko karibu kuliko siku zile, tulipoanza kumtegemea Bwana.
12
Usiku umefikia kucha, mchana upambazuke: kwa hiyo tuziache kazi za giza, tujivike mata ya mwanga!
13
Tushike mwenendo upasao mchana! Tusiwe walafi na walevi, wala wagoni na waasherati, wala wagomvi na wenye wivu!
14
Ila jivikeni Bwana Yesu Kristo! Itunzeni miili yenu na kuiangalia, isishindwe na tamaa!*
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16