bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Romans 11
Romans 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 12 →
1
Basi, niseme: Mungu aliwatupa walio ukoo wake? La, sivyo! Kwani hata mimi ni Mwisiraeli, ni wa uzao wake Aburahamu, ni wa shina la Benyamini.
2
Mungu hakuwatupa walio ukoo wake, aliowatambua kale. Au hamyajui, Maandiko yanayoyasema, Elia alipomlalamikia Mungu kwa ajili ya Waisiraeli?
3
Akasema: Bwana, wafumbuaji wako wamewaua, wakapabomoa pote pa kukutambikia, nikasalia mimi peke yangu, tena roho yangu nayo wanaitafuta, waichukue.
4
Lakini jibu la Mungu linamwambia nini? Nimejisazia watu 7000 wasiompigia Baali magoti.
5
Basi, vivyo hata siku hizi za sasa liko sazo lililochaguliwa kupata magawio.
6
Lakini yakiwa magawio, siyo malipo ya matendo. Kama sivyo, magawio hayangekuwa magawio, kwani kama huko ni kulipa matendo, siko kugawia; kama sivyo, matendo yangekuwa ya bure.
7
Basi inakuwaje? Waisiraeli waliyoyatafuta, hawakuyafikia, lakini wachaguliwao tu ndio walioyafikia. Lakini wale wengine walishupazwa mioyoni mwao, kama ilivyoandikwa:
8
Mungu aliwapa roho ya usingizi na macho yasiyoona na masikio yasiyosikia mpaka siku hii ya leo.
9
Naye Dawidi anasema: Sharti meza zao ziwawie matanzi na mitego, wanaswe, walipizwe mabaya yao.
10
Macho yao na yatiwe giza, wasione, migongo yao nayo ipindike siku zao zote!
11
Basi, niseme: Walijikwalia, waanguke tu? La, sivyo! Ila maanguko yao yamewaletea wamizimu wokovu, wenyewe wawaonee wivu, wapate kujikaza.
12
Lakini maanguko yao yakiwa yameuletea ulimwengu mapato mengi, nako kushindwa kwao kukiwa kumewaletea wamizimu mapato mengi, je? Hapo, watakapokuja wote, hayo mapato hayataongezeka sanasana?
13
Nasema nanyi mlio wamizimu. Mimi kwa hivyo, nilivyo mtume wa wamizimu, na niutukuze utumishi wangu!
14
Hivyo labda nitawatia wivu walio ndugu zangu kimtu, nipate kuwaokoa mmojammoja.
15
Kwani hapo walipotupwa waliwapatia wao wa ulimwengu wokovu; basi, hapo watakapopokelewa watawapatia nini, isipokuwa kufufuka na kutoka penye wafu?
16
Tena limbuko likiwa linatakata, limbiko nalo litatakata. Tena shina likiwa limetakata, matawi nayo yatatakata.
17
Lakini kama yako matawi yaliyovunjwa na kuondolewa, kisha wewe uliye mdanzi tu ukatiwa mahali pao, ukagawiwa fungu lako la shina na utomvu wa ule mchungwa,
18
usijivune kwao yale matawi! Lakini ukijivuna ujue: si wewe unaolipa shina nguvu, ila shina linakupa nguvu wewe!
19
Labda utasema: Matawi yalivunjiwa mimi, nipate pa kutiwa.
20
Ni vizuri; yalivunjika mle, kwa ajili hayakushikamana; wewe nawe ukashinda mle kwa nguvu ya kushikamana. Usijikweze, ila uogope!
21
Kwani Mungu kama asivyoyaonea uchungu yale matawi yaliyochipukia mlemle, hata wewe hatakuonea uchungu.
22
Basi, humo utazame utu na ukali wake Mungu! Ukali uko kwao walioanguka, lakini kwako wewe uko utu wake Mungu, ukifuliza kuukalia huo utu. Ikiwa sivyo, hata wewe utakatwa.
23
Nao wale watatiwa tena, wasipofuliza kuukalia ukatavu; maana Mungu yuko na nguvu ya kuwatia mle tena.
24
Tazama: Wewe ulichipuka katika mdanzi, kisha ukakatwa humo, ukatiwa katika mchungwa usio shina lako; basi, wale waliochipukia mlemle, ni vigumu gani kuwatia tena katika mchungwa wao wenyewe?
25
Kwani sitaki, ndugu, mkose kulijua fumbo hili, mkajiwazia wenyewe kuwa wenye akili. Waisiraeli wengine wao wameshupazwa mioyoni, mpaka wingi wa wamizimu utakapokwisha kuingia.
26
Hivyo ndivyo, Waisiraeli wote watakavyookoka, kama ilivyoandikwa: Mle Sioni atatokea mponya; ndiye atakayemgeuza Yakobo, aache mabezo.
27
Nalo hili ni agano, ninalolifanya nao: Nitayaondoa makosa yao.
28
Kwa hivyo, wanavyoukataa Utume mwema, ndio wachukivu kwa ajili yenu; lakini kwa hivyo, walivyochaguliwa, ndio wapendwa kwa ajili ya baba zao.
29
Kwani Mungu hayajutii magawio na wito wake.
30
Kama ninyi: Kale mlimkataa Mungu, lakini sasa mmehurumiwa kwa ajili ya ukatavu wao hao;
31
vivyo hivyo hata hao sasa wameikataa ile huruma iliyowatokea, kwamba nao siku ziwafikie, watakapohurumiwa.
32
Kwani Mungu aliwaunga wote pia, wamkatae, apate kuwahurumia wote.
33
*Tazameni, jinsi ujuzi na utambuzi wake Mungu unavyofurika kuwa mwingi! Kweli maamuzi yake hayachunguziki, njia zake nazo hazinyatiliki!
34
Kwani yuko nani aliyeyatambua mawazo ya Bwana? Au yuko nani aliyekula njama naye?
35
Au yuko nani aliyeanza kumpa kitu, apate kulipwa naye?
36
Kwani yote yalitoka kwake yeye, yakafanywa naye yeye, tena yatarudi kwake yeye. Yeye ndiye atakayetukuzwa kale na kale. Amin.*
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16